Akaunti za Belle 9 Mitandaoni zavamiwa; Diamond atukanwa

Belle 9: Mimi sina tatizo na Diamond, ni baada ya watu kuhack akaunti yake na kumtukana Diamond

Watu wasiojulikana wamehack akaunti ya facebook ya msanii Belle 9 na kuweka post yenye picha ya msanii Diamond na kuandika maneno yanayoashiria matusi ya nguoni.



Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Belle 9 amesema yeye anajulikana sio msanii wa kufanya vitu kama hivyo.

“Mimi sina tatizo na msanii wala sina upande wowote,” alisema Belle 9.

“Hili ni tatizo kama matatizo mengine, ni geni kwangu kwa sababu halijawai tokea lakini kwa wasanii wengine yalishatokea.

Kwa hiyo naweza sema bado watu wangu wanaendelea kurekebisha tatizo na kuirudisha akaunti yangu. Mimi naimani kuwa watu wameelewa kwa sio mimi kwa sababu mimi sio mtu wa mambo hayo,” aliongeza Belle.
Chanzo: Bongo5
 
Habarini!

Naona leo Bell 9 kaingia kwenye headline huko insta na anapokea matusi ya kila aina ya nguoni hadi ya kwenye ndala....Anachambwa na Issue zake zina kuwa Exposed sana hadi aibu pamoja na Upole wake wote leo watu wanamtolea uvivu huko,watu wamevurugwa hata wale waliokuwa wanampenda Bell Tisa leo wamevurugwa

Eti anatafuta kick mara sijui nini yaani ni vurugu tupu huko Insta! Bell 9 hili balaa hata lisahau anajaribu kujitetea wapi watu hawamuelewi

Unajua kafanya nini Bell 9 kwenye Account ake alipost picha ya Diamond platnumz na caption yake akawa amemtukana hapo ndo alipo chokoza watu huko Insta! ila yeye anadai account ake ilikuwa hacked lakini watu hawaelewi
 

Attachments

  • 1456994639221.jpg
    38.1 KB · Views: 52
Kwakuwa Chibu si mtu wa kukurupuka imekubeba mpk unaelezea kilichotokea kwa ufasaha ila wangekuwa wengine apo washakujibu.kabla ata huja sahihi maneno yako
 
Mashabiki wengine wasengenyaji sana..Dogo ameshatoa maelezo ila mijitu haielewi..Kweli mapenzi ni uchizi
 
Belle 9 si wa hivo hanaga shida na mtu.
 
Mashabiki wengine wasengenyaji sana..Dogo ameshatoa maelezo ila mijitu haielewi..Kweli mapenzi ni uchizi

Insta imekaa kimajungu sana kwa kuwa watumiaji wake wengi ni type ya zile za pwani zenye ujuha ndani yake na huziambii kitu...MTU kapata tecno kwa USAID unadhani ataificha tabia yake hata kwa mbindeee. Hahaaaaaaa ingia kwenye bifu na mswazi wa pwani afu ujidai unajua fact kama zitakuokoa maana kwake ugomvi ni shibe na source of pride...lazma unyooshwe
 
acha kuonea watu wa pwani ww, kwani mange k ni mtu wa pwani ? kila mtu anatabia yake
 
Tusubiri reaction ya Simbaa atakaporudi DUBAI
 
'we we nakutaka wewe,nakutaka wewe nakutamaaniiii' moja ya mstari kwenye wimbo wa Belle9,Siukumbuk Jina
Mhhhhhh hakuna wimbo wa Belle9 nisioujua ila huu mstari mbona kama sijawahi kuusikia?
Au ni huu wimbo mpya nini?Maana bado sijausikiliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…