Ajira za walimu

Ajira za walimu

MAIKO EDMUND

New Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
2
Reaction score
5
MUGARULA PUBLIC SERVICE RECRUITMENT MODEL (MPSRM). ALL PROFESSIONS.

Summary: Direct placement of graduates based on minimum qualification (not exact), year of graduation and age successively in the lower ranks of the respective fields.

WAHITIMU NA FAMILIA ZAO WAPUNGUZIWE MATESO. SOMA 7&12(IV). Final Edition.

Sehemu ya kwanza: Upangaji vituo vya kazi.

1. Kupata kazi/ajira kwenye utumishi wa umma ni haki ya kila raia aliyetayari na mwenye sifa za msingi za fani husika.

2. Kama tunavyotambua safari ya masomo/elimu ni safari ya kujitoa kwa mali, muda na hali. Ni uwekezaji wa gharama na wa muda mrefu ambao unatarajiwa kuwa manufaa baada ya kuhitimu hasa kupitia ajira (kuajiriwa/kujiajiri). Kwa nchi yetu ambayo iko kwenye orodha nchi maskini au mara chache kuingia uchumi wa kati chini, elimu huziacha familia nyingi kwenye umaskini mkubwa baada ya kutumia rasilimali nyingi kufadhili elimu ya mtoto au watoto wao.

3. Mitaala yetu kwa kiwango kikubwa ni ya kuwawezesha zaidi wahitimu kujiariwa kuliko kujiari hivyo wahitimu kwa asilimia kubwa wanahitaji nafasi za kuajiriwa hasa serikalini. Kutokana na uchache wa nafasi zinazotangazwa serikalini, kupata nafasi hizo umekuwa ni uwekezaji mwingine ambao unaonekana kuwa ghali na wenye mateso mengi. Matumizi makubwa ya pesa (nauli, kulala, chakula), muda na usumbufu kwenye hatua zote ni mkubwa. Lakini usaili wa dakika 30-300 unafuta safari ya elimu ya zaidi ya miaka 15 aliyoitumia msailiwa kupata elimu husika. Hapa changamoto ni mfumo.

4. Kumekuwa na changamoto kubwa ya waajiri na jamii kulalamikia uwezo mdogo wa wahitimu kutoka vyuoni kinyume na ilivyotarajiwa. Mamlaka iweke nguvu ya ziada katika kudhibiti ubora wa mfumo wa ELIMU au VYUO kuliko kudhibiti wahitimu kupitia usaili.

5. Ajira kwa fani nyingi kama sio zote zimekuwa zikitolewa kwa mfumo wa usaili lakini zoezi hili linaficha madhaifu ya mfumo mzima wa elimu au vyuo na kurudisha lawama kwa matunda ya mfumo (wahitimu).

6. Kutokana na changamoto hizo mbili (i) madhaifu ya mfumo wa elimu/vyuo na (ii) gharama baada ya masomo zinazo endelea kufilisi wahitimu na familia zao ambazo naamini zinaendelea kufanyiwa kazi kwa ukaribu, suluhu ya kudumu kwenye kupata watumishi wa umma iwe kama ifuatavyo;

- Mosi, wahitimu wote kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali wawekwe kwenye kanzi data ya serikali kupitia vyuo husika na wahakikiwe au wajisajili wao wenyenye punde wanapohitimu, inaweza kuwa ajira portal au nyingine.

- Pili, kila nafasi zikipatikana kwenye vyeo vya chini vya fani husika, wahitimu wa fani hiyo wapangiwe vituo vya kazi na kwa maslahi (mshahara) ya vyeo hivyo vya chini bila ya usaili kwa kuangalia kiwango cha elimu cha chini kinachohitajika wenye zaidi yake wawe na nafasi, mwaka wa kuhitimu na umri.

- Tatu, nafasi kwenye vyeo vinavyofata kwa fani husika ndizo zitokane na usaili kwa wenye sifa waliokazini (transfer vacancies). Watumishi wapande vyeo vya juu na huku chini wengine waingie moja kwa moja (by default).

- Nne, nafasi zinazoachwa wazi baada ya usaili zijazwe moja kwa moja (by default) kutoka kwenye kanzi data ya wahitimu wanaosubiri ajira. Itakuwa rahisi kwa wahitimu kuweka matarajio ya ni lini atafikiwa kupitia kanzidata husika ambayo kila mhitimu ataweza kuwa akaunti huko hivyo kupunguziwa MATESO YA SASA.

  • Mfano nafasi iliyopo inahitaji wahitimu wenye Astashahada/Stashahada na tuna wahitimu wa shahada au zaidi wenye fani hiyo na walihitimu kabla basi wapangwe kwenye nafasi hizo kwa mshahara huo huo wa cheo husika.
  • Au nafasi iliyopo inahitaji wahitimu wenye kiwango cha elimu cha shahada, basi ITANGAZWE kama wapo wenye sifa hizo kwenye vyeo vya chini WAOMBE NA WASAILIWE, kama hawapo BASI WAHITIMU wakongwe ambao hawana kazi waliopo kwenye kanzi data wapewe nafasi hizo kwa maslahi (MSHAHARA) ya cheo kilichotagazwa, wapewe mafunzo.

7. Wapo wahitimu wameajiriwa sekta binafsi wanalipwa chini ya kima cha chini cha mshahara, wengine chini ya viwango vya mishahara vya serikali, wengine wanajitolea kwa posho ndogo hadi BURE nayo kupata nafasi au malipo ni kwa mbinde, kuwapa ajira rasmi kwa maslahi yaliyopo itakuwa vizuri kuliko kuachwa kwa sababu nyepesi ya elimu kubwa (over qualified), itawasaidia hata kukopesheka.

8. Kwa sababu tayari serikali imetangaza kuendesha usaili wa mchujo wa kuandika (written) kwenye vituo mbalimbali karibu kila mkoa kwa njia ya mtandao hivyo itakuwa rahisi zaidi kwa mwombaji aliyekazini kujigharimia na kupata ruhusa ya siku moja au mbili kuhudhuria usaiili huo wa mchujo.

9. Hii itasaidia serikali kutumia vizuri rasilimali watu, kuondoa gharama na usumbufu kwa wahitimu na familia zao (nchi maskini). Pia serikali itawajibika kuhakikisha vyuo vinatoa wahitimu wanaofikia umahiri unaotakiwa kuliko KUWAKWEPA kupitia mgongo wa usaili ambao umegeuka mateso.

10. Inafikirisha sana mhitimu kukaa mtaani kwa kigezo cha kuwa na sifa za juu (OVER qualified) kwa miaka zaidi ya saba huku waliohitimu baada yake wakiwa wanapata kazi au mhitimu kushindwa USAILI kwenye ajira za umma ina maana arudi chuo au kuna siku usaili utakuwa mwepesi kwake? Hujawahi kushindwa tangu Chekechea mpaka Chuo Kikuu, una miaka zaidi ya nane mtaani harafu usaili unakupiga (This Time Tomorrow….). Kuwa na elimu ya juu (over qualified) isiwe kama laana bali neema watu wahamasike kuipata.

11. Tukumbuke usaili una mambo mengi kuanzia msongo wa mawazo unaotokana na kukaa uraiani muda mrefu bila ajira/kazi ya kueleweka, gharama kubwa zinatumika kwenye mchakato wa usaili ambazo muda mwingine ni mkopo au umekausha mtaji na hujui itakuwaje, kusahau baada ya kukaa uraiani kwa muda mrefu, uwezo wa asili wa mhusika kujieleza, makosa ya kibinadamu, yasiyo ya kibinadamu na mengine mengi.

12. Mtindo huu wa MPSRM wa utoaji ajira katika utumishi wa umma una faida nyingi kwa mtu mmoja mmoja, jamii na Taifa kama ifuatvyo;

- Kwanza, Taifa na jamii itanufaika zaidi na wataalamu wake wote wenye sifa za ziada kwenye vyeo vya chini kulingana na elimu zao kwa kuongeza ufanisi kwenye nafasi za chini walizonazo kwa wakati huo huku wakishirikiana na kubadilisha ujuzi na uzoefu na wafanyakazi wenzao.

- Pili, kutunza utu wa wahitimu. Mahitaji ya msingi kwa binadamu wote ni sawa hivyo mhitimu kuanza na cheo cha chini kulingana na elimu yake na kwa maslahi yaliyopo itasaidia kumudu mahitaji ya msingi ya kila siku na hivyo kuwa salama.

- Tatu, itakuwa sehemu ya vijana kujitolea kujenga Taifa lao kupitia vipaji vyao vya kitaaluma, kupata uzoefu na kama Taifa kupata wataalamu wazuri wenye uzoefu kwenye ngazi za juu za vyombo vya maamuzi na watunga sera.

- Nne, nadharia hii italeta msawazo wa kifikra kwa vizazi kuwa hatua ya kwanza kazini kwa wote ni sawa na kupanda (cheo/maslahi) ni jitihada binafsi za ziada za kielimu, ufanisi na uzoefu kazini. WANAJESHI WOTE WANAANZIA UKURUTA (WADUDU) ILA SIO WOTE HUFIKIA UKUU WA JESHI, HAWAJAWAHI KUKWAMA.

13. Mwisho si kwa umuhimu, wahitimu wanaohudumia nafasi za chini kulingana elimu yao wapewe unafuu fulani mfano kutokatwa mikopo ya elimu ya juu mpaka watakapofikia vyeo wanavyostahili kulingana na elimu yao.

14. Tuendelee kuombea mambo yafuatayo;
  • Uhusiano wa waajiri na waajiriwa wanaoacha kazi kwa muda na kwenda kufanya usaili.
  • Hadhi ya walimu ambao hawakufanikiwa kupata kazi serikalini kwa wanafunzi wao.
  • Hadhi ya walimu waliofeli usaili ndani ya jamii. Kote duniani fani yenyewe imekuwa ikisika kama THE LAST OPTION PROFESSION for failures (low performing), poor and lower middle class except few with passion and with special duties. The global status and society’s perception on education profession.
  • Ustahimilivu wa wahitimu na familia zao kutokana ongezeko la umaskini uliotokana na mchakato wa usaili. Matumizi makubwa ya pesa (chakula, nauli na malazi n.k) wanayotumia wasailiwa wote ni bilioni kadhaa. Ni uwekezaji baada ya uwekezaji wa miaka mingi mpaka kuhitimu. Wengine kushindwa kuhudhuria kwa sababu za kifedha.

15. THEORETICAL FRAMEWORK (FUMO WA KINADHARIA);
Utilitarian theory (By Jeremy Bentham & John Stuart in 18th & 19th century) – An ethical theory that determines right or wrong by focusing on outcomes (education system outputs). It insists on actions that maximize happiness and well-being for the affected individuals (having fair recruitment model of system outputs). The state should ensure happiness and well-being to the greatest number of people from its actions.

16. WAHITIMU NA FAMILIA ZAO WAPUNGUZIWE MATESO.

lameckmethod@gmail.com (+255 759648187)
KYERWA-KAGERA-TANZANIA
Jumamosi 15/07/2023.

#StoriesOfChange2024
#MawazoBoraNaEndelevu
 
"Wengi wanaamini ajira bila connection haipatikani, ndio maana sisi wabunge ni mashahidi, kila mbunge kwenye jimbo lake ana meseji lukuki za kuombwa kusaidia watu wapate ajira..kwa hiyo watu wanaoajiriwa kwa kuamini connection ndio imewapa ajira, wanapoingia ofisini wanaenda kufanya kazi kwa connection hizo hizo..." - Mbunge wa Sumve, Kasalali Emmanuel Mageni.
 
Back
Top Bottom