Narudia kusema "UAMINIFU" ni ndiyo nguzo ya ndoa na mapenzi kwa ujumla. Unajua kama hakuna uaminifu hakuna upendo, kukiwa na upendo bila uaminifu hakuna kitu. Nahisi tu huyu kiumbe akiwa siyo mwaminifu hata ungekuwa unafanya malovee kuliko makungwi atatoka nje kwenye kutafuta wale wasiojua.
Mapenzi ni Uamiinifu siyo vinginevyo. Kweli kuna kipindi wanawake tunajisahau sana, imagine mume anarudi nyumbani mapema akijua mke upo walau umpe chai ya jioni, wewe umo kwenye mihagaiko ya umbeya na biashara zisizo na uelekeo. Sasa yule HG yeye yupo kufanya kila kitu, ukiomba chai iko tayari, maji ya kuoga yako tayari, hivi kweli wewe mwanamke ingetokea house boy akafanya mambo kuliko mumeo si ungeelekeza majeshi huko.
Wadada badilika sana tuwape heshima waume zetu, hata kama si wazuri kama tunavyofikiri.
Ndiyo maoni yangu leo. Lets cross fingers and pray tuwe fair yale tusiyoweza kuvumilia tukifanyiwa basi tusifanye instead tufanye yale yanakubalika kiroho.