Akaunti za Belle 9 Mitandaoni zavamiwa; Diamond atukanwa

Akaunti za Belle 9 Mitandaoni zavamiwa; Diamond atukanwa

Kisambo

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2014
Posts
845
Reaction score
514
Kupitia Account yake ya Instagram Belle 9 Amepost Picha ya DiamondPlatnumz na Kuporomosha Matusi ya Nguoni
ImageUploadedByJamiiForums1456961916.194319.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1456961964.510547.jpg

================
================
Belle 9: Mimi sina tatizo na Diamond, ni baada ya watu kuhack akaunti yake na kumtukana Diamond

Watu wasiojulikana wamehack akaunti ya facebook ya msanii Belle 9 na kuweka post yenye picha ya msanii Diamond na kuandika maneno yanayoashiria matusi ya nguoni.

Belle99.jpg


Akizungumza na Bongo5 Alhamisi hii, Belle 9 amesema yeye anajulikana sio msanii wa kufanya vitu kama hivyo.

“Mimi sina tatizo na msanii wala sina upande wowote,” alisema Belle 9.

“Hili ni tatizo kama matatizo mengine, ni geni kwangu kwa sababu halijawai tokea lakini kwa wasanii wengine yalishatokea.

Kwa hiyo naweza sema bado watu wangu wanaendelea kurekebisha tatizo na kuirudisha akaunti yangu. Mimi naimani kuwa watu wameelewa kwa sio mimi kwa sababu mimi sio mtu wa mambo hayo,” aliongeza Belle.

Chanzo: Bongo5
 
Duhhh hayo matusi kama ya mwantumu sidhani kama yanaweza kutoka kwa belle Tisa.....afu mambo ya wema,zari, diamond na kiba kama wimbo wa taifa tumeshachoka...
Leteni hata habari za bibi Cheka bhasi tuvutiwe alau kidogo
 
Sio mbaya kama mtu kakuudhi mfanyie kile ambacho roho yako itakufanya ujiskie vizuri.... Kama diamond kazingua atukanwe tu kwani ye ndo nani!!
 
Kwanini ni account zao tuu kila Siku zinahakiwa?
 
huyu bele asiyekuwa kila mwaka kumbe naye yumo.
 
Back
Top Bottom