Akatwa Mkono na Titi na Mumewe Akimtuhumu Kufuta Missed Call ya Mwanaume Mwingine.

Akatwa Mkono na Titi na Mumewe Akimtuhumu Kufuta Missed Call ya Mwanaume Mwingine.

Mcanada

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
982
Reaction score
1,942
AKATWAA WEB .jpg

Maria Marwa aliyekatwa mapanga
***

Maria Marwa (36) mkazi wa Kijiji cha Isango, wilayani Rorya mkoani Mara, amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga na kukatwa mkono wa kushoto na titi la kushoto na mume wake kwa madai ya kukosekana kwa namba ya simu iliyopigwa kwenye simu ya mwanamke huyo.

Akisimulia tukio hilo mwanamke huyo amesema usiku wa kuamkia Septemba 8 mwaka huu baada ya chakula cha usiku mume wake Werema Ibaso, alimuomba ampatie simu yake na kuanza kumhoji juu ya namba ya simu iliyopigwa siku mbili nyuma ambapo mwamke huyo alipoikosa ndipo mwanaume huyo alipochukua panga na kuanza kumkata kata maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Akizungumzia sababu ya kukata mkono na titi Daktari wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara, amesema mgonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa kuchelewa hivyo majeraha aliyokuwa ameyapata yalianza kuharibika.

EATV ilimtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime, Rorya Geofrey Sarakikya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema jeshi la polisi linaendelea kumsaka mwanaume huyo ambaye baada ya kufanya tukio hilo na kutoroka kusikojulikana.

CHANZO - EATV
 
Hii ni ile ile wivu wa mapezi,unakuta simu imeita akaikata,ikaita tena akakata,alivyoona jamaa anamfuata kaifuta ghafla,jamaa anaangalia hakuna simu iliopigwa,hapa ni bora uvunje tu simu halafu utoke nje ukatembee,kuliko kuanzisha mzozo...
 
Elimu ni kitu muhimu sana. Kipi bora kupotezea uwe huru au umjeruhi mtu uishi kama digidigi.
Wanaume msipokuwa na akili mtaishia Sana jela. Na ukienda jela kwa kesi za kipumbavu lazima ukaolewe. Ingia jela kwa kesi za pesa utaheshimika.
 
Akamatwe na yeye akatwe uume na mguuu pumbavu sana akili kama limnyama.
 
Back
Top Bottom