Carica_papaya
JF-Expert Member
- Nov 22, 2018
- 767
- 1,272
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
MBOWE, magufuli na samia nawazoom tuGTs,
Hakika ukiyasikia ya miaka hii ya utumishi wa umma na kustaafu utashangaa hivi kwanini watu wanang’ang’ania ofisini baada ya muda wa utumishi kuisha?
Kuna mtumishi mmoja hapa Dar alistaafu kwenye taasisi moja ya umma, akaongezewa mkataba kwa mfululizo miaka miwili, mwaka wa tatu wakamkatalia, ila yeye akalazimishq dereva awe ana mfuata, baadaye dereva akazuiwa na ofisi basi njemba akawa anajiendesha mwenyewe na akajiwekea kiti ofisini. Aliendelea na huo mtindo mpaka akafariki mwezi wa nne mwaka huu baada ya mapumziko ya Pasaka.
Hii inamaanisha nini??
Ninavyoona hakuna mtanzania mwenye cheo anataka kuachia cheo chake:
1. hili linaanzia kwa wanasiasa, hakuna mbunge yupo tayari kustaafu
2. Hakuna mkurugenzi wa shirika lolote la umma yupo tayari kustaafu, yaani atafanya lolote huko aongezewe muda hata miaka miwili
3. Hakuna mkuu wa mkoa, RAS, au yeyote kwenye hizo kada anataka kustaafu, yupo tayari kufanya lolote abaki kwenye nafasi au aongezewe muda
Hivyo namuunga mkono Mh. Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa hiyo NGO yake maana ni utamaduni wa walionacho kutaka kuendelea na vyeo, yaani bora auwe mtu kuliko kuachia cheo.
Unasemaje, bro? Nyie madereva mmekuwaje?Sisi madereva waliostaafu na bado wakapewa mikataba yao feki mmoja alisababisha bonge la ajali coz alisinzia njiani.
Kuna mzee alikua 60+ akala miaka kadhaa ya mkataba.Unasemaje, bro? Nyie madereva mmekuwaje?
I see!Kuna mzee alikua 60+ akala miaka kadhaa ya mkataba.
Sasa safari ndefu mfano za Mwanza akataka ale per-diems.
Wanafiki, si alikuwepo wakumwanguashia jumba bovuIla walikuwa wanamsingizia Magufuli kwamba anataka kubadili katiba ahahaha