Akaunti ya Instagram ya Serikali kutumika kuwanadi wagombea wa uchaguzi wa CCM

Akaunti ya Instagram ya Serikali kutumika kuwanadi wagombea wa uchaguzi wa CCM

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Nimeliongea hili kwenye uzi wangu VYAMA VYA UPINZANI AZIENI HAPA... kuhusu ndoa ya CCM na Serikali ambapo hii akaunti inayojinasibisha kuwa ni ya serikali ikitumika kama eneo la kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama dola

Screenshot_20221115_133446.jpg

Akaunti ya Instagtam kwenye bio yake

Screenshot_20221115_133522.jpg

Hivyo inawezekana hii ni akaunti ya mtu binafsi lakini tujiulize ana mamlaka gani kuibatiza kuwa ni akaunti ya serikali ?

Je kama ni ya mtu binafsi kama watakavyokuja kujitetea, ni watu wangapi wameshaingia mtegoni na kutapeliwa kupitia akaunti hii wakiamini ni ya umma?

Katiba mpya ni suluhisho la utapeli huu wa kisiasa lakini mpaka tupate hiyo katiba ni lazima tusijidanganye kuwa wataileta

Na swali la kujiuliza, nani anafaidika na uhuni huu?
 
Acha uma.tacro hiyo ni page ya mtu binafsi. Na hiyo kuandika government organization ni mapenzi yako kuchagua unapofungua akaunti insta, serikali haiwezi kuzuia
 
Nimeliongea hili kwenye uzi wangu VYAMA VYA UPINZANI AZIENI HAPA... kuhusu ndoa ya CCM na Serikali ambapo hii akaunti inayojinasibisha kuwa ni ya serikali ikitumika kama eneo la kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama dola

View attachment 2417457
Akaunti ya Instagtam kwenye bio yake

View attachment 2417458
Hivyo inawezekana hii ni akaunti ya mtu binafsi lakini tujiulize ana mamlaka gani kuibatiza kuwa ni akaunti ya serikali ?

Je kama ni ya mtu binafsi kama watakavyokuja kujitetea, ni watu wangapi wameshaingia mtegoni na kutapeliwa kupitia akaunti hii wakiamini ni ya umma?

Katiba mpya ni suluhisho la utapeli huu wa kisiasa lakini mpaka tupate hiyo katiba ni lazima tusijidanganye kuwa wataileta

Na swali la kujiuliza, nani anafaidika na uhuni huu?
Tanzania kwa sasa hatuendi na katiba hivyo ni sawa tu.
 
Acha uma.tacro hiyo ni page ya mtu binafsi. Na hiyo kuandika government organization ni mapenzi yako kuchagua unapofungua akaunti insta, serikali haiwezi kuzuia
Imewagusa huko ulikokutaja umekurupuka kujibu

Fungua akaunti kwenye hizo platform kiaha jiiye Government entity kama utalalia godoro la nyumbani kwa usalama
 
Chama-dola cha CCM siyo chama halali cha kisiasa.

Chama halali cha kisiasa kinatakiwa kutumia ushawishi na siyo kubebwa na vyombo au taasisi za dola maana yake kiache kujivika Utawala wa Kiimla

Soma zaidi :

IPPMEDIA
https://www.ippmedia.com › habari
CCM: Tunatumia dola kubaki madarakani

7 Mar 2020 — KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ali, ... ya sifa, sifa kubwa ya dola ni kukusanya kodi ......


MIFUMO YA SIASA​

Julai 05, 2017


SIASA ,UTAMADUNI NA UTANDAWAZI
1. KUCHANGANUA MIFUMO YA SIASA ILIYOPO KATIKA JAMII ILI KUBAINI NA ATHARI ZAKE.

1. DHANA YA SIASA
Siasa;-
ni njia ya kufanya maamuzi katika taifa, mji au hata dunia nzima (siasa ya kimatatifa).

Sehemu muhimu ya siasa ni majadiliano kati ya watu mbalimbali wenye nguvu au mamlaka.

Katika demokrasia kila mtu ana kiasi fulani cha nguvu, kwa hiyo siasa ya demokrasia ina maana ya watu wote kuchangia maamuzi.

2. MIFUMO YA SIASA
Hapa chini, mifumo mingine ya kisiasa huelezwa kifupi:

Utawala wa Kifalme
ni mfumo wa uongozi unaompa mamlaka ya dola na ya serikali Mfalme. Katika mfumo huu madaraka hurithiwa na mtu wa familia ya kifalme.

Utawala wa Kiimla
ni mfumo wa uongozi unaotoa madaraka yasiyo na mipaka kwa kiongozi. Katika utawala huu watu binafsi hawana haki na uhuru katika maamuzi.

Utawala finyu
ni mfumo unaowapa wachache nguvu za maamuzi katika dola na serikali. Nafasi ya wachache hawa hutokana na haiba na uwezo wao kiuchumi, kijamii, kijeshi au kutokana na mafanikio yao katika nyanja mbalimbali za maisha. Mfumo huu ni nadra sana siku za hivi karibuni. Pia waweza kuitwa utawala wa makabaila.

Utawala wa Umma
ni utawala unaotokana na jamii kuamua misingi ya kujiongoza. Mfumo huu wa utawala hujulikana kama Utawala wa Kidemokrasia.
Demokrasia;- kwa asili neno hili limetokana na maneno mawili ya kigiriki ambayo ni demos linalo maanisha watu na kratos linalo maanisha nguvu tawala.kwa maana hiyo demokrasia ni utawala aunguvu ya watu.
Demokrasia
ni mfumo unatoa fursa ya madaraka kwa umma moja kwa moja au kutokana na kuwakilishwa.hivo tunapata aina mbili kuu;-

  1. Kuwakilishwaji
  2. Moja kwa moja(ushirikishwaji wa watu wote)……………….
na umegawanyika katika sehemu nne.
  1. Demokrasia Baguzi
ni aina ya Demokrasia inayojikita katika kulinda nguvu za kiuchumi zaidi.
  1. Demokrasia Duni
ni aina ya demokrasia inayotokana na makundi ya watu na kisha kupitia makundi hayo watu kuunda serikali mfano: chama - serikali.
  1. Demokrasia Endelevu
ni aina ya demokrasia inayotoa fursa ya usawa na kupinga matabaka katika jamii.
  1. Demokrasia Shirikishi
katika aina hii ya Demokrasia wachache hupewa dhamana na wengi katikauwakilishi wa jamii katika maamuzi.
Wachache uchaguliwa na wengi kwa njia ya Demokrasia huru na haki kwa kufuata Katiba ya nchi hiyo. Mfano: Wabunge uwakilisha wananchi wao katika kuleta maendeleo na kuishauri serikali juu ya maendeleo ya nchi.
.Misingi ya demokrasia.

  • Usawa
  • Uwajibikaji
  • Uchaguzi ulio huru na haki
  • Uhuru wa kiuchumi
  • Utawala wa sheria
  • Vyama vingi vya kisiasa
  • Haki za binadamu
  • Uadilifu.
3.ATHARI ZA MIFUMO YA SIASA KATIKA JAMII-ULIMWENGUNI.
SWALI;Kuna athari gani zinazoweza kujitokeza kutokana na mifumo hii ya siasa katika jamii na ulimwengu kwa ujumla.
4.DHANA YA DOLA
Dola
( nchi, serikali, taifa; ing. state) ni utaratibu wa kisiasa wa jamii katika eneo fulani.

Ufafanuzi wa "Dola"

Fani mbalimbali huwa na maelezo tofauti kiasi juu ya maana ya dola:
  • sheria hufundisha dola kuwa mamlaka ya jamii ya taifa; ina tabia tatu za kimsingi ambazo ni
    • eneo la dola,
    • taifa au watu wa dola na
    • mamlaka ya dola juu ya watu na eneo lake.
  • elimu jamii hufundisha kufuatana na Max Weber dola kuwa jumuiya au jamii ambayo ina mamlaka ya kukubalika ya pekee katika eneo fulani; hivyo ni uhusiano wa utawala wa watu juu ya watu unaofuata haki na sharia.
  • elimu siasa hufundisha dola kuwa muundo wa mamlaka ya umma kwa ajili ya kuratibu mambo ya umma.
  • falsafa hufundisha dola kuwa utekelezaji wa shabaha za kimaadili za kila mtu na jamii kwa pamoja, Hegel alisema dola ni mwendo wa Mungu katika historia; msingi wake ni akili inayotaka kuwa uhalisia.

Aina za Dola

Dola hutokea kwa maumbo mbalimbali kwa mfano jamhuri au ufalme. Dola inaweza kujitegemea kabisa au kuwa sehemu ya shirikisho au muungano kama Muungano wa Madola ya Amerika. Ndani ya maumbo haya kuna njia mbalimbali za kutekeleza mamlaka na kuratibu serikali kwa mfano kwa njia ya demokrasia au udikteta.

Vyombo vya Dola
Kiini cha dola ni utekelezaji wa mamlaka katika eneo fulani. Hapo kuna chombo kinachoitwa serikali chenye mamlaka haya mkononi. Serikali inaangaliwa na taasisi nyingine.

Katika madola ya kisasa kuna mgawanyo wa madaraka wa dola kwa taasisi mbalimbali:

  • bunge huamua juu ya sheria
  • serikali inatekeleza sheria
  • mahakama zinaangalia utekelezaji na kuamua kama kuna mawazo tofauti
Vyombo vingine ni matawi mbalimbali ya serikali kulingana na katiba ya dola.
NGUZO KUU ZA SERIKALI

  1. serikali
  2. Mahakama
  3. Bunge
Vyombo hivi ni vyombo vya utendaji katika nchi,shughuli hizo ni kutekeleza utoaji wa haki,mamlaka ya utendaji kutunga sheria na utekelezaji wa shughuli za umma.na kila chombo hutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa katiba.

SERIKALI UTAWALA
Ni chombo kinacho tekeleza madaraka ya utawala na chenye mamlaka kwa mujibu wa katiba, na serikali yetu hufuata misingi ya kidemokrasia na haki ya jamii.

Na wananchi ndio wenye mamalaka kamili na serikali huwajibika kwa wananchi na utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo ya nchi.


Nguzo hii huundwa na viongozi mbali mbali, kila kiongozi huyo huwa na shughuli zake tofauti za utendaji katika serikali
Source : MIFU,O YA SIASA
 
Back
Top Bottom