Riskytaker
JF-Expert Member
- Mar 14, 2024
- 568
- 2,522
Serikali imekuwa ikitangaza ajira lakini mara kwa mara matokeo hayalingani na ahadi. hii ni kwakada zote
Hivi karibuni, tumeshuhudia uajiri wa walimu 6,000 badala ya 14,000 waliotarajiwa, bila maelezo ya kina kuhusu upungufu huo.
Hii ni dalili ya ukosefu wa uwazi na kutowajibika kwa wale wanaosimamia ajira hizi.
Katika dunia ya leo, hatuwezi kupoteza muda na michakato isiyoeleweka. tunashudia michakato ya ajira kuchuka hata miezi 6 bila sababu za msingi
Taifa linahitaji hatua madhubuti, si maneno matupu. Serikali inapaswa kueleza kwa uwazi: Je, kuna changamoto za bajeti? Kuna upendeleo au urasimu usio na tija? Au ni mazingira ya rushwa yanayozuia ajira hizi kutolewa kwa haki?
Hatuhitaji ahadi zisizotekelezeka wala ucheleweshaji usio na sababu. Kazi zitatangazwa, basi zitolewe kwa wakati! Mfumo wa ajira unapaswa kuwa wa wazi, wa haraka, na wenye tija kwa nchi. Serikali iwe makini—wananchi wanahitaji utekelezaji, si visingizio!
ikumbukwe hizi ajira zilitangazwa mwaka jana mwezi july
halafu ni vyema kama kuna changamoto sekratariet ya ajira ikatoka hadharani ikasema kuna sababu moja mbili tatu ambazo znapelekea situation nzima.