Akili inapokataa kuamini na kuukubali ukweli

Akili inapokataa kuamini na kuukubali ukweli

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
AKILI INAPOKATAA KUAMINI NA KUUKUBALI UKWELI

Kaniandikia:

"MMS kila mara unapoandika UISLAM ndipo unapochefua watu.

Ubongo wako umekataa kulikubali hilo, nami nakuacha kama ulivyo.

Lakini ujue unakera sana. Mimi ni mmoja wa wengi tunaopenda kusoma maandiko yako lakini hata para ya 1 nikiona tu mambo ya uislam naacha. Siendelei kusoma.

Tupo wengi wa aina yangu."

Nami nikampa jibu langu:

"Sishangai hilo kwani lipo siku zote wala wewe si wa kwanza.

Soma kitabu cha Historia ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni (1977)kitakufurahisha.

Historia yote ya mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika ilifutwa.

Lakini mimi waasisi wa harakati za uhuru ni wazee wangu na nikiijua historia hii na nilitambua kwa nini imefutwa.

Nimeiandika historia hii na sasa ni sehemu muhimu sana ya historia ya Tanganyika na Afrika kwa ujumla.

(Historia hii sasa ipo katika Dictionary of African Biography (DAB) toka mwaka wa 2011).

Halikadhalika ni sehemu ya historia ya Julius Nyerere awe amependa au hakupenda kwani hiyo ndiyo historia yake.

Vipi ubongo wangu ukatae historia yangu kwani huko ni mimi kujichukia.

Unadhani mimi natishika kwa wewe kusema ati mko wengi hamnisomi?

Kama wewe unavyoudhika na kusoma historia ya Waislam katika kupambana na dhulma ya ukoloni ndivyo mimi ninavyo tafakhar yaani kujifaharisha na historia ya jamii ninayotoka.

Babu yangu Salum Abdallah ni mmoja wa hawa wazalendo walipigania uhuru wa nchi hii.

Wala siwadharau wale ambao wazee wao hawakuwapo katika harakati hizi.

Isingewezekana wote wawepo.

Kama wapo wanaochefuka kama wewe basi jua pia wapo wanaopendezwa na historia hii.

Wewe unaacha kusoma kisa huipendi historia hii.
Historia ya Waislam inakuchefua.

Wako wanaoipenda historia hii na ndiyo kisa kitabu kimechapwa mara nne toka kitoke mara ya kwanza kwa Kiingereza mwaka wa 1998.

Kitabu kimependwa kwa kuwa nimeandika historia ya kweli si ile iliyowanyanyapaa wazalendo wakubwa waliounda AA na TANU wakapigania uhuru wa Tanganyika hadi ukapatikana 1961 kisa ni Waislam.

Huna sababu ya kuitesa nafsi yako uko huru kuni block."

Akanijibu:

"Mimi vitu vilivyojaa UISLAM usisumbuke kunitumia, huwa sivisomagi.

Uwe na siku njema, KK."

1664338792775.png
1664338813653.png
1664338835125.png
1664338879495.png
 
Haya kumekucha tena,

Sawa Mzee wetu tayari umetupa mwanga namna historia ya uhuru imechakachuliwa na umeshaweka kumbukumbu kupitia vitabu vyako, sasa tusonge mbele tupatie maandiko mapya ya muendelezo baada ya hao wazee wa kiislam kukomboa nchi.
 
Naitamani ile Afrika ambayo haikuwa na hizi imani zisizo asili yetu, Afrika ya upendo umoja na mshikamano wa kweli
Afrika iliyokuwa na mila, desturi na tamaduni zake zisizochakachuliwa wala kunajisiwa na tamaduni za kigeni

Leo hii kuna wengi wametengenezeana nyufa na kuwekeana mipaka kwasababu tu ya imani za kambo! Hatuna umoja tena, na mshikamano wetu uko shakani
 
Daud...
Katika kitabu cha Abdul Sykes sehemu ya tatu inaeleza nini kilitokea baada ya ukombozi.

Unaweza kuanzia hapo kisha ukaendelea na vitabu vingine vilivyoandikwa na waandishi wengine.

Kwa hakika ni somo lenye mafunzo mengi.
Tafuta hicho kitabu hapo chini:

1664341167359.jpeg
 
Kifupi tu niseme sioni sababu ya malumbano ninachokiamini kila Mwafrika aliteswa na hawa wageni sio waarabu wala wazungu na bila shaka walitukuta na Imani zetu za asili yetu hakuna sababu yoyote ya kutetea historia ya uislam au ukristu hao wote ni maharamia tu sisi tulikua na imani zetu Mzee wetu Mzee Said ukimuangalia vizuri ana vinasaba vya uarabu au tuseme Uasia flani mimi binafsi huwa namuelewa vizuri sana kwa muktadha huo anatetea asili yake kwa maana ya huo uarabu au uajemi au vinginevyo nadiriki kusema hana huruma na blacks ndio maana hawatambui wazee wa bara hata akizungumzia huwalenga walewale namaliza kwa kusema Waafrika turudi kwa Imani zetu tusichanganywe na imani za watesi wetu [emoji109]
 
Mzee wangu nimependa msimamo wako,,,siku zote ni Bora kusimamia ukweli uchukiwe kuliko kuwa furahisha watu ili upendwe.
 
Naitamani ile Afrika ambayo haikuwa na hizi imani zisizo asili yetu, Afrika ya upendo umoja na mshikamano wa kweli
Afrika iliyokuwa na mila, desturi na tamaduni zake zisizochakachuliwa wala kunajisiwa na tamaduni za kigeni

Leo hii kuna wengi wametengenezeana nyufa na kuwekeana mipaka kwasababu tu ya imani za kambo! Hatuna umoja tena, na mshikamano wetu uko shakani
Kk ni vigum saana binadamu kuwa katika mrengo mmoja, uwe wa imani au Jambo lolote lile.. amini msipotofautiana kwenye dini mtatofautiana kwenye siasa, ukabila n.k..

kwani huoni na kusikia hata kwenye hizo tamaduni na desturi wapo wanaosema zimepitwa na wakati na wengine wanasema zakale ni mzur, tayal pamegawanyika hapa.

Umuhimu ni kuvumiliana kwenye hii migawanyiko, tutofautiane ila isiwe sababu ya chuki na ugomvi

Hiyo afrika unayoitamani ww isingeweza kufika huku tuliko.
 
Okay
 
Mzee mdini sana huyu
Ila wamanyema kawaida yao kujiona waarabu na kipilipili kichwani
Ujinga mtupu
 
Naomba kujulishwa . Hao wanaoombewa kutambuliwa Kama wapigania Uhuru walikuwa wanapigania Uhuru wa waislam? He walilenga Uhuru ukipatikana Tanganyika iwe nchi ya kiislam na wasiokuwa waislam waslimishwe wote? Kwa maoni yangu Uhuru uliopiganiwa ni wa Watanganyika wote. Kama Wana harakati walikuwa waislam wengi tunawapongeza Kama Watanganyika Wala so kwa uislamu wao.
 
Niggaz...
Umeuliza swali na ukalijibu swali lako mwenyewe katika hilo swali uliouliza.
Umegusia mambo mengine na mimi nitajitahidi kukujibu kadri ya uwezo wangu.

Umeuliza kama Waislam walipigania uhuru wa Waislam peke yao?
Jibu ni hapana.

Ilitokea kuwa waasisi wa harakati hizi pale walipounda African Association (AA) wengi wao walikuwa Waislam.

Waasisi hawa majina yao ni haya: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Suleiman Majisu, Rawson Watts na Raikes Kusi.

Kwa nini Waislam walikuwa wengi?

Kleist peke yake katika hawa waasisi ndiye aliyeandika historia ya maisha yake kabla hajafa 1949 na mswada huu umechapwa kama sura ya kitabu na anasema kuwa Wakristo walikuwa wanazuiwa na viongozi wao wasijiusishe na siasa.

Lakini chama kilikuwa wazi kwa wote kujiunga na kupigania maslahi ya Mwafrika.

Hilo la kusilimisha watu sijui umelitoa wapi.

Lakini nitakupa maelezo kidogo ili ufahamu hali ilivyokuwa ndani ya AA pale New Street na haya ni kutokana na maelezo ya Kleist kama alivyoandika katika mswada wa kitabu chake kabla hajafariki.

Kleist anasema mambo mengi ya Waislam yakiwa ni malalamiko kwa serikali yalikuwa wakipitisha kupitia AA na hili wakaona si jambo lililo sawa kwa kuwa AA kilikuwa chama cha Waafrika wa imani zote.

Waislam ambao walikuwa wengi ndani ya AA wakaamua mwaka wa 1933 kuunda chama kingine kwa madhumuni ya dini yao.

Chama hiki ni Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na viongozi wake wakiwa Mzee bin Sudi (President) na Kleist Sykes (Secretary) wakati ule viongozi hawa wawili wakiwa wameshika nyadhifa kama hizo katika AA.

Nimeona nikueleze historia hii ili uelewe staha na kuheshimiana kulikokuwapo katika AA.

Hakika kama ulivyosema uhuru umepiganiwa na Watanganyika wote lakini wapo watu michango yao ilikuwa muhimu na mikubwa zaidi.

Ndiyo unaona hakuna picha Nyerere yuko na Maaskofu wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika picha zote kazungukwa na Waislam yeye akiwa na John Rupia.

Hata safari ya kwanza ya Nyerere UNO mwaka wa 1955 dhifa ya kumuaga ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika dua ya kumuombea Mungu aende na kurudi salama ilifanyika nyumbani kwa Ali Mshama Magomeni ambako kulikuwa na tawi kubwa la TANU.

Ilipokuja kuandikwa historia ya TANU na mimi kuona si historia ya kweli ya TANU kwa kuwa historia ya TANU nifahamu toka AA kwa kuwa wazee wangu ndiyo waasisi wa harakati za uhuru nikaamua kuandika historia hiyo na kuonyesha mchango wa Waislam.

In Shaa Allah tutasomeshana historia hii kwa taratibu hadi itaeleweka kwani penye ukweli uongo hujitenga.

Usikubali kutishwa na historia hii.

Hivi ndivyo ilivyokuwa hatuwezi kubadili historia.
 
Back
Top Bottom