Tetesi: Akagera National Park ya Rwanda inavyochukua wanyama wa pori ya Burigi na Kimisi na kuwafungia kwenye fensi

Tetesi: Akagera National Park ya Rwanda inavyochukua wanyama wa pori ya Burigi na Kimisi na kuwafungia kwenye fensi

R.B

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
6,296
Reaction score
2,575
Akagera national park ya Rwanda inavyochukua wanyama wa pori la Burigi, Kimisi ,Rumanyika na Ibanda na kuwafungia kwenye fence- H. Kigwangala umelala

Akagera national park ni mbuga inayounganisha mapori ya Tanzania na Rwanda , Tanzania kuna mapori mengi ambayo badala ya kuyapandisha hadhi tumeyaacha kama game resrve ambayo ni wa pori la Burigi, Kimisi, Rumanyika na Ibanda. Rwanda mbuga yao inayoungana na mapori haya wameifanya national park .

Inalindwa na jeshi la Rwanda, kutoka na vita wanyama wengi walikuwa upande wa Tanzania miaka ya 80 mpaka 90, wilaya ya Biharamulo wanyama walikuwa wanakuja mpaka mjini suala la kuona simba, chui, swala, nyani na kifaru ilikuwa suala la kawaida na tembo lakini kwa sasa wamepotea.

Na hii historia imeanza baada ya Rwanda kupandisha hifadhi ya Akagera na kuifanya nationa park.

1. Wanatumia jina la Akagera kuwahadaa watalii wanaodhani wanakuja mkoa wa Kagera na kiuhalisia mbuga hiyo inapakana na Kagera kwani wanashare wanyama na mapori ya Kagera

2. Mapori ya Kagera yalivamiwa na wanyarwanda kimkakati na kuanza kuchoma moto mapori ya Tanzania na kuwafukuza wanyama kuhamia pori lao la Akagera.

3. Jeshi la jirani lilianza kuteka pori la Burigi, na serikali kupeleka operation ya kusindikiza magari ili hali Rwanda wanafukuza wanyama na kuwapeleka pori lao .

4. Baada ya wanyama wa kila aina toka mapori ya Kagera kujaa pori la Akagera wamezungusha fence ya moto wa umeme kuwazuia wasirudi na wanaoingia kwenye fence hawarudi .

Ushauri wa bure: Tulishakosea zamani tusifufue makaburi, nashauri ipandishwe hadhi pori la burigi na kuwa national park ili tudhibiti wanyama wetu ili kujua idadi ya wanyama na kuwatrack
 
Tatizo ni rushwa kutoka kwa hao maafisa wanyama pori lilichangia sana wanyama hao kuhama, nakumbuka mapori ya Kimisi na Burigi yalijaa wafugaji wa kinyarwanda ambao walikuwa wakiingizwa na hao askari wanyama pori kwa malipo maalumu. Uingiaji wa mifugo na shughuli za kibinadamu ziliwafukuza wanyama na kuamua kukimbilia AKAGERA.

Tatizo lingine ni wananchi wa maeneo haya wengi wao hawana Uzalendo au hawajioni kuwa ni raia wa Tanzania kutokana na Oparesheni nyingi za Wahamiaji Haramu kuwakumba, wanajiona kunyanyapaliwa hivyo hawaoni haja ya kushiriki katika uhifadhi wa maeneo hayo.

Hata kama litageuzwa kuwa hifadhi kama askari wanyama pori hawatakuwa na uzalendo na wasipopewa marupurupu basi hali itaendelea kuwa vilevile.

Ushauri wangu ni kwamba iwekwe vifaa maalumu vya kuwa-track wanyama wetu wanaovuka eneo la hifadhi, wafugaji wasiruhusiwe kuingia kwenye hifadhi, askari wanyama pori wapewe mishahara minono, marupurupu pamoja na vitendea kazi vya kisasa, na mwisho iwekwe adhabu kali (ikibidi iwe ya kifo) kwa wale wote wanaoshiriki kwenye kuvamia hifadhi na wanaokamatwa kwa ujangili.
 
Hoja ni ulinzi au kupandishwa hadhi?

Serengeti Ni national park lakini wanyama wanaenda Kenya kila siku.
 
Hii ndio jamii forums niijuayo. Hoja mujarabu. Nadhani serikali ilifanyie kazi hili, kwanza kufuatilia ukweli wake, pili kuja na mkakati wa kuzuia hilo lisitokee tena.lakini pia kuna umuhimu wa kuangalia upya Uhusiano wetu na Rwanda. Sio watu Wazuri kwetu.
 
Rwanda wana maliasili kidogo sana ukilinganisha na idadi ya watu, hivyo wanayanyonya nataifa zembe kama DRC na TZ, wanaijua nguvu ya TZ hivyo kwetu wanakula kwa akili zaidi lakini huko DRC wanatumia msuli zaidi. Ni aibu nchi kama TZ tunachezewa na kanchi kama rwanda
 
Huwezi kumfilisi Bill Gates kwa kumuibia Tsh milioni mia. Tz ni tajiri wa rasilimali za wanyama na mbuga za wanyama. Hatuwezi kuathirika kwa udokozi wao wa swalla wawili, watatu.
 
Unapofanya urafiki na jirani lazime uwe na tahadhali sana hasa ukifanya urafiki na nchi za maziwa makuu kama Rwanda!!! I tell you be careful sana!! They may have longterm plans against you !!! Ni wapole kama huwa lakini wajanja kama nyoka
 
Back
Top Bottom