Akaunti fake ilivyorudisha mahusiano yangu na mpenzi wangu kwa haraka sana

Akaunti fake ilivyorudisha mahusiano yangu na mpenzi wangu kwa haraka sana

Hizo mambo Mm nimefanya Sana Kama kwa mademu watatu ni story ndefu Sana na watu wengine wanaweza hisi ni uongo bt hivi vitu vipooo, in short kuna mdada nafanya naye kaz staff moja sio mzur Sana Ila ni mapepe Sana na story Zake anajifanya mataw ya Juu Sana.Siku moja nikafungue account fake fb nikamtumia friends request akakubal then tunaanza kuchat siku ya kwanza ya pili baada ya siku tatu nikaanza kumtongoza akaomba nimtumie picha nikatuma picha ya rafk yang anayeishi mkoan, bas mdada akaniulza nafanya kaz gan? Nikamjib Mm ni muhasib wa kampun fulan na nipo dar. Mdada akaona kapata mtu wa maana Sana, na mm nikamwambia natafuta mke, bas tunaanza kuchat Kama wapenz, baadaye akanitumia namba ya cm tukawa tunachat na Mm nilimuazima mtu namba ambayo haitumii, na kwa kuwa cm yang ilikuwa uwezo wa kufungua whatsapp mbili bas moja yang ya kawaida na nyingne ya huyo mdada na nikamuweka DP Kabisaaa.nilikuwa nampelekesha mpaka akawa akanitumia picha za nusu utupu, na wakat akawa mpaka akanitumia hela, kuna ck Mm mwnyw nilikuwa Nna Shida ya hela nikamfata ofisin nikamuomba anikopeshe laki 2 bt bint akasemaje hana, Nikamjib Pouwaaaa, hapo hapo nikaingia whatsapp nikamtext bby mambo Nna Nna Shida Sana na laki 3 vp waweza niazme? Akaniambia nisubir Kama Lisaaa aende bank kuchukua kwel baada ya lisaaa naona mzigo unasoma m pesa.
 
kuna watu naona mna muda mwingi sana msiojua muufanyie nini..
 
Kanitoa chamboo wallah hii tabia tulifanya chuo kusajili namba alafu unaanza kumtongoza baby wako
Mambo ya kizamanii... siku hizi namba mpya mtu unaifanyia tathmini. Hawa wasukuma bhana....
 
Story ina chumvi nyingi hii....
Hizo accounts zote ulifungua kwa kutumia email au phone number?
 
Habari wanajamvi
Bila kupoteza muda,hivi karibuni nimejikuta kwenye mateso ya kimapenzi baada ya kuhitilafiana na mpenzi wangu

Jinsi ilivyokuwa
Nina mpenzi wangu ambaye tumekuwa kwenye mahusiano ndani ya miezi kadhaa iliyopita,anakaa mtaa wa pili kutoka mtaa ninaokaa
Wiki moja iliyopita niliingia kwenye mgogoro mkubwa wa kimapenzi ambapo ulivunjika ila baadae nikaurudisha kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu ndani ya siku tatu,ni baada ya kunifumania nikiwa katika harakati za kumgegeda mwanamke mmoja ambaye nafanya naye kazi
Kiukweli huyo mpenzi wangu ambaye nampa jina la Stella ila siyo lake alikuja kwangu bila taarifa akanikuta live nikila mate na Fatuma na tukiwa tupo vifua wazi na huyo dada wa ofisini ambaye nampa jina la Fatuma
Ilikuwa ndo siku ya kwanza kutaka kumgegeda Fatuma baada ya kumfukuzia kwa muda wa mwezi mmoja huku akipiga chenga na kunifanyia utafiti kama nina mpenzi mwingine.
Kwa uwezo wangu wote nilijitahidi kumficha Fatuma kama nina mpenzi mwingine muda huo ananifanyia uchunguzi mpaka siku ya tukio
Wakati namuandaa Fatuma tukiwa sebuleni sikufunga mlango,niliwaza kuwa ngoja nimuandae akiwa tayari,nafunga mlango wa sebuleni kisha nishike mkono nimpeleke chumbani kwa ajili ya kazi,kumbe ndo Stella anaingia bila hodi

Niliishiwa pozi,Stella akitetemeka aliuliza huyu ni nani,? Nikaishiwa pozi na Fatuma akashindwa,kuongea na akahamaki,
Fatuma aliamka kutoka pale kwenye sofa akasimama akavaa blezia na blauzi yake na kuchukua mkoba na kuondoka bila hata kuongea neno
Stella alinigombeza akaniambia Mimi na wewe mapenzi basi na kuondoka,nilibaki nimeduaa,na kujilaumu nimefanya nini hiki,muda huo ilikuwa SAA 12 jioni
Nilinyenyuka kwenye sofa baada ya kufikiria kama dakika 45 na kwenda kuoga.
Nilijaribu kumpigia Fatuma ili nimuombe msamaha kwa lililotokea hakupokea sim,nikampigia Stella akawa ameisha niblacklist,akaniblock WhatsApp, nikachoka mwili mzima

Kiukweli nilikuwa bado namhitaji Stella,na bado nilikuwa nampenda sema tu ni ile hali ya tamaa za wanaume,
usiku huo nilienda kwa Stella kuomuomba msamaha lakini niliambulia maneno makali ya dirishani na mlango haukufunguliwa na sikupewa hata nusu dakika ya kujitetea,nikaamua kurudi kwangu nikiwaza kweli Stella ataniacha,nifanyeje asiniache,bado nakupenda Stella niliwaza usiku kucha.
Siku iliyofuata ilikuwa siku ya weekend hivyo nilibaki ndani nikiwaza kuhusu tukio la Jana na Stella kuniacha.Wakati nawaza nikapata mbinu ya kumfanya Stella arudishe mapenzi yake kwangu ,asiniache

Kipindi cha nyuma wakati naanzisha mahusiano na Stella,aliniuliza kama nina mtu mwingine,nikasema"kwa vile nakupenda nitakwambia ukweli,nilikuwa naye ila sikutembea naye na mpango wa kutembea naye sina"hayo majibu hayakuwa ya kweli,ukweli ni kuwa katika kipindi hicho sikuwa na mtu
Akaniuliza "kwa nini unataka kumuacha unanitaka Mimi?" Nikamwambia " Huyo mwanamke ananitongoza mwenyewe,na mimi simpendi,ananilazimisha tu lakini namkwepa,ila uzuri ni kuwa sijawahi kutembea naye,ila kwako nimedata" hayo maneno hayakuwa ya kweli,lengo ni kutaka kumuaminisha kuwa na Mimi naweza kupendwa na kutongozwa na mwanamke,
Huyo mwanamke nikampa jina la Haika,

Ili nimuaminishe zaidi nikafungua akaunti fake Facebook, nikatafuta picha ya mwanamke mrembo miongoni mwa marafiki zangu nikaiweka kwenye profile hiyo,nikaomba marafiki wachache lakini baada ya saa moja nikawa na friendrequst zaidi ya 1000 wengi wao wakiwa wahindi nikazikubalia request zote
Kisha nikaingia messenger nikaanza kuchati na Stella kwa jina hilo la Haika John.
Nikamwabia samahani dada,wewe ni kweli ni mke wake Maga?,Stella akajibu"kwa nini uulize hivyo?
Nikamwambia huyu kaka Maga nilikuwa naye kwenye mahusiano lakini sasa hivi amebadilika na kuniambia ana mke tayari anaitwa Stella kama vipi mtafute fb atakwambia ukweli ndo nimekutafuta" Stella akasita kuwa wazi akajibu,mmmh Mimi sidhani,Stella akauliza kwani mmekuwa naye kwa muda gani? Nikajifanya Haika nikajibu," Nikamjibu wiki mbili"akauliza je umewahi kutembea naye? Nikajibu hapana, kisha Stella akasema ni kweli alichokwambia Mimi ndiye mkewe,nikajibu asante Dada maisha mema kumbe huyu kaka alikuwa ananidanganya" nikalog out, dakika chache tu Stella akanipigia ,akaniulizia kuhusu huyo Haika, nikamwambia baada ya kuona ananisumbua nilimwelekeza fb akutafute ili ukufaham kuwa wew ndiye mke wangu asiwe ananisumbua,vip amekuambiaje Stella akajibu "ameniliuza tu kuwa wew ni mke wa Maga nikasema,muulize yeye atakwambia Mimi sina majibu" Nikacheka moyoni,nikajisemea ungejua kuwa uliyechat naye ni Mimi usingesema hivyo",pia nikajisemea moyoni hapa kazi imeisha Stella amesema vile kwa akaunti ya Haika basi kazi imeisha,
Baada ya siku mbili tukaanza mapenzi na Stella,baada ya siku mbili zingine nikafungua akaunti nyingine,nikaipa jina Joyce Sera,nikamfuata Stella inbox nikachat nikilaumu Haika alivyo na mpango wa kumnyang'anya mpenzi,anavyotamba kuwa atakunyang'anya Maga hawezi akakubali kiurahisi,Stella naye akajibu" imekula kwake atafute tu mwingine ,Maga nimeisha mmiliki,pia kupitia hiyo akaunt ya Joyce nikajifanya adui namba moja wa Haika
Stella alifurahishwa na Joyce kwa kumpinga Haika ,huyu Joyce alijitambulisha kama Mdogo wake Haika,basi Stella akamuona Joyce kama mtu wake wa karibu sana hivyo akamuomba namba ya sim ili wawe wanawasiliana na kuwa mashoga
Baada ya Stella kuomba namba nikafikiria namba ya sim nitaitoa wapi,nikapata wazo la kumuomba Dada mmoja kama ana line ambayo haitumii kwa bahati nzuri alikuwa nayo, nikachukua namba za sim,nikamtumia pia naye Stella akaweka namba yake pale inbox
Ile line ya simu nilichokifanya nikaifungulia akaunti WhatsApp,kisha nikaitunza mahala
Sim yangu nikaiwekea double space WhatsApp,upande mmoja ni Mimi upande wa pili ni Joyce,
Nikawa nachat na Stella kwa upande wa pili wa WhatsApp kama Joyce nikimpondea Haika na pia nikajifanya namfahamu Maga,nikamsifia maga kwa maneno mazuri mazuri kibao.
Uzuri ni kuwa Stella hakuwahi kupiga hiyo simu kuongea kwa njia ya sauti,yeye alijikita kuchat nayo WhatsApp

Hayo ndiyo yaliyokuwa yametokea kipindi hicho namtongoza Stella,


Baada ya hili fumanizi akili ikanituma kuanza ule mchezo wa Haika na Joyce.
Siku hiyo nikaanza kuchati na Stella kwa WhatsApp kwa akaunt ya Joyce kama shoga yake
Vip Stella hujambo? Akajib " Sijambo,vip mwenzangu kulikoni na Maga mbona ameniomba namba za Haika, pia ananiomba nimuombee msamaha ,kwa kumkataa Haika ambaye alikuwa anampenda kiasi kile," Stella akachelewa kujibu,ila baadae akamwambia MPE tu
Nikasemea moyoni" duh,ngoma bado ngum", basi nikaendelea kuchati naye nampondea Haika,baadae nikajifanya kimya kidogo kuwa kama vile naongea na Haika kuhusu ombi la Maga
Kisha nikanza kuchat tena," unajua shoga ni nini cha ajabu Haika kakubali,jamani shoga unamuachia Haika mume? Stella hakujibu,nikajifanya kutulia ,ilipofika jion, nikaanza kuchat naye ," shoga vipi,naona Haika anaandaa safari kwenda kwa Maga kesho kwa hiyo,ndo anaenda kuyajenga hivo,kaishatumiwa nauli shosti,"hapo Stella akaanza kujibu "kweli shoga " nikajibu ndiyo,tena asubuhi atakuwa amefika kwa Maga.Hakujibu akapiga kimya ,basi na mimi nikaona Haya mambo ni mazito

Ikawa saa saba za usiku nikasikia mesege inaingia kuangalia,ni Stella,njoo sasa hivi hapa kwangu naumwa sana unipeleke hospital.Nikaamka kitadani paap nikasimama ,na kuanza kucheka ,mimi ndo Maga kwa kweli ,kazi imeisha, nikavaa fasta nikaenda mpaka kwake ,akafungua nikaingia chumbani,akanza kulia kwa nini namtesa ,basi nikamtuliza,nikamuomba msamaha yakaisha,tukalala mpaka asubuh,ila hakuniulizia kuhusu safari ya Haika

Kesho yake akaniambia ataenda kwangu kushindiapo hataenda kazini kwake,hivyo nimuachie ufunguo pale ninapoweka,nikasema haina shida,nikaenda kwangu kwa Furaha nikaoga nikaenda kazini,Stella alienda kwangu ile asubuhi na kufanya usafi nakupika na kuingia kitandani kupumzika,kisha akatext WhatsApp akimuuliza Joyce kuhusu safari ya Haika kwa Maga ,nikamjibu wamezenguana asubuhi hivyo hana tena mpango,nikachekaaa,mpaka wenzangu wakaniuliza vip bro umepata Tatu mzuka nini

Mwisho hii stori si ya kutungwa ni ya kweli,vijana unapaswa utumie ubunifu katika mapenzi kuliko kutumia nguvu kubwa kwa mambo kama haya
Asnteni
We jamaa ni zaidi ya genius nimenyoosha miguu juu!
 
mimi nilivyo aisee ningeshtukiwa tu stella anashangaa anakuta sms kutoka kwa haika "vp arifu?" mchezo unaungua kii iv yan
 
mimi nilivyo aisee ningeshtukiwa tu stella anashangaa anakuta sms kutoka kwa haika "vp arifu?" mchezo unaungua kii iv yan
[emoji1] [emoji2] [emoji2] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji2] [emoji1] [emoji1]
 
Siku zote huwa naanza kusoma conclusion ndo narudi juu... Baadaye
 
Back
Top Bottom