Ndugu yangu naona unajaribu kufikiria akili ni nini ila umeshindwa kunga'mua ukaamua utumie mifano ambayo haijitoshelezi [emoji2]
Anyway nitakusaidia kukuelewesha,
Kwanza kabisa ili uwe na akili ni lazima uwe na ubongo, ila unaweza kuwa na ubongo lakini usiwe na akili nyingi,
Chukulia mfano una puto tupu (empty baloon) ambalo tulifananishe na ubongo wa mtoto aliyezaliwa leo,
View attachment 1965912
Mtoto kadri muda unavyozidi kwenda anakuwa anajifunza mambo mbali mbali kama vile majina ya watu vitu n.k pia anajifunza matendo (tabia) kwa kuangalia kutoka kwa watu wanao mzunguka, hapo anakuwa analijaza puto(ubongo) upepo (akili au kwa kiingereza mnaita mind), content zinazojazwa kwenye ubongo zote lwa pamoja ndio tunaziita akili
View attachment 1965923
Kwahiyo akishakuwa mtu mzima tunamchukulia kuwa ana akili timamu sababu puto lake(ubongo) lina hewa nyingi (akili) au content pia anakuwa na uwezo wa kuchakata hizo content kutofautisha nembo jema na jambo baya
Tunachotofautiana binadamu ni wingi wa upepo (akili) mfano mtu aliyesoma sana tunasema ana akili nyingi sababu puto lake kalijaza content muhimu mnaita maarifa,
You can not create something from nothing
Newton asingegundua law of gravity kama asingesoma maandiko ya GALILEI GALILEO, Michael Faraday asingegundua laws of electrolysis kama asingejichimbia kusoma vitabu kwenye library ya baba yake, R.Ohm asingegundia resistance kama asingesoma vitabu alivyokuwa analetewa aviwekee ma cover,
Kimsingi akili ni mkusanyiko wa taarifa mbali mbali kwenye ubongo ambao hutengeneza taarifa ya kitu, vitu au maarifa