BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Akili Bandia ya Bard ambayo inamilikiwa na Google ili kushindana na Akili Bandia ya ChatGPT imefanya mabadiliko.
Google Bard imeongeza upatikanaji wake kwa lugha zaidi ya 40 ikiwemo lugha ya Kiswahili. Sasa hivi unaweza kuuliza akili bandia ya Google maswali yoyote kwa lugha ya kiswahili na inajibu kwa lugha ya kiswahili.
𝗣𝗶𝗮 𝗸𝘂𝗮𝗻𝘇𝗶𝗮 𝗹𝗲𝗼 𝗔𝗸𝗶𝗹𝗶 𝗕𝗮𝗻𝗱𝗶𝗮 𝘆𝗮 𝗕𝗮𝗿𝗱 𝗶𝘁𝗮𝗸𝘂𝘄𝗮 𝗻𝗮 𝗺𝗮𝗯𝗼𝗿𝗲𝘀𝗵𝗼 𝘆𝗮𝗳𝘂𝗮𝘁𝗮𝘆𝗼:
🔘 Uwezo wa ku-pin majibu. Hivyo itasaidia kama kuna majibu ambayo ungependelea kuyahifadhi.
🔘 Ina uwezo wa kuzungumza na kuyasoma majibu kwa sauti - Read Aloud
🔘 Ina uwezo wa kuchagua urefu wa majibu; unaweza kuchagua ikupatie maelezo mengi au maelezo machache.
🔘 Sasa unaweza ku-upload picha na ikaitazama na kukupatia majibu kwa kukagua picha. Imeunganishwa na Google Lens.
🔘 Imeongeza uwezo wa ku-export kwenye Google Colab na Python Replit
SWAHILITEK