Akaunti za mitandao ya kijamii (FB & IG) ya Humphrey Polepole haipatikani tena

comrade_kipepe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2019
Posts
8,748
Reaction score
18,096

Kwa hiyo sasa hivi jamaa atakuwa amezungukwa na watu 6 mmoja kakaa kwenye kiti kama nilivyoota jana huku yeye kapiga magoti anatoa password na email watu wanafuta tu account zake zote, halafu baaada ya hapo sijui hatua gani itafuata
 
Aisee hii ni dalili mbaya mbaya mbaya mno.

Wameona kumteka haitoshi wamefuta mpaka na account yake ya instagram kufuta kumbukumbu ya matukio yote aliyoyasema hadharani.

Nchi inatisha, ndani ya miaka hii minne ya awamu ya sita matukio ya kiuhalifu yanazidi kuongezeka kila kukicha.

Simanzi na huzuni zinazidi kutawala kila kukicha.

Na mpaka uchaguzi huu uishe tutakiona cha mtema kuni.

CCM out , mmeshindwa kusimamia amani ya nchi, wananchi tunaishi kwa mashaka sana.

Wananchi hatuna uhakika wa kulala na kuamka salama majumbani mwetu na hata tukitoka hatuna uhakika wa kurudi salama.
 
Taarifa za muda huu tayari akaunti ya Instagram na Facebook ya aliyekuwa balozi nchini Cuba, Humphrey Polepole imeondolewa rasmi😭😭😭
 
Taarifa za hivi punde akaunt ya facebook ya aliyekuwa balozi wa tanzania nchini CUBA tayari imeondolewa rasmi na watekaji 😭😭 balozi ameona isiwe tabu kawapa password zake.
Mungu mlinde huko alipo 😭😭😭
 
Write your reply...safi sana hapa namsikiliza mama samia kwa radio amatema madini tu kwa aman kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…