Wakuu
Mkandara na
Zakumi
Jiji la Dar-Es-Salaam ni picha kamili what is wrong with our national politics, priorities, weledi wa viongozi na madhara ya kukosa dira si la taifa tu, ata kwenye local governments target policies.
Sielewi kabisa shughuli ya mameya na kazi ya serikari za mitaa it is as if wao kazi yao kuuza viwanja tu. Kama unaangalia hata thread zingine jukwaa la siasa kuna baadhi ya wabunge wanachukua lawama sana kwa shughuli za viongozi wa serikari za mitaa.
Ukiangalia siasa hizi hizi za serikari ya mitaa nyanda za juu kama Mwanza na Musoma jamaa kule wameanza kuwajabika kwa sababu ya siasa za ushindani majuzi walimfungia meya matata asishiriki kwenye budget ya mwanza mjini kwa sababu aaminiki tena kwa mujibu. Kuna thread kazaa za uchakachuaji wa majengo ambazo manispaa ya Mwanza inasimamia na watu wana amshana kule kutafuta accountability.
Hayo mambo yamesaidia serikari za mitaa kuanza kuangalia miundombinu na namna bora za kutumia mapato yao nyanda za juu. Mfano mwanza mjini kuna anza kuwa kusafi kwa sababu wametenga budget ya kusafisha katikati ya mji kama nakumbuka vizuri. Bado wanachangamoto lakini siasa za serikari za ngazi hizi kule zimeanza kuzaa matunda kutokana na vuguvugu la siasa za ushindani.
Dar-Es-Salaam ni kichefu chefu kuna thread kazaa alizo anzisha
critical thinker or some name bearing those hallmarks, ameweka hoja kadhaa kenye jukwaa la siasa akiponda uongozi wa jiji la Dar-Es-Salaam, kikubwa akihoji wahusika bado hawana concept ya kazi kubwa na changamoto walizo nazo kama viongozi wa jiji kubwa hili kuuweka katika ramani kama mji wa kisasa.
Pili serikari aina malengo ya afya, ingekuwa lengo la usafi ni afya wange encourage kwanza wafanya biashara ku-adapt better practices kama ulivyosema kwakuwa wana serve a large proportion of those marginalized among us na wangetenga sehemu maalum za kibiashara hili watu wasitapake hovyo mabarabarani.
Since their services have higher demands to be ignored. Ni bora kungekuwa na course za kuwafundisha jinsi ya kufanya biashara katika mazingira ya usafi (maana wengine practices zao ni kwa sababu ya ignorance na kwa tanzania sidhani kama kabla ujafunguwa kibanda chako cha chakula unahitaji hata kuwa na certificate ya 'food hygiene' or 'health and safety'), lakini lazima tuwe wakweli most of these businesses are just about hand to mouth hivyo lazima waangaliwe kwa jicho la huruma na kuboreshewa mazingira ya kazi.
Kingine hapa kuna uhaba wa supportive sector kwenye service za chakula amna wajasiriamali watu wanaenda kwa mama ntilie inabidi wale palepale watu wanashindwa kutengeneza hata mabox ya plastic au 'polystyrene containers' hili wafanyakazi wabebe hata take away uchafu wakatupie kwenye ma-bin ya kazini. Yaani hata chips unafungiwa kwenye magazeti au foil paper urojo wote unakumwagikia come on watu wamekaa ulaya miaka yote hata kusema jamani embu tuwatengezee maboksi ya chips au expansive can that be, sasa kweli wataweza hata kutengeneza yale makabati ya chips ya mabati na mashine za kuweka chakula kibaki cha moto. Hivyo ni vifaa ambavyo nadhani sasa vinahitajika sio dar-es-salaam bali tanzania nzima and are commercial sound kwenye kuboresha mazingira na afya. Sisi bado na kuna vast opportunity ila watu wamelala nimejiuliza sana hawa watu walionza kurudi kabla yetu miaka yote hawakuona opportunities zilizojaa zaidi ya kwenda kushindana na wenye malori sijui mabasi no wonder wengi wanafail wakirudi kwa sababu ni zero creativity.
Kwa hivyo magoi goi wa serikari za mitaa na wao wanatakiwa kuinvest on infrastructure ambazo zinalenga kuboresha usafi wa mazingira na wafanya biashara wadogo watozwe a small licence fee towards that contribution na sio kodi ya mapato hilo siliafiki kutokana na faida zenyewe kuwa ndogo.
Tatu kutanua mji wa Dar-Es-Salaam traffic is centered towards on direction, all the outer zones head towards one direction at the moment, hivyo kupanua soko la kariakoo would just increase the capacity but it wont reduce the congestion of both the motors and people heading there, in addition to the already large population that is sheltered in those high rises (hapana aisee kariakoo if you ask me kwa sasa soko inabidi liondoke kabisa, jamaa wamearibu sana na migorofa, sijui ni ushamba). With those facts there would be even larger piles of rubbish to clear.
Inabidi watu wakae chini na waangalie sababu za kwanini watu wanaenda kariakoo na kupunguza safari za huko, serikari za mitaa zetu zimezubaa. Mfano kama UK ambapo kuna mfumo kama wa Tanzania local governments zinashindana kutafuta wawekezaji. Unakuta serikari inaona ikijenga soko ikalimiki ni good investment maana unapokea kodi za mapango na licence fees za kufanyia kazi, serikari kuu inachukua kodi where necessary na wao wanapata licence fees na kodi na kuna magari ya kukusanya uchafu kwa wenye biashara za chakula kama mafuta na food products huku wakichajiwa.
Lakini sio sisi tunashangaa na hayo mapato ndio yanasaidia ku-improve sehemu nyingine kama ku-invest kwenye properties, miundombinu kama mitaro etc lakini wao wanategemea mapato ya matangazo na mgao wa central government lakini creativity ni zero.
Na kodi zinazokusanya Dar unakuta serikari kuu kila kodi inarudisha kwenye mji kwa namna moja ama nyingine kuboresha jiji zima kama miundo mbinu za barabara kuu, vituo vya mabasi au hata kujenga Airport (sisi tunaona kama vile uwanja wa ndege ni public good, wakati wenzetu wanaona kama vile cash cow).
Mfano safari za ndege sasa hivi zinavyozidi kuwa cheap watu wanasafiri sana kibiashara a long stay car park ya wiki inaleta hela, ukifungua uwanja mkubwa na sehemu za maduka tayari yale yale ya uchumi wa sokoni yana amia airpot with a different marketing strategy in mind to entice big names only kama vile mabaa ya kisasa kuwepo hapo, supermarket ya size ndogo etc na vitu vingi tu. Lakini wapi?
Nne, umegusia kitu muhimu sana (Sheria) ambacho bila ya kigezo hicho kupewa national attention maendeleo yetu yatachukua muda mrefu sana. Sheria kwa Tanzania si kitu cha muhimu au ambacho kina fahamika na wengi hili kiweze eshimiwa. Tatizo hili linaanzia na mfumo wa elimu nahisi, likiendelezwa na poor regulators.
Kwa sasa watu pekee ambao naona wanafanya kazi yao ni wakaguzi wa bidhaa those people are taking their role serious atleat ukiwafananisha na regulators wengine na sasa naona wafanya biashara makanjanja wanaanza kufikiria mara mbili kuleta bidhaa feki jamaa wanazuia production, wanafunga biashara au wanataifisha bidhaa mchana kweupe. With that commitment in the long run itazaa matunda tu ya kuheshimu quality demanded by the government.
Ukirudi kwenye ufahamu wa sheria na wafanyakazi wa umma ni tatizo, sheria nyingi za serikari azifikii malengo yange kwakuwa implementers wenyewe ndio wasio ziheshimu huko makazini kwao au kuzi-enforce. Kwa wenzetu inakuwa ngumu sana kupachikana kwenye ajira kwa sababu mfanyakazi yeyote anatakiwa azielewe sheria za mazingira ya kazi yake maana hizo ukizivunja, kampuni inapelekwa mahakamani na kupigwa faini za nguvu. Sasa wewe usishangae kwa mfano Tanzania labda kungekuwa na sheria ya usimamizi wa usafi (mtu ambae anatakiwa akague mazingira ya usafi ndio atakuwa mpokeaji mkubwa wa rushwa na kuacha watu watupe uchafu sehemu zisizo takiwa) na hivyo ndio mambo yanavyofanyika sehemu zote za serikari.
Hapo ndio nadhani ndio tatizo lilipo wafanyakazi wengi hawaelewi hata sheria za kazi zao vinginevyo huwezi kwenda hospitali dokta akuchunie akijua hilo ni kosa lakufungwa with the right watch-dogs au hata hospitali yenyewe inayotibu wagonjwa ndio chanzo cha magonjwa wako wapi wasimamizi wa afya, without laws and enforcement officers tutasogea polepole sana, mi nadhani imefikia wakati hili swala hilo lipewe kipaumbele sehemu za umma na private. Maloya wetu embu nao wawe wajasiriamali kidogo kusaka opportunities za uzembe, serikarini kwa sasa kuna mpunga wa nguvu watu kuzidi kuwa matajiri kwenye fani hiyo kutokana watendaji wahuni waliojaa Tanzania.