Kumbe wanasiasa wamesoma masomo ya sanaa?! Ndio nimejua leo hii. Hembu nitajie masomo aliyosoma Ndungai, Mwandosya, sarungi, Magufuli, kawambwa, hussein Mwinyi, kigwangalla, billali, prof msola, shein na wengine wengi. Ukifika mwisho wa kudodosa majina hayo njoo useme kwamba wanasayansi wanadharauliwa kwa kuwa vigogo wamesoma sanaa. Kama kila mtu atavutia hoja kwake basi nyerere angewafanya walimu kuwa matajiri kwa kuwa yeye alitoka kundi hilo. Ugumu wa somo fulani ni kwa mtu husika wala si kweli kwamba sayansi ni ngumu kuliko sanaa. Angalia shule za kata wanafunzi wanafanya vyema masomo ya sayansi kuliko yale ya sanaa hasa Geography,je ugumu na urahisi umetoka wapi sasa?