SoC02 Ajira zipo lakini ni ngumu kumeza. Mapinduzi kwenye Elimu yanahitajika

SoC02 Ajira zipo lakini ni ngumu kumeza. Mapinduzi kwenye Elimu yanahitajika

Stories of Change - 2022 Competition

Iman Anyandwile

New Member
Joined
Feb 25, 2019
Posts
2
Reaction score
1
Ni Tanzania, mahala ambapo rasilimali zimezagaa lakini hakuna anaejua namna ya kuzifaidi. Watoto wanapelekwa darasani ili waweze kutwaa maarifa yanayoweza kuwasaidia kunufaika na rasilimali lakini nani ajuaye kuwa hata yule mwalimu amfundishaye mtoto nae hajui namna sahihi ya kutwaa utajiri huo unaowazunguka bali anafundisha kwa mujibu wa mtihani wa taifa.

Ni wazi leo hii hapa kwetu tunaomba serikali kubadili miundombinu ya shule zetu kama vile madarasa ya kisasa, Vyoo, madawati, mazingira ya kuvutia, na walau kuwepo tehama ni jambo zuri lakini ni wachache huwa wao wanashinikiza kubadili mzizi mkuu wa elimu yaani mtaala wa elimu kiujumla kwani hata kama miundombinu itabadilishwa halafu mtaala ukaachwa ni wazi kuwa bado shida ya ujinga itaendelea kulikumba taifa kwani mtaala mzima wa elimu yetu huwa umejikita kwenye kumuandaa mwanafunzi kwaajili ya mtihani wa mwisho afaulu ili wizara husika pamoja na viongozi wa nchi wapewe sifa kwa kuongeza ufaulu. Lakini wanasahau lengo kuu la elimu kwenye kuondoa ujinga na kumuandaa mwanafunzi kupambana na mazingira wala siyo vinginevyo. Baadaye inashindikana kumuandaa mwanafunzi ili aje kupambana na mazingiza yanayomzunguka, bali anaandaliwa mwanafunzi mwenye madaraja ya kutisha yaani ufaulu wa juu lakin hajui chochote kuhusu namna ya kutumia taaluma yake kutatua changamoto zinazomkabili ikiwemo kupata kipato binafsi kupitia taaluma yake pasi na kutegemea kuajiliwa na serikali hivyo kuleta mlundikano wa wasomi mtaani wasio na kazi...

Ni wakati sahihi sasa mapinduzi kwenye Elimu yanahitajika. Serikali ifanye yafuatayo kuleta ahueni kwa vijana huku mitaani.

Kwanza kabisa taasisi ya elimu kabla ya kumshinikiza mzazi ampeleke mtoto shule basi wao kama taasisi ni wajibu wao kujua mahala ambapo watampeleka huyo mtoto baada ya kusomeshwa sio tena kumtelekeza.

Pili taasisi ya elimu inapaswa kuangalia ni namna ipi itatumika kupunguza idadi wasomi wapya nchini. Hii ni njia sahihi ambayo itasaidia kupata wahitimu wenye taaluma wachache ambao serikali inaweza kuwamudu. Njia ya kupunguza wasomi ni pamoja na kufanya (standardization) kwenye mitihani yaani mitihani migumu kama ile ya miaka ya 90 huko ili kupata wataalamu wachache. Hii ni vizuri ikatumika kuanzia darasa la 7 ili kumpata form one aliye imarika mpka chuoni ni mchujo huo huo.

Je, wale waliochunjwa na kufeli wataenda wapi? Ni muda sahihi utakuepo kwa serikali kutoa vipaumbele kwenye taasisi za ufundi stadi, kilimo, michezo na sanaa kwani itakuwa kama darasa la mchujo kwao. Ikumbukwe enzi za ukoloni, mtu akihitim vizuri darasa la saba (standard VII entry examination) basi anaangaliwa kwenye kazi za kuvalia suti na tie, lakini kwa wale waliokuwa wanafeli hawakutupwa ila walipewa nafasi kwenye Ualimu, unesi na usaidizi (secretary) hivyo serikali inapaswa kuandaa mbadala wa ajira ili kuhakikisha kila mwananchi anafaidi mema ya nchi hii tajiri siyo wafaidi wao peke yao kila mtu anatamani kula.

Pia, Serikali inapaswa kurejea jedwari la mishahara kwa watumishi wa umma, kwani hakuna uwiano wowote kwa baadhi ya taasisi. Mfani mzuri mbunge hana sababu yoyote ya kulipwa milion zaid za 10 kwa mwezi huku aliyemfanya awe mbuge akila chini ya laki 5 kwa mwezi. Ni muda serikali iweke uwiano mzuri japo sio lazima ukawa sawasawa kwa kila mtumishi. Mshahara wa kimo cha mwisho ukawe si chini ya laki 8 kwa mwezi huku ule wa kimo cha juu ukiwa si zaidi ya milion 5 kwa mwezi hata kwa raisi nae(inclusive). Hii itawapa wengi fursa za ajira kwani ile milundikano ya mamilioni iliyotakiwa kulipwa kwa mtumishi mmoja basi inaajiri watumishi wengine.

Serikali kupitia taasisi ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu basi inatakiwa kutoa fedha za kutosha ili wanafunzi kwa namna nyingine wapate kama mitaji ya kufanyia biashara na kilimo. Na isiwe ombi (application), iwe ni wajibu wa bodi kumuwezesha kila mwafunzi aliyehitimu kidato cha 6 kunufaika na fedha hizo na hazipaswi kurejeshwa kwani ni moja kati ya motisha iliyowafanya wafike hapo.Mwanafunzi wa chuo ni muda sasa wakupewa walau zaidi ya laki 5 kila mwezi ili aweze kujikimu na kujiongeza hivyo kupunguza lawama kwa Serikali.

Tanzania sasa ni wasaa wa kuwa na atleast chuo kimoja cha taaluma. Mfano chuo kimoja cha taaluma ya ualimu chenye kuzalisha waalimu sio zaid ya elfu moja kila mwaka ili kuondoa mlundikano wa waalimu mtaan. Mwalimu nimemuweka kama mfano kwani ni taasis inayoongoza kuwa na jobless wengi hivyo basi sio ualimu tu bali vyuo vyote vijikite kwenye kuzalisha fani husika pasipo na michanganyo. Mfano IFM izalishe watu wa fedha tu nao ni kwa kuzingatia uhitaji wa soko la ajira, hivyo hivyo kwa SuA, NIT na vyuo vinginevyo.

Muhimu zaidi ni kwa serikali kuingia mikataba ya lazima na kwa muda mfupi na wafanyakazi. Serikali inapaswa kumlipa mfanyakazi mshahara mkubwa kwa mwezi kulingana na taalum yake lakini mfanyakazi huyo hatakiwi kudumu kwa muda mrefu unaozidi miaka 10-15. Ajiri wafanyakazi kwa mkataba wa miaka 10 baada ya mkataba kuisha basi kijana ajira yake nayo itaishia hapo. Lakini awe analipwa vizuri na hakuta kuwa na mafao (pension) baada ya ukomo wa mkataba. Hii itamsaidia kwenda kujiendeleza kwani tayari ameonja mema ya nchi hivyo anaachia njia kwa vijana wenzake kupata fursa kama yake. Hii itaweka njia wazi kwa wahitimu wengine kupata nafasi nyingi zaidi kwenye ajira.

Pia, Elimu haipaswi kuwa bure hata kidogo, Wizara ya Elimu kuweka elimu bure sio kuongeza enrollment bali ni kuikandamiza taasisi. Hivyo ni muhimu huweka tozo kwenye elimu ili kuwavutia wenye nia kwani itasaidia kuondoa mlundikano wa wanafunzi madarasani.

Yamesemwa yote hayo, lakini kuyatekeleza inahitaji kiongozi aliyejitoa ufahamu na kuziba masikio kwani si rahisi kuyafanya haya kwa akili za kawaida na najua kutakuwa na lawama pamoja na laana kwa kiongozi yeyote atakayethubutu kutekeleza hayo.
 
Upvote 2
Basi huu umekua mjadara mkubwa sana mfumo wa Elimu kubadilishwa , lkn utabadilishwa vip , na wafanye vip yanaelezwa shida ni utekelezaji.
 
Pia ishu ni kubadilishwa kwa viongozi wa elimu mfano mawazili. Kabla wazili hajatimiza malengo alojiwekea anatolewa na wanaanza upya. Hii si sawa
 
Hapa Abraar Education Centre tuliliona hilo tatizo mapema na tunashukuru tukaamua tusingoje kupatiwa ufumbuzi na mtu bali tujitume wenyewe na tuanzishe shule/masomo yanayolenga kumjenga mwanafunzi kujitegemea kwa kutoa masomo ya fani tofauti tofauti kwa vitendo.

Pia tunatoa uzoefu wa kazi na fani tofauti kwa wahitimu wote wa vyuo / shue ambao hawafahamu wapi pakuanzia au wapi pakupatia ujuzi ujuzi hapa kwetu wana fursa za kujijengea ujuzi kwa vitendo. Na wale walioacha/achishwa kazi ambao wanasaga viatu tuna mpango tunaouita (Abraar stepping stone) ambao umempa ahueni au kumwezesha mtafuta kazi pa kupumulia wakati tunasaidiana kumtafutia cha kufanya.

Mwenyezi Mungu amejaalia nia zetu na ndani ya muda mfupi sana toka tuanzishe madarasa yetu ya Abraar (waja wema) hivi sasa tunajivunia madarasa ya watu wazima na watoto yanayofundisha fani na stadi mbali mbali kwa vitendo.

Pitia nyuzi zetu ujionee hatua tunazopiga na matunda mema yameanza kuonekana waziwazi; https://www.jamiiforums.com/find-threads/started
 
Back
Top Bottom