Rahma Salum
Member
- Sep 7, 2020
- 30
- 59
Ubalozi wa China nchini Uingereza umeomba mtandao wa Twitter kufanyia uchunguzi akaunti ya Liu Xiaoming Balozi wa nchini humo baada kuonesha kupenda maudhui ya picha ya ngono kupitia mtandao huo.
Tukio lilitambuliwa mara ya kwanza na Mwanaharakati wa haki za binadamu Uingereza na kusababisha gumzo kwa watumiaji wa mtandao wa Twitter kutaka kufahamu kama akaunti ya Balozi huyo imedukuliwa ama la.
Hata hivyo akaunti imeonesha kupenda zaidi ya chapisho moja lenye maudhui yanayo pinga Chama Tawala cha Kikomunisti nchini China.
Aidha machapisho yote yaliyo pendwa “liked tweets” yamefutwa na kubaki machapisho mawili tu ambayo yalichapishwa na Balozi mwenyewe. Balozi ana zaidi ya wafuasi 85,000 katika akaunti yake rasmi.
Septemba 9 kupitia maelezo Ubalozi wa China umeitaka Twitter kufungua uchunguzi ili kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo.
“Hivi karibuni baadhi ya wanaopinga China wameonesha dalili ya kushambulia akaunti ya Twitter ya Balozi Liu Xiaoming na kutumia njia ya kurudufu ili kudanganya Umma. Ubalozi wa watu wa China unalaani vikali tabia hiyo” Chapisho la Ubalozi wa China
Balozi Xiaoming ameritwiti “retweet” chapisho hilo na kuongeza maelezo yenye ujumbe “a good anvil does not fear the hammer”
Chanzo CNN