Akili gani hii mtu ananunua costa milion 100 kwa ajili ya kupewa laki 1 kwa siku

Akili gani hii mtu ananunua costa milion 100 kwa ajili ya kupewa laki 1 kwa siku

Sio biashara kichaa, hiyo pesa angeiweka benki faida yake ni ndogo sana. Piga laki kwa siku, kwa mwaka ni ngapi? Omaba tu mikosi ipite pembeni.
 
Wewe hebu tuambie wafanye biashara gani? Managed mara pikipiki ooh mara bajaji. Tuambie wewe wawekeze wapi pesa zao?
 
Biashara ni kwa wenywe akili tu

Biashara Lengo lake kubwa ni kufanya pesa isipotee Lakin iwe inazaa

Wewe mwenye Milion 100

Ambae ujawekeza na alie wekeza baada ya iyo miaka miwili yeye atakuwa anakitu ww huna
 
Kuna mshua ana malori anaweza kuwa kijiweni na wenzie mara dereva wake anatokea kwa mbali kwa miguu mzee anaanza kutukana 'we ms@@@@nge mwanaharamu k@@@@@@yo ishia huko huko usiniletee balaa! Ha ha ha ha. Lakini kuna watu wanaimudu hii biashara acha tu. Kuna majirani zangu Wapemba huwa nawaoana nje ya nyumba yao yenye uwanja mkuuuuuubwa wanacheza draft huwa najiuliza na kihererehere changu hawa vipi hawachoki kukaa. siku moja jumapili napita hapo kwao geti liko wazi niliona Nissan Civilian 8, yes nane zinafanyiwa service, daladala na zote ziko kwenye hali nzuri. Sasa wacha sisi tuendelee kusema hii biashra haifai. Hata mimi hii biashara sitaki hata kuiskia.

Kwakweli siri ya kata aijuaye mtungi...
Kuna watu wanastamina ya kukimbizana usiku kucha kukaba biashara ili ilete faida aliyokusudia.

Aahahahaa nimechekaa, ama tujaribu biashara ya bodaboda tushirikiane kumbana dereva tukiwa wawili hawezi kutuchezea, bodaboda nayo inalipa...😜.
 
Mleta mada 8ns roho ya kichawi kutea kuhangaika na biashara za watu hangaika na za kwako
 
Hii ni biashara nyingine kichaa yaani unawekeza milion 100 Kwa ajili ya laki 1 Kwa siku na hiyo pesa unalipata kkwa mbinde na siku nyingine utaletewa mpaka elfu 50.

Aisee huyu mtu anaakili timamu kweli yaani mwaka unaisha hata nusu ya Bei alionunulia kicosta chake haijarudi yaani hapo bado hata ajali haijapata ambapo inaweza kupata mzinga ukaambulia skrepa aisee mtu mweusi anasafari ndefu Sana ya utajiri duniani.
Hata zile tata na eicher hazifiki huko ni ml 65- 70 tena kipindi kile mtu akinunua moja kwa cash wanampa nyingine kwa mkopo
 
Hata zile tata na eicher hazifiki huko ni ml 65- 70 tena kipindi kile mtu akinunua moja kwa cash wanampa nyingine kwa mkopo
2015 Tata Marcopolo mpya ilikuwa 96.mil. Hiyo ya mil.70 labda ni used ambayo haijatumika sana.
 
Hii ni biashara nyingine kichaa yaani unawekeza milion 100 Kwa ajili ya laki 1 Kwa siku na hiyo pesa unalipata kkwa mbinde na siku nyingine utaletewa mpaka elfu 50.

Aisee huyu mtu anaakili timamu kweli yaani mwaka unaisha hata nusu ya Bei alionunulia kicosta chake haijarudi yaani hapo bado hata ajali haijapata ambapo inaweza kupata mzinga ukaambulia skrepa aisee mtu mweusi anasafari ndefu Sana ya utajiri duniani.
Una hoja lakini pia kwa upande mwingine sikubaliani na wewe.

Nionavyo mimi, mafanikio ya muda mrefu ya biashara hayategemei biashara unayoifanya yatategemea uwezo wa muendeshaji(imagination power). Mtu mwenye maono na biashara yake huwezi mlinganisha na mtu anayeifanya kwa kuiga mafanikio ya mwingine.
 
fatilia vizuri hii biashara mkuu, usije na hesabu za juu juu.
wengi wanaofanya daladala ya kuingiza 100k kwa siku hawanunui hiyo bei. wengi wanakimbilia nissan civilian 55M hadi 60M. aliyejiongeza atatoa 70M apate ile old na hesabu kwa gari mpya 130 hadi 150k inategemea na route.

wanaonunua hizo za M100 wanafanya special hire ama tlb ya kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine na hesabu zake zinavuka 200k kutegemea na route.

ukija njoo na unachokifaham usije na maneno ya kuambiwa utakatisha watu tamaa wanaotaka kuwekeza kwenye hii biashara.
Kama kuelewa ataelewa.
 
Back
Top Bottom