Akaunti ya Benki ya mtu aliyefariki

Kwani magufuri alikuwa na account ngapi?...ridhikeni na kile mlichopewa kipindi alipokuwa hai..mtu amehangaika kuwapa vitengo nyeti serikalini.bado unalalamika mkuu
 
Kwa ushauri wa haraka peleka cheti cha kifo bank wafreez hizo account kabla lolote halijaendelea kufreez account Sio lazima uwe msimamizi Wa mirathi.

Mradi wakiwa na uthibitisho mwenye account kafariki wanaziblock Kwa usalama zaidi

Huku mkiendelea na utaratibu mwingine
 
kwenda kote benki mara mhakamani halafu hujui kuna sh ngapi ghafla unakutana na 200 TSHS.
 
Mkuu Account zinafungwa pesa zisitoke tu au kama unataka kuweka pesa napo itashindikana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mke na watoto wanaweza kuitumia kwa muda tu kutoa pesa ATM kuna baadhi ya familia wazaz Wana wapa watoto namba za Siri za card, kwaiyo mke na watoto wanajua password, mfano za Baba, mama, kaka na dada

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe inawezekana.... Leo mhudumu pale mahakamani anasema eti ni lazima ifungwe
Uyo muhudumu ana cheo gani? Usikute ni karani Tu wa mahakama kujitia ujuaji.

Suala lako linawezekana dear, muhimu msimamizi wa mirathi awasilishe ombi lake kwa maandishi mbele ya hakimu anayeisikiliza Hilo shauri.

Hakimu kwa niaba ya msimamizi wa mirathi atatoa order kwa meneja wa bank kumuomba hiyo account isifungwe kwa sababu zitakazoainishwa.

Muhimu ni kukimbizana na muda.
 
kwenda kote benki mara mhakamani halafu hujui kuna sh ngapi ghafla unakutana na 200 TSHS.
na hapo umesafiri kutoka kijijini ileje zaidi ya mara mbili kuja mjini kufuatilia pengine zaidi ya kilo 4 ishakutoka afu unakutana na balance radio frequency 104.94 fm mgawanyo uende kwa watu wa5.
 
Sawa asante sana. Ntaenda pia bank. Maana secretary wa pale masjala sijamuelewa kabisa. Eti na hela zilizopo humo zinahamishiwa kwenye account ya mahakama??
Ninachokiona ni kuwa uyo secretary anafanya kazi isiyomuhusu.
Mtu anapofariki na baada ya msiba kuisha ndugu hukaa kikao, kikao kitateua msimamizi wa mirathi, orodha ya Mali alizoacha marehemu na madeni huorodheshwa.

Baada ya Hapo msimamizi wa mirathi ataenda mahakamani akiwa na muhtasari wa kikao na cheti cha kifo kwa ajili ya kufungua shauri. Utaambiwa ulipie Ada ya mahakama then shauri hupangiwa hakimu wa kusikiliza.

Kumbuka mpaka kufikia hatua hiyo bank Haina taarifa Kama mwenye account amefariki. Anayetoa taarifa za kufariki kwa mteja na kutaka account ifungwe ni hakimu anayeisikiliza shauri husika Sasa andika Maombi kwenda kwa hakimu kumuomba hiyo account isifungwe ww ukiwa Kama msimamizi wa mirathi na uoneshe Maombi hayo ni maamuzi ya pamoja ya wategemezi wa marehemu.


Hakimu akiridhia ataandika barua kwenda kwa meneja kumtaka asifunge hiyo account kwa sababu mlizoorodhesha.

Ila ukweli ni kwamba account ya marehemu inapofungwa fedha huamishiwa kwenye account ya mahakama iliyopo bank kuu wakati tukisubiri hukumu la shauri la mirathi kwa ajili ya utekelezaji.

Pole dada, epuka kupokea maelekezo kutoka kwa wasiohusika.
 
Inategemeana

Akaunti huwa ziko za aina mbili yaani binafis ( personal account) - Hizi mtu akifariki ndugu watakaa kikao cha familia, watateua executor au administrator ( sina kiswahili chake 🙂) executor au administrator ataenda mahakamani kuomba usimamizi wa mirathi , akishapewa usimamizi wa mirathi atainotify Bank kwa kupelekea cheti cha kifo, Bank itafunga hiyo account na kupeleka salio lote BOT kisha BOT itawagawanyisha wanafamilia waliobaki pesa iliyokuwepo kwenye account kama ilivyo amuliwa kwenye shauri la mahakamani huu utaratibu unahusisha pia biashara za watu binafsi (sole proprietor) maana wakiwa wamekufa na biashara zao zimekufa pia


Kwa account ambazo ni registered business ikimaanisha umesajili BRELA na biashara inasimama kwa jina lake lenyewe kama biashara imefungua akaunti (Non personal account ) akaunti za aina hii huwa hazifungwi kwakuwa misingi ya biashara za aina hii inaelekeza kwamba mmiliki na biashara ni watu wawili tofauti (separate entity concept) - so ikitokea mmiliki amefariki Bank haitafunga akaunti ya aina hii badala yake shauri litafunguliwa mahakamani baada ya kikao cha familia kukaa ili kuteua mrithi wa hisa katika biashara hiyo au kwa kufuata maelekezo kwenye memorandum and articles of association ambayo kimsingi ndo huwa kama katiba flani kwenye hizi account


Sasa akaunti inayozungumzia ipo katika mazingira gani lakini kama imesajiliwa BRELA ...familia itakaa na kuteua msimamizi kisha atenda mahakamani kuomba usimamizi wa mirathi ya marehemu na kama hiyo biashara ina directors au shareholders wengine watakaa kikao cha bodi ya wakurugenzi na kupokea maelekezo ya familia juu ya mrithi wa marehemu kwa kuzingatia maamuzi ya shauri lililofunguliwa mahakamani

Lakini kama akaunti ilikuwa ni biashara ya mtu binafsi na haijasajiliwa BRELA hiyo account itafungwa tu
 
Nimecheka, ukirudi mwambie secretary taaluma yako ni ya uchapishaji wa hukumu mengine sio utaalamu wako, akisema kwanini mwambie pesa zinaingiaje account ya mahakama nimecheka [emoji23] ni mahakama gani hiyo ya kino
Siku hizi mahakimu wameambiwa wachape hukumu wenyewe kuepusha makosa ya uandishi ya masekretari wasiojua kitu kwenye uwanja wa sheria.
 
Na akaunti za sosho midia zinawezekana kutwaliwa na ndugu, watoto au mtu yeyote?

Kunaweza kuwa na profile inayoingiza hela.
 
Ngoja tumuulize mke wa Mengi atakuwa na experience
 
Sawa mkuu
 
Asante sana umeeleweka vyema
 
Sawa asante sana. Ntaenda pia bank. Maana secretary wa pale masjala sijamuelewa kabisa. Eti na hela zilizopo humo zinahamishiwa kwenye account ya mahakama??
Unataka kupigwa sasa hapa na hao wa mahakama. Hakuna sheria ya pesa za marehemu kuhamishiwa account ya mahakama.
 
Well said kiongozi... Hivi kwa uzoefu wako kwa mtu ambaye alikuwa muajiriwa wa serikali (mfuko wa pensheni wa PSSSF) inaweza kuchukua muda gani??
Asante sana mkuu.
Binafsi sijawahi kukutana na hali kama hiyo, so sina uzoefu hapo.
 
Unataka kupigwa sasa hapa na hao wa mahakama. Hakuna sheria ya pesa za marehemu kuhamishiwa account ya mahakama.
Kama hujui kitu kaa kimya, pesa ya marehemu account ikishafungwa na branch yake pesa yote inaingizwa kwenye account ya mahakama, then mkishajaza fomu za mahakama za wanufaika na mgao wao mahakama ndio inazigawa zile pesa kama mlivyojaza kwenye fomu mgawanyo direct kila mnufaika anaingiziwa kwenye account yake.

Hakuna wa kupewa pesa zote eti yeye ndio atawagawia wenzanke.

Ila kwenye mgao mjane lazima apate mgao mkubwa zaidi kuliko watoto ndio busara inataka hivyo mahakama inaawachia wenyewe mpange mgao wenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…