Akihutubia Bunge la Marekani, Netanyahu alisema ni wakati sahihi wa Iran kupigwa

Akihutubia Bunge la Marekani, Netanyahu alisema ni wakati sahihi wa Iran kupigwa

Bulelaa

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
1,342
Reaction score
3,247
Israel ndilo taifa linaloongoza kwa kutengenezewa vikundi vingi vya kigaidi ili tu lisiwe na amani na pengene mpango wa viongozi wenye kutengeneza vikundi hivyo, ni kulifuta Taifa hilo.

Irani kuchangamkia vita kwa sasa dhidi ya Israel, ni Isarel baada ya kumuua Gaidi na kiongozi wa makundi ya kigaidi ya Gaza bwana Ishmael Haniyer ndani ya taifa lake.

Israel alichokifanya, alijua na ameshajiandaa fika juu ya lolote na uamzi wowote wa taifa hilo la Iran

Kuna msemo usemao, Kabala hujaingia gharama ya kujenga nyumba, ni mhimu kwanza kufahamu gharama yake na si ukurupuke tu tayari kwa ujenzi.

Unapokurupuka kuanzisha ujenzi kabla ya kujua gharama na kisha kujiridhisha iwapo gharama zake utazimudu, jiandae kuchekwa maana hutakamilisha ujenzi, utaishia njiani tu.

Myahudi siyo mpumbavu, bado anapenda kuishi kama walivyo binadamu wengine, anapenda amani kama zilivyo nchi zingine

Shida inaanzia pale kwa majirani zake ambao wao hawapendi awepo hapo, wao wanaliona ni taifa linalo kinzana mila na tamaduni za mataifa hayo ya kiarabu, waarabu wa pale, wangewafurahia wayahudi siku moja waitwe kwa jina la mungu wao, hiyo ndiyo ingekuwa salama yao

Israel Kwa kuwa wanajua wapo pale kwa nguvu ya ujuzi wao, hawana muda wa kupoteza, Wamekuwa na kazi moja tu, kuhakikisha wanakuwa salama kwa ujuzi na maarifa waliyonayo

Na ndiyo maana wamekuwa ni taifa lenye technology kubwa na ya hali ya juu kwenye mambo ya ulinzi na kiusalama na wataendelea hivo kwa sababu wanafahamu, bila ya hivo Taifa lao litafyekwa na warabu

Israel, ndilo taifa linaloijua vizuri Iran kuliko Iran kuijua Israel.

Vitendo vya kuuwawa kwa viongozi mbalimbali ndani ya aridhi ya Irani, ni kiashiria cha kwamba, Israel anaijua Irani nje ndani, na Waziri Mkuu wa Israel anaposema, ni muda sahihi wa Iran kupigwa, tayari anazo tarifa zote za udhaifu wa taifa la Iran.

Kutoka 35:31-35
31 naye amemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na akili, na ujuzi, na kazi ya ustadi kila aina

32 na kuvumbua kazi za werevu, na kufanya kazi ya dhahabu, na fedha, na shaba,

33 na kukata vito vya kutilia, na kuchora miti, atumike katika kazi za werevu kila aina.

34 Naye amemtilia moyoni mwake ili apate kufundisha, yeye, na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani.

35 Amewajaza watu hao akili za moyoni, ili watumike katika kazi kila aina, ya mwenye kuchora mawe, na kazi ya werevu, na ya mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yo yote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
 
Back
Top Bottom