Akaunti ya Benki ya mtu aliyefariki

Akaunti ya Benki ya mtu aliyefariki

Hela zikishaenda kwenye account ya mahakama zitagawiwa kwa warithi baada ya hakimu kupitisha. Ni kama 4 months process mpaka warithi wapewe hela zao baada ya kuingia account ya mahakama
 
Fanyeni kikao cha familia
Teueni wasimamizi wa mirathi
Katika kikao bainisheni hiyo Akaunti na umuhimu wake, nendeni mahakamani mkafungue kesi ya usimamizi wa mirathi wale wasimamizi wakishateuliwa watapewa documents za mahakama
Hizo documents mnaweza kuzitumia kwenda nazo Bank ili wasimamizi waweze kuendelea kuitumia hiyo Akaunti au vinginevyo.
Asante.
Yeye amesema mahakama ndio itapeleka barua bank na hela zitahamishwa akaunt itafungwa. Hakuna ruhusa kuomba mda zaidi kwa ajili ya miamala mingine kwa wale wasiojua kama mhusika amefariki. Lakini nilishawahi kuona wengine wamepewa hiyo ruhusa
 
Ngoja nikuulizie kwa hyo kaka kisha nikupe jibu la uhakika walifanyaje maana alikua akiniapa hizi story sema sikuzitilia maanani sana
Sijakuelewa ndugu
 
Kumbe inawezekana.... Leo mhudumu pale mahakamani anasema eti ni lazima ifungwe
Mnaweza kuiendeleza ila ikitokea tatizo lolote la kumuhitaji muhusika wa account changamoto itaanzia hapo.

Na Kwa kiusalama wanandugu mnaweza kugeukana mmoja anaweza akatoa hela . Ni vema mkaifunga mkafungua mirathi mkagawana kilichopo au km mtakiendeleza Kwa utaratibu mwingine baada ya kuzitoa kwenye account ya marehemu mkafungua account ya group
 
Nimecheka, ukirudi mwambie secretary taaluma yako ni ya uchapishaji wa hukumu mengine sio utaalamu wako, akisema kwanini mwambie pesa zinaingiaje account ya mahakama nimecheka [emoji23] ni mahakama gani hiyo ya kino
Pesa haingii mahakamani isipokuwa mirathi ikitoka ikiwa imekubaliwa , bank wanatoa chek ya balance iliyopo kwenye account ya marehemu , chek haiwez kutoa pesa mpka igongwe muhuri wa mahakama husika iliyosimamia hiyo mirathi, halafu inarudishwa bank, pesa zitatolewa ikiwa warithi wote mliotajwa kwenye mirath mkiwepo bank kaona maelekezo mengi naona kaamua kumfupishia hapo.
 
Wakuu habari zenu?

Ninaomba msada na muongozo kuhusu hili jambo. Mfano kuna account bank ambayo mhusika wake alishafiriki ila warithi wa marehemu wangependa account isifungwe na kisheria waruhusiwe kuisimamia kwa muda flani kwakuwa kuna miamala ya fedha (za kibiashara) ambayo bado inaingia kwenye hiyo account. Inawezekana?

Miamala ya Biashara kwenye account ya mtu binafsi au ya Biashara?
 
Yeye amesema mahakama ndio itapeleka barua bank na hela zitahamishwa akaunt itafungwa. Hakuna ruhusa kuomba mda zaidi kwa ajili ya miamala mingine kwa wale wasiojua kama mhusika amefariki. Lakini nilishawahi kuona wengine wamepewa hiyo ruhusa
Kuna members wamekupa maelezo sahihi ila ngoja nikunyooshee kidogo.

Je wewe ni mnufaika wa hiyo mirathi, kama ndio je hizo pending transaction zinatalajiwa kuingizwa lini kwenye hiyo account?

Kama ni hivi karibuni subilini msifunguwe mirathi kwanza pesa iingizwe.

Pesa ikishaingizwa mnafunguwa mirathi ambapo utaratibu ni kwenda mahakamani na mukhtasari wa kikao cha familia ambao mmeteuwa msimamizi wa mirathi, mukhutasari ugongwe muhuri wa serikali ya mtaa, ni vizuri mkiandika kwa mkono msichape tafuteni mwanafamilia mwenye muandiko mzuri atawaandikia.

Mkishafunguwa mirathi mahakamani kama hakuna malumbano yoyote ya kifamilia kugombea chochote shauri linapelekwa faster na msimamizi wa Mirathi anateuliwa na mahakama na anapewa barua ya utambulisho wa msimamizi wa mirathi.

Sasa hapo ndipo mahakama itaandika barua kwenda bank husika kufunga account ya/za marehemu na kuleta hesabu ya pesa yote kwenye account ya mahakama, hii barua anapeleka msimamizi wa mirathi.

Baada ya hesabu kupokelewa kwenye account ya mahakama, msimamizi wa mirathi atapewa fomu ya idadi ya wanufaika/ warithi ajaze mgawanyo wa pesa yote ya marehemu kwa wanufaika bila kuzidisha hesabu wala kupunguza kwa kile kilichopo kwenye account.

Mkishakamilisha kujaza hizo form na kuzirudisha mahakamani zikiwemo copy za card zenu za bank basi kifuatacho ni kusubiri kwa muda kama wa mwezi mmoja utasikia msg kwenye simu muhamala umeshasoma kwenye account zenu simple as that.

Kama kuna vitu sensitive unaona vinakusumbuwa nicheck private nitakupa muongozo wote, hakuna kitu kinaniuma kama mtu anafariki halafu pesa zake zinapotea kwa sababu ya kukosa backup tu na baadaye familia inaishi kwa dhiki wakati marehemu aliwaandalia maisha na future nzuri.
 
Pesa haingii mahakamani isipokuwa mirathi ikitoka ikiwa imekubaliwa , bank wanatoa chek ya balance iliyopo kwenye account ya marehemu , chek haiwez kutoa pesa mpka igongwe muhuri wa mahakama husika iliyosimamia hiyo mirathi, halafu inarudishwa bank, pesa zitatolewa ikiwa warithi wote mliotajwa kwenye mirath mkiwepo bank kaona maelekezo mengi naona kaamua kumfupishia hapo.
Duhh mkuu asante kwa mchango wako....ila watu wametiririka vitu tofauti...
Itabidi nipitie sheria ya mirathi..
 
Kuna members wamekupa maelezo sahihi ila ngoja nikunyooshee kidogo.

Je wewe ni mnufaika wa hiyo mirathi, kama ndio je hizo pending transaction zinatalajiwa kuingizwa lini kwenye hiyo account?

Kama ni hivi karibuni subilini msifunguwe mirathi kwanza pesa iingizwe.

Pesa ikishaingizwa mnafunguwa mirathi ambapo utaratibu ni kwenda mahakamani na mukhtasari wa kikao cha familia ambao mmeteuwa msimamizi wa mirathi, mukhutasari ugongwe muhuri wa serikali ya mtaa, ni vizuri mkiandika kwa mkono msichape tafuteni mwanafamilia mwenye muandiko mzuri atawaandikia.

Mkishafunguwa mirathi mahakamani kama hakuna malumbano yoyote ya kifamilia kugombea chochote shauri linapelekwa faster na msimamizi wa Mirathi anateuliwa na mahakama na anapewa barua ya utambulisho wa msimamizi wa mirathi.

Sasa hapo ndipo mahakama itaandika barua kwenda bank husika kufunga account ya/za marehemu na kuleta hesabu ya pesa yote kwenye account ya mahakama, hii barua anapeleka msimamizi wa mirathi.

Baada ya hesabu kupokelewa kwenye account ya mahakama, msimamizi wa mirathi atapewa fomu ya idadi ya wanufaika/ warithi ajaze mgawanyo wa pesa yote ya marehemu kwa wanufaika bila kuzidisha hesabu wala kupunguza kwa kile kilichopo kwenye account.

Mkishakamilisha kujaza hizo form na kuzirudisha mahakamani zikiwemo copy za card zenu za bank basi kifuatacho ni kusubiri kwa muda kama wa mwezi mmoja utasikia msg kwenye simu muhamala umeshasoma kwenye account zenu simple as that.

Kama kuna vitu sensitive unaona vinakusumbuwa nicheck private nitakupa muongozo wote, hakuna kitu kinaniuma kama mtu anafariki halafu pesa zake zinapotea kwa sababu ya kukosa backup tu na baadaye familia inaishi kwa dhiki wakati marehemu aliwaandalia maisha na future nzuri.
Asante sana maelezo yako yanaeleweka.
Na je kama baadhi ya wanufaika kama wazazi ambao ni wazee wa kijijini hawana account bank??
 
Ya mtu binafsi...si unajua kibongo bongo

Jitahidini tu kumalizana nayo, Sasa a afanyaje biasha? Sole proprietor? Analipaje kodi? Hii ngumu Sana, labda kama ni hela ndogo, lakini kama ni mamilioni, msiendeleze mwaweza kurithi matatizo ya mpendwa wenu.
 
Sawa asante sana. Ntaenda pia bank. Maana secretary wa pale masjala sijamuelewa kabisa. Eti na hela zilizopo humo zinahamishiwa kwenye account ya mahakama??
Ukitoa report to Mahakamani au Bank account wana freeze wana mark no debit,
 
Wakuu habari zenu?

Ninaomba msada na muongozo kuhusu hili jambo. Mfano kuna account bank ambayo mhusika wake alishafiriki ila warithi wa marehemu wangependa account isifungwe na kisheria waruhusiwe kuisimamia kwa muda flani kwakuwa kuna miamala ya fedha (za kibiashara) ambayo bado inaingia kwenye hiyo account. Inawezekana?
Wewe unataka uoperate akaunti ya mfu kama nani?

Mbona mnajitakia matatizo maishani?

Mtu akifa utaratibu toa taarifa mahakamani na Bank

Immediately Bank wakiwa na Uthibitisho wa hati ya kifo au taarifa yenye uhalisia lazima akaunti wai freeze au wana mark no debit ili watu wasitoe pesa yeyote kusubiri amri ya Mahakama

Mahakama watawahitaji warithi kama kuna wosia wa kisheria hakuna haja ya mavikao ya Familia, Kama wosia hakuna lazima familia ikae na wajadili, Familia ni watoto, mke, wazazi wa Marehemu na wote waliokuwa tegemezi kwa Marehemu hasa wasiojiweza

Muhtasari wa kikao na cheti cha kifo, Hakimu a Naambatanisha na kupeleka Bank kwa ajili ya hatua zingine

Je Marehemu alikuwa na akaunti ya aina gani? Kampuni au Binafsi

Kama kampuni, Vikao vya shareholders vitafanyika kulingana na Memorandum na Articles of association zina state kitu gani mtu akifa?

Kwa individual akaunti lazima ifungwe huo ndio utaratibu wa mahakama labda kama kwenye akaunti ilikuwa ni Joint ya watu wawili kuna exception zinaweza kufanyika kisheria kuondoa picha na signature ya mfu akabaki mzima
 
Inaweza kutumika kama hela inayotoka hapa ni kwaajili ya matibabu au ada za wanafunzi kwa kutumia Certificate of Emergency.
Idhini ya kufanya hivyo inakuwa mikononi mwa mahakama kama mchakato wa kumpata msimamizi wa mirathi haujakamilika.
 
Wewe unataka uoperate akaunti ya mfu kama nani?

Mbona mnajitakia matatizo maishani?

Mtu akifa utaratibu toa taarifa mahakamani na Bank

Immediately Bank wakiwa na Uthibitisho wa hati ya kifo au taarifa yenye uhalisia lazima akaunti wai freeze au wana mark no debit ili watu wasitoe pesa yeyote kusubiri amri ya Mahakama

Mahakama watawahitaji warithi kama kuna wosia wa kisheria hakuna haja ya mavikao ya Familia, Kama wosia hakuna lazima familia ikae na wajadili, Familia ni watoto, mke, wazazi wa Marehemu na wote waliokuwa tegemezi kwa Marehemu hasa wasiojiweza

Muhtasari wa kikao na cheti cha kifo, Hakimu a Naambatanisha na kupeleka Bank kwa ajili ya hatua zingine

Je Marehemu alikuwa na akaunti ya aina gani? Kampuni au Binafsi

Kama kampuni, Vikao vya shareholders vitafanyika kulingana na Memorandum na Articles of association zina state kitu gani mtu akifa?

Kwa individual akaunti lazima ifungwe huo ndio utaratibu wa mahakama labda kama kwenye akaunti ilikuwa ni Joint ya watu wawili kuna exception zinaweza kufanyika kisheria kuondoa picha na signature ya mfu akabaki mzima
Punguza povu relax... una point nzuri ila ukipunguza jazba utaeleweka vizuri zaidi
 
Back
Top Bottom