Hahaaa, Mkuu hii ya kufunga kaptura na kamba (kinyamwezi hiyo kamba wanaiita Mkwato/mkwatu) naikumbuka sana na umenirudisha long time. Niliishi kwa miaka kadhaa nje ya Mkoa wa Tabora na niliporudishwa kuanza shule kijijini ndipo nilianza kuona vituko kama hivi.
Nilishindwa kuelewa jamaa wanawezaje kutembea msituni bila viatu na visiki vya nyasi vinachoma kishenzi na hadi leo imenishinda. Ila kiboko ilikuwa ni hii.... (Ntaiandika chini).
Pole kwa kipigo kutoka kwa Mzee ila nafikiri ilikusaidia ili uanze kuheshimu vitu vya watu, hahahaaa 🙂 Huyo sister mkumbushe siku moja jinsi alivyokusabishia kipigo.
Vijijini ilikuwa raha sana maana vibinti vina sketi tu bila chupi na sisi ni vikaptura tu bila chupi. Sasa siku moja nilipata kipigo kwanza fimbo na mwisho nikaambiwa nichuchumae na kupitisha mikono ndani ya miguu na mikono ije ishike masikio - Kaptura ndiyo katikati imechanika na sina chupi...... Nilifanya show ya bure na ilikuwa mzinga wa SOO!!!!! Kwa kawaida, kuona vinonino vya watoto wa darasa la tano kushuka chini, ilikuwa si ajabu. Kweli maisha duniani yamebadilika maana sasa hivi vyupi karibu kila mtu anaweza kununua maana zinatoka China na India hadi unashindwa kujua, watengenezaji wanapata hela gani.
Mwisho nimalizie hiyo habari nilikuwa naandika hapo juu............. (Kama unakula au waweza pata kichefuchefu basi iiishie hapa hapa na usisome zaidi ya hapa) ........ Kiboko ilikuwa kuwa kijana akitawaza kwa kuweka Masaburi chini ardhini na kujiburuza ili kujisafisha, lohhh. Hii hadi leo huwa najiuliza, huwa inabidi wakae mkao gani ili kufanya huo UJUZI wao?