Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu kwanza sitaki uniombe radhi,pili mimi sio mtoto mdogo nilete uongo kwwnye habari amabyo inagusa maisha ya watu, hii habari ni ya kweli,na ndio maana ukiangalia post yangu imekupa maelezo ya kutosha sana, tembelea web ya TAMISEMI utakiona ninacho kuambia
Ahsante
Kweli mkuu. Mimi ni mtu mzima. Nimefanya kosa japo si kwa kukusudia. Naomba unisamehe. Niliingia kwa makosa. Nadhani ni uchovu. Ila baada ya kukosolewa na mwingine nimerudia na nimeona taarifa yenyewe. Nimekosa kukuchukulia kama wale wanaotoa mzaha tangia hili jambo lilipoanza. Tafadhali usinikasirikie ndugu yangu. BASI NITARUDI NCHINI KUJIPANGA NA HAYO MAPYA JAPO KAZI IPO.
Aksante mungu! Coz nimechoka kufuga MAKUKU!
hii ajira au uchafu!...kuliko kuwa mwalimu ni bora nikavue samaki. Mshahara wenu wa mwezi mimi natumia siku moja!..teh!teh!...bongo ni majangaz you know!
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA AJIRA KWA WALIMU WAPYA MWAKA 2013/14
Jumla ya Walimu wapya 36,021 ambao wamehitimu mwaka 2013 kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini wataajiriwa rasmi na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri) ifikapo tarehe 01 Aprili 2014. Kati ya idadi hiyo walimu wa ngazi ya Cheti (Daraja III A) ambao hufundisha katika shule za Msingi ni 17,928 na walimu wa shule za sekondari ni 18,093 (wakiwemo 5,416 wa Stashahada na 12,677 wenye shahada).
Orodha rasmi ya walimu wapya ikionesha Halmashauri mbalimbali walikopangwa itatangazwa kwenye tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (PMORALG | Prime Minister's Office - Regional Administration and Local Government) na ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training) ifikapo tarehe 15 Machi, 2014.
Walimu wote wapya wanatakiwa kuripoti bila kukosa kwenye Halmashauri walikopangiwa ifikapo tarehe 01 Aprili, 2014 ili waanze kazi mara moja.
Inasisitizwa kwamba walimu waripoti tarehe hiyo ili taarifa zao za kiutumishi zifanyiwe kazi na Waajiri wao yaani Wakurugenzi ili kuwawezesha kupata mshahara mwezi Aprili 2014 na hivyo kuepuka ulimbikizaji wa mshahara kwa watumishi wapya wanaoanza ajira.
Mwalimu yoyote ambaye ataripoti baada ya tarehe 10 Aprili, 2014 bila sababu za msingi zinazokubalika kiutumishi atakuwa amepoteza nafasi hiyo.
Ikumbukwe kwamba Upangaji wa Walimu wapya kwenye Halmashauri umezingatia uwepo wa mahitaji ya walimu. Vile vile, fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba na nauli ambazo zitalipwa kwa kila mwalimu atakayeripoti kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali zimetumwa kwenye Halmashauri walikopangwa walimu hao. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kwenda kuripoti katika Halmashauri alikopangwa.
Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haitafanya mabadiliko yoyote ya vituo vya kufanya kazi walimu wapya isipokuwa kwa utaratibu wa kawaida wa uhamisho baada ya mwalimu kutimiza vigezo na masharti ya uhamisho.
Ni vema ifahamike kuwa ajira zinazotangazwa ni za walimu wapya. Walimu ambao tayari ni watumishi umma waliokuwa vyuoni kwa ajili ya kujiendeleza kielimu na hivi sasa wamehitimu mafunzo yao, wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao
Hata ningekuwa mwalimu kazi ya ualimu siitaki labda nje ya tz
hii ajira au uchafu!...kuliko kuwa mwalimu ni bora nikavue samaki. Mshahara wenu wa mwezi mimi natumia siku moja!..teh!teh!...bongo ni majangaz you know!
Majina ln wanatoa
Labda jambazi