Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Ili kuboresha utendaji na weledi wa Jeshi la Polisi nchini ni vyema serikali ikaweka kigezo cha elimu kama kipaumbele kwa ngazi zote za polisi.Hii ni kutokana na umuhimu na unyeti wa kazi za ulinzi wa usalama wa raia na mali zao.
Waajiriwe vijana waliomaliza diploma, digrii na masters tu katika jeshi la polisi. Hakuna sababu tena ya kuendelea kuajiri watu ambao hawajafika kiwango hicho cha elimu kama tunajinasibu tunaipa elimu kipaumbele katika nchi yetu, pia vijana wa ngazi hizo za elimu wamejaa mitaani wakizurura na bahasha zao kutafuta ajira na wengine wameanza kuendesha boda boda kitu ambacho ni matumizi mabaya ya rasilimali watu.
Tulifanye jeshi la polisi kuwa la kisasa kwa kuipa elimu kipaumbele katika ajira zake kwani inawezekana.