Hamjambo wana JF?Katika upembuzi wangu niliofanya kwenye hizi ajira za Walimu nimegundua kwamba,walimu wa masomo ya Sayansi kama vile Physics,Chemistry,Maths na Biology ni wachache sana!Hii ina maana kwamba masomo hayo yanaogopwa sana siku hizi.Serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi kurekebisha hali hiyo.Naomba maoni yenu Wana JF.