Ajiua baada ya mkewe kumpikia ‘majani ya kunde’ kwenye sikukuu ya mwaka mpya

Ajiua baada ya mkewe kumpikia ‘majani ya kunde’ kwenye sikukuu ya mwaka mpya

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Mwanaume mmoja nchini Kenya anayejulikana kwa jina la Boniface Okwero anaripotiwa kujiua baada ya kupikiwa majani ya kunde na mkewe kama mlo wa siku ya Mwaka Mpya.

Okwero ambaye ni mkazi wa kijiji cha Nanyungu Emauko inaelezwa kuwa aliporudi nyumbani kutoka kwenye mizunguko yake siku hiyo ya Mwaka Mpya na kukuta majani ya kunde, uliibuka ugomvi mkubwa baina yao huku akimuuliza mkewe kwanini hajapika nyama au kuku kama mlo wa sikukuu.

Kwa mujibu wa kiongozi wa eneo hilo Boniface Oyosa, baada ya mzozo huo mkubwa, marehemu aliichoma nyumba yao moto ambayo alikuwa akiishi na mkewe huyo na baadaye kujiua. Aliongezea kuwa mwanamke alipika chakula hicho kwasababu hakuwa ameachiwa pesa ya kutosha kununua na kupika kuku au nyama.

Muungwana
 
Inaobekana wakenya baada ya miaka 5 kutakuwa na idadi kubwa ya wendawazimu.
 
Back
Top Bottom