Ajira za walimu

Ajira za walimu

manyata

Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
41
Reaction score
6
Hamjambo wana JF?Katika upembuzi wangu niliofanya kwenye hizi ajira za Walimu nimegundua kwamba,walimu wa masomo ya Sayansi kama vile Physics,Chemistry,Maths na Biology ni wachache sana!Hii ina maana kwamba masomo hayo yanaogopwa sana siku hizi.Serikali haina budi kuchukua hatua za makusudi kurekebisha hali hiyo.Naomba maoni yenu Wana JF.
 
Uhaba wa walimu wa sayansi utadumu sana kwani hawapewi umuhimu unaopasa. Laiti wangepewa motisha sawa na mainjinia na madaktari wanafunzi wangehamasika kuyasoma masomo hayo na uhaba wao usingeonekana tishio. Tatizo kubwa ni la hawa wanasiasa kuwa bias kwa kuwa wao walisoma masomo ya sanaa so hawaoni umuhimu wa sayansi. Hebu wabadilike kwa kuyapa masomo ya sayansi kipaumbele namba moja!
 
Uhaba huo hautadumu sana. Wizara ya Elimu imekuja na crash program kwa akili ya kusaka waalimu wa sayansi. Inaweza kuchukua muda mpaka hapo shule za kata zitakapoimarika na kuandaa wanafunzi watakaofaulu masomo hayo. Kituu kinachoweza kukwamisha kasi ni utitiri wa shule za kata. Shule za kata hazina mazingira rafiki kwa sayansi, hivyo wanafunzi wengi hukata tamaa kujiunga, wachache wanaojiugnga hufeli.
 
Kumbe wanasiasa wamesoma masomo ya sanaa?! Ndio nimejua leo hii. Hembu nitajie masomo aliyosoma Ndungai, Mwandosya, sarungi, Magufuli, kawambwa, hussein Mwinyi, kigwangalla, billali, prof msola, shein na wengine wengi. Ukifika mwisho wa kudodosa majina hayo njoo useme kwamba wanasayansi wanadharauliwa kwa kuwa vigogo wamesoma sanaa. Kama kila mtu atavutia hoja kwake basi nyerere angewafanya walimu kuwa matajiri kwa kuwa yeye alitoka kundi hilo. Ugumu wa somo fulani ni kwa mtu husika wala si kweli kwamba sayansi ni ngumu kuliko sanaa. Angalia shule za kata wanafunzi wanafanya vyema masomo ya sayansi kuliko yale ya sanaa hasa Geography,je ugumu na urahisi umetoka wapi sasa?
 
Kwa WALIMU WAPYA 2013/14. Unahitaji kuhama na umepangiwa Singida wilaya mpya ya Mkalama.. kunanafasi ya kubadilisha hama toka Mkalamma nenda wilaya ya Iramba singida. Wahi mapema, piga namba hizi 0769581662 au 0782850113. Iramba ni kuzuri kuliko Mkalama.
 
Anae taka kwenda Tarime mji na mimi niende Geita mji au vijijini. Piga 0768074472
 
Back
Top Bottom