Akidi ya Baraza la ardhi la kata

Akidi ya Baraza la ardhi la kata

DENAMWE

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2019
Posts
862
Reaction score
871
Naomba kufahamishwa idadi/akidi ya watu/wajumbe wanaoruhusiwa wakati wa kuamua kesi kwenye baraza la ardhi la kata.

Hapa namaanisha ni wajumbe wangapi wanaotakiwa kuwapo kwenye kikao cha kutoa uamuzi wa kesi iliyowasilishwa barazani.
Katibu anapatikanaje?

Je, Katibu ni anaruhusiwa kupiga kura?
 
UNAJUA NINI KUHUSU BARAZA LA ARDHI LA KATA ?

NA BASHIR YAKUB -


Tunapozungumzia mgogoro wa ardhi tunazungumzia mgogoro katika viwanja, mashamba, nyumba na majengo. Wengi wetu tunapokutwa na migogoro ya ardhi hukimbilia mahakama za wilaya au mahakama kuu ya ardhi. Lakini tunasahau kuwa lipo baraza la ardhi la kata ambalo baadhi ya migogoro haifai kwenda huko wilayani au mahakama kuu kabla ya kupitia hatua hiyo. Makala yataeleza kuhusu baraza la ardhi la kata na mashauri yanayotakiwa kuanzia hapo.

1.NGUVU YAKE NI KATIKA KATA TU.
Baraza la ardhi la kata ni mahakama ya ardhi katika kata husika . Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 10 ( 1 ) cha sheria ya mahakama za usuluhishi wa migogoro ya ardhi. Baraza hili mipaka yake ni katika kata husika kwa maana ya kuwa mipaka ya kata ndio mamlaka yake kijiografia.

Kwa maana hii kila kata hutakiwa kuwa na baraza lake la usuluhishi wa migogoro ya ardhi . Baraza la ardhi la kata fulani haliwezi kuvuka mipaka na kwenda kuamua mgogoro wa ardhi wa kata nyingine.

2. JE INATAKIWA WAAMUZI WANGAPI KATIKA BARAZA.
Unapokuwa na mgogoro katika baraza hili ni muhimu kujua ni watu wangapi wanatakiwa kuamua mgogoro wako. Mara kadhaa hasa huko vijijini waamuzi katika mabaraza haya wamekuwa wakijikalia tu na kutoa maamuzi pasi na kuzingatia akidi.

Unapaswa kujua kuwa kuna akidi maalum ya kisheria na hivyo kabla ya kuamuliwa mgogoro wako ni vyema ukahoji akidi hasa ikiwa haijatimia.

Kifungu cha 14( 1 ) kinasema kuwa vikao vya usuluhishi vya baraza vitakaliwa na wajumbe wasiopungua watatu huku mmoja akitakiwa kuwa mwanamke (kama wakiwa watatu kwa mfano (nyongeza yangu). Hii ni akidi ya kisheria na hivyo yafaa ujue kuwa unayo haki ya kuhoji ikiwa akidi hii haijatimia.

Ni muhimu kutoruhusu kikao kuendelea ikiwa akidi haijatimia kwakuwa maamuzi yatakayotolewa na akidi pungufu kisheria yatakuwa batili. Kwahiyo hata kama umeshinda ushindi wako utakuwa ni kazi bure.

3. JUMLA YA WAJUMBE
Kifungu cha 11 cha sheria ya mahakama za usuluhishi wa migogoro ya ardhi kinasema kuwa baraza la usuluhishi litakuwa na wajumbe wasiopungua wanne na wasiozidi nane . Kati yao watatu inabidi wawe wanawake. Hawa ni wajumbe wa jumla ambao ndio huunda baraza zima. Zingatia hii sio akidi ya kila kikao ila ni wajumbe kwa ujumla wao.

4. KAZI KUU YA BARAZA.
Kazi kubwa ya baraza la ardhi la kata imeelezwa vyema katika kifungu cha 13 ( 1 ) cha sheria ya mahakama za usuluhishi wa migogoro ya ardhi. Kifungu kinasema kuwa kazi ya msingi ya baraza ni kutafuta amani na utulivu katika eneo husika kupitia kusuluhisha na kuwasaidia wahusika walio katika migogoro kufikia suluhu yenye maelewano katika masuala yanayohusu ardhi.

5. KUZINGATIA MILA WAKATI WA USULUHISHI.
Kwakuwa baraza hili linahusu kata sheria imetoa mwanya kwa wasuluhishi kuhusisha taratibu za kimila katika kutafuta suluhu. Hii ni kwakuwa masuala ya ardhi na usuluhishi kwa kiasi kikubwa yameambatana na mila. Sheria inaamini kuwa kwakuwa wasuluhishi watakuwa wanatoka kata husika basi pia watakuwa wanajua taratibu za kimila za eneo husika.

Hii ni kutokana na kifungu cha 13 ( 3 ) kinachosema kuwa baraza katika kufanya kazi zake za usuluhishi litahusisha kanuni yoyote ya kimila inayohusu usuluhishi.

Kifungu kinasema kuwa ikiwa taratibu za kimila hazitatumika basi kanuni za maamuzi ya asili ( principle of natural justice) zaweza kutumika.

6. BARAZA HALISULUHISHI MGOGORO UNAOZIDI MILIONI TATU.
Kifungu cha 15 cha sheria ya mahakama za usuluhishi wa migogoro ya ardhi kinasema kuwa baraza la kata halitakuwa na uwezo wa kusuluhisha mgogoro ambao thamani yake ni zaidi ya milioni tatu. Thamani ya mgogoro huangaliwa kwa kutizama thamani ya ardhi inayogombaniwa. Thamani ya ardhi inayogombaniwa ikizidi milioni tatu basi mgogoro huo hauwezi kuanzia baraza la ardhi la kata.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
 
Back
Top Bottom