Wanabodi,
Leo hii baada ya kutafakari kwa kina juu ya swala zima la Katiba mpya likifuatiwa na kile wanachokiita changamoto juu ya Muungano na kero zake kwa wananchi wa pande mbili za Muungano. Kusema kweli nawashangaa sana wasomi wa nchi yetu, wengine ni Maprofesa na watu wanaojiamini ama kuaminiwa kuwa wanaweza kutupatia katiba bora inayotokana na wananchi hivyo wazitumie elimu zao ipaswavyo lakini sivyo!.
Baada ya kusikiliza hili bunge la Katiba na wajumbe wake wakipewa fursa ya kuzungumzia hoja zao juu ya muundo wa Muungano. Kwanza kabisa nimegundua kwamba sii wajumbe wengi wanafahamu asili ya muungano wetu, wengi wao wana maswali zaidi ya kuwa wao ndio walochaguliwa kupata ufumbuzi wa swala la katiba mpya. Ni madakatari wasojua ugonjwa huu ila wapo kujifunza na kujua ukweli wa gonjwa hili la Muungano. Na kinachochefua zaidi hasa kwangu mimi mwananchi msikilizaji, ni pale mjumbe wa baraza hili anaposimama na kuzungumzia mapungufu ya upande wa pili lakini asiweze kuzungumzia mazuri ya kile anachoki support kuwa ndio mbadala wa mahitaji ya wananchi wa pande zote mbili.
Ndio kusema hata wale wanaosema serikali 2, wameshindwa kueleza ni mabadiliko gani yatafanyika ili kuondoa kero zilizopo ama pia wale wanaotaka serikali 3 wameshindwa kuelezea mazuri ya serikali hizo 3 pasipo kunukuu (copy and Paste) rasimu ya katiba ilopendekezwa na tume ya Warioba. Na isitoshe wajumbe wote hawafahamu ya kwamba dhumuni kubwa la kurusha kongamano hili la baraza la Katiba live ktk luninga -TBC television ni kuwapa fursa hawa wajumbe kuwashawishi wananchi juu ya pendekezo lao la katiba hii ili siku itakapo pelekwa kwao wataiunga mkono kwa asiliimia kubwa.
Kibaya zaidi, na ajabu kubwa sana ni kwamba, hawa wajumbe hawa wanaodai serikali 3, wanashindwa kueleza ukweli ya kwamba ili serikali ya Tanganyika iundwe upya yaani itoke ktk tumbo ya Tanzania na kuwa hai ni lazima Muungano uliopo uvunjwe maana Tanganyika ipo na wanakubali uwepo wa Tanganyika ndani ya katiba tulonayo.. Pili, na ili muungano uwe wa Ushirika (Federation) ktk serikali 2 au 3 ni lazima muungano huu (political Union) ufe kwanza na waasisi wake hawatakuwa tena Mwalimu Nyerere wala Karume maana sababu zile za miaka ya 60's hazipo. Je ni sababu zipi? wananchi hatuzijui!.
Sasa nizungumzie, AJIZI hii kuwa nyumba ya UMASKINI.
Muda mrefu sana sisi wote tumekuwa tukijiuliza maswali kwa nini Tanzania ni maskini? hao hao wasomi wamekuja na kila aina ya sababu lakini sababu zote zimekuwa amakutokana na kero wala sii wao wahusika ila kundi jingine iwe CCM au wananchi wenyewe wavivu wa kazi, kumbe ukweli unabakia kuwa UMASKINI wetu unatokana na UVIVU wa sisi sote KUFIKIRI,Uvivu wa ubunifu na tafakari za kina juu ya mahitaji ya wananchi isipokuwa kero zinazoweza kuwaondoa ktk uongozi ama majukumu walokabidhiwa - Kero zimekuwa sababu. Hivyo ndio kusema uvivu wa kufikiri ni nyumba ya njaa na nyumba ilokuwa na njaa hujiwa na UMASKINI!.
Nitawapeni mfano mdogo sana niloushuhudia hapa Dar es Salaam.
Majuzi tu Manispaa zote za mkoa wa Dar es Salaam zilifanye Operation Usafi wa jiji hili. Ni wazo zuri sana tena hakuna jambo zuri ktk afya na usalama wa mwanadamu kama usafi. Na hakika mji wa Dar ulikuwa na kila sababu ya kufanya operation hii ili kuusafisha mji. Hakuna mtu anayependa Uchafu isipokuwa ni tabia ya baadhi ya watu kutokuwa na ustaarabu wa kuelewa athari za uchafu.
Sasa itazame ajizi ya Mtanganyika. Maamuzi yalofikiwa kuusafisha mji ilikuwa kuwafukuza watu wote wenye vibanda pembezoni mwa nyumba hata za biashara. Nilishuhudia watu wakivunjiwa majiko yao, mali zao zikitupwa na nyingine zikikusanywa kama uchafu wa mji lakini baada ya zoezi hili kubomoa vibanda vyote sikuona gari hata moja la kusafisha sehemu ile walobomoa mabanda yale ili kutoa mfano wa usafi!.
Nitarudia tena, USAFI wa mji ni kuondoa uchafu wa bidhaa zilizokwisha tumika ama kuuzwa, usafi ni kusafisha mazingira wanayofanyia kazi hawa wachuuzi na sii kweli kabisa kwamba uchafu wa mji ni hizo BIDHAA wanazouza kwa wananchi ili kukidhi wahitaji ya wananchi. Demand ipo kubwa lakini hatuna masoko ya kutosheleza. Zaidi ya hapo hawa wachuuzi kama wangesisitizwa kusafisha maeneo yao kila baada ya kazi, mji huu usingekuwa mchafu, hivyo Ajizi ya Mtanganyika ipo ktk kufikiri, kubuni na kutoa maamuzi yanayokidhi hoja ama mahitaji yaliyopo isipokuwa wepesi wa kuhofia kero!.
Mnaweza kusema hawa wachuuzi hawasikii lakini tazama basi, hivi kweli Manispaa za mji zinawezaje kukusanya tozo la siku kwa hawa hawa wachuuzi kila siku lakini washindwe kusimamia usafi? Je haiwezekani manispaa hizi hizi kuwatoza faini kubwa wale waloshindwa kuacha sehemu zao za kazi safi? Isipokuwa jibu rahisi kwao ni kubomoa vibanda vyote vya wachuuzi bila kujali gharama walizoingia ama kusababisha upungufu zaidi wa bidhaa hizona upandaji wa bei za mazao na matunda kwa walaji. Hivi kweli zoezi hilo litaleta Usafi mjini ama ndio linaongeza matatizo zaidi hata kwa walaji?
Tazama swala la Usafiri, Hivi kweli ili kuuweka mji wetu safi unaweza kufukuza Bodaboda na daladala zote toka mjini bila kuhakikisha kwamba kuna usafiri wa kutosha kutoka mjini hadi vitongoji vyake? leo hii wananchi wanalipa hadi Tsh 1000 hasa saa za jioni kutokana na maamuzi ya viongozi kuondoa Kero na msongamano na misululu ya magari mjini. Lakini basi ndio kusema wananchi wanakosa usafiri hivyo kuchelewa kurudi makwao hadi usiku mkuu. Hivyo ndio kusema makosa makubwa ya Mdanganyiika ni katika kufikiri na ubunifu ktk maamuzi yanayojenga na sii kubomoa. Leo hii ukiweka mabus ya kutosha kwa jiji la Dar es Salaam, bila shaka hizo Daladala na Boda boda zitapotea zenyewe. Nai anapenda kubanana ndani ya hizi daladala ama kupakiwa na bodaboda ambazo usalama wake ni kwa rehma ya Mungu! Hivyo hivyo uchafu wa mji ni Taka zinazotupwa hovyo mabaraabani iwe na wanunuzi, walaji ama wachuuzi wenyewe ndio dawa ya usafi wa mji sio bihaa inayouzwa..
Nini basi sababu ya kutumia mifano hii kuhusiana na kichwa cha mada hii AJIZI NYUMBA YA UMASKINI.
Wazungu wanasema hivi:- Necessity is the mother of invention - Mahitaji ni mama wa ubunifu.
Hii ni methari nzito sana na kwa ujumla wake ndio siri ya MAENDELEO na UTAJIRI wa mtu, watu na nchi. Ni sehemu inayokidhi hoja zote za huduma, kiuchumi, kisiasa na hata maisha ya kila mmoja wetu. Ila sote tunatofautiana ktk ubunifu na maamuzi ktk kukidhi mahitaji haya, na hapo ndipo sisi tunakwama kwa sababu tunashindwa kufikiri, tumeshindwa ubunifu ila huchukua njia rahisi zaidi kuondoa kero zilizokuwepo.
Kwa nini basi tunachukua njia rahisi? nimekuja gundua kwamba sisi Watanzania ama waafrika tuna hulka ya kutokidhi MAHITAJI. Huacha mahitaji hayo yawe ktk hali liyopo hadi inapokuwa KERO. Tazama jiji la dar linavyokuwa ilihali sewerage system yake ni ya toka mwaka 1950..Akili kweli?..Majengo yanapanda juu tu huku chini kunanuka! iNa ikisha fikia kilele za kero hutafuta njia na mbinu za kuondoa KERO hizi na sii MAHITAJI yalozaa KERO hizo. Hivyo unaweza kuondoa kero kwa muda lakini hutaweza kuondoa mahitaji (necessity) kwa kutumia suluhisho la Kero. Ni sawa na mgonjwa wa Malaria anapokunywa Panadol kutuliza homa ya kichwa!
Itaendelea