Akamatwa kwa kuendesha Ubalozi Feki kwa Miaka 7 India

Akamatwa kwa kuendesha Ubalozi Feki kwa Miaka 7 India

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Jeshi la Polisi Nchini India limemkamata mwanaume mmoja aitwaye Harsvardhan Jain, kwa tuhuma za kuanzisha Ubalozi feki ambapo amekodisha Jumba la Kifahari pamoja na Magari ya Kifahari na kuyaegesha nje ya jumba hilo yakiwa na namba feki za ubalozi wa Nchi ya Westarctica.

1753350006229.png

​
Inadaiwa kuwa Harsvardhan Jain, alijitambulisha kama Baron wa Westarctica ambaye ni kiongozi wa nchi hiyo na amekuwa akisafiri kwa magari ya kifahari yenye namba za kidiplomasia ambapo pia alitumia picha zilizopigwa na aliyekuwa Baron akiwa na Rais, Waziri Mkuu na watu mashuhuri ili kujipatia nafasi na heshima katika jamii ya watu wa hadhi ya juu ambapo amekuwa akitumia ubalozi huo feki kulaghai watu hususani waliopo nje ya India na pia kushiriki katika utakatishaji wa fedha haramu.
1753349958645.png
Aidha Jain hapo awali alikuwa ameshtakiwa mwaka 2011 kwa kosa la kumiliki simu ya setilaiti kinyume cha sheria na maafisa wa polisi nchini India walipofika kwenye jumba hilo wamekuta nyaraka mbalimbali zikiwemo Pasipoti za kidiplomasia 12 kutoka mataifa bandia, nyaraka zenye mihuri ya Wizara ya mambo ya nje ya India, Mihuri ya mataifa 34, fedha za kigeni, Kiasi cha rupia Mullioni 4.4 (sawa na millioni Tsh.130) pamoja na namba za magari 18 za kigeni.

Westarctica ni taifa bandia lililoanzishwa mwaka 2001 na Afisa wa Jeshi la Wanamaji la Marekani Travis McHenry, Alijitangaza kuwa Mtawala Mkuu wa eneo hilo na Westarctica ambapo inadaiwa kuwa nchi hiyo ipo katika bara la Antaktika na ina ukubwa wa takribani maili za mraba 620,000, McHenry alitumia mwanya katika Mkataba wa Antaktika, ambao unakataza nchi yoyote duniani kudai sehemu ya bara hilo kuwa sehemu ya nchi yake ambapo mkataba huo haukusema chochote kuhusu watu binafsi Sambamba na hilo cha kushangaza zaidi muda mfupi tu baada ya kukamatwa kwa jumba hilo kupitia kurasa Instagram wa ubalozi huo feki wa Westarctica walitangaza kufungua ubalozi Mkuu mpya katika jiji la New Delhi nchini India.​

============For English Audience==========
​
Police in India have arrested a man who allegedly ran a fake embassy from a luxury bungalow near New Delhi for seven years, using it to front job scams and a money-laundering operation under the guise of representing fictional countries like “Westartica” and “Saborga”.
The suspect, 47-year-old Harshvardhan Jain, had styled himself the “Baron of Westartica” and projected the image of a globe-trotting diplomat, complete with diplomatic vehicles, forged documents and Photoshopped images of him alongside world leaders. But authorities say his real enterprise was far more mundane – and criminal.

Jain allegedly duped jobseekers by promising them employment abroad and laundered money through shell companies via the hawala system – an informal, unregulated method of transferring funds that operates outside traditional banking channels – according to the Special Task Force of Uttar Pradesh Police.

“The accused was running the bogus embassy from a rented house and projected himself as a consul or ambassador of non-existent countries such as Westarctica, Saborga, Poulvia and Lodonia,” Additional Director General of Police Amitabh Yash told The Times of India.

SOURCE: THE GUARDIAN

​
 
India napo inaonekana mbumbumbu wengi kama Mbogo tu. Hilo jina lilitakiwa kuwagutua hata wananchi wa kawaida kabisa kuwa hapo hakuna ubalozi Bali utapeli
 
Hizo hela zote za kukodi alikuwa anatafuta hela Gani? Angekuja bongo afungue betting au kilimo cha pork😆😁
 
Back
Top Bottom