Ajiua kusa mume, madeni na msongo wa mawazo

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Nchini Kenya, Mwanamke aliyetambulika kama Mercy Nyasaka amejiua baada ya kuacha ujumbe mzito kwa ndugu wa karibu kupitia Whatsapp akimuaga na kueleza anayoyapitia, Mercy alifiwa na bintiye miaka miwili iliyopita mnamo Machi 1, 2023, kifo ambacho kilimsababishia huzuni kwa kiasi kikubwa kulingana na machapisho yake mbali mbali kwenye mitandao ya kijamii haswa Facebook

Licha ya kufiwa na bintiye Mercy mara kadhaa alichapisha machapisho yaliyoashilia kuhisi kukatishwa tamaa na mwenzi wake, na misukosuko mingine ya maisha ikiwemo na matatizo ya kifedha


Katika ujumbe aliotuma siku ya ijumaa kupitia WhatsApp kwa ndugu yake wa karibu, Mercy alimfahamisha kwamba hawezi kuendelea kuyakabili matatizo ya maisha pamoja na kifo cha bintiye, ikiwa ni pamoja na mkopo wa gari, mchumba aliyemkosa, na mkopo wa KSh300,000 aliokopa kwa kutumia hati miliki ya ardhi kama dhamana.

"Samahani kwa kukukatisha tamaa kwa njia hii lakini wakati utapata ujumbe huu nitakuwa nimeondoka kwa muda mrefu," sehemu ya ujumbe aliotuma Mercy.
 
Dah maisha yanachanganya sana, wakati huyo anajiua kwa issue kama hiyo kuna magangwe kitaa wana majanga hayo ya marehemu madogo sana lakini wanaishi tena Kwa furaha kabisa.
 
Expectation vs reality.

Wakute kwenye mitandao sasa na maisha ya kujionesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…