"Mustakabali wa akili bandia barani Afrika ni upi?" Wakati swali hili linaingizwa kwenye majukwaa kadhaa ya akili bandia mitandaoni, jibu lake huwa ni: "mustakabali wa akili bandia barani Afrika umejaa fursa… utaonesha nafasi muhimu katika sekta mbalimbali kama vile huduma za afya, kilimo na elimu." Hakika, serikali na makampuni ya nchi za Afrika hivi karibuni yanaonekana kukubaliana na maoni haya, na kupitia ushirikiano wa kimataifa, yanaendelea kuagiza na kutumia teknolojia ya akili bandia, ili kusaidia maendeleo ya uchumi wa Afrika kuelekea kuwa wa kidijitali na kiakili.
Kuhusu ushirikiano kama huo, wataalamu wengi wa akili bandia wameupongeza sana, lakini pia kuna sauti nyingine, kwa mfano baadhi ya taasisi za washauri bingwa wa Marekani zinadai kuwa "akili bandia inaweza kudhoofisha nafasi ya Marekani kama kiongozi wa dunia" , kama kauli hiyo, Sauti ya Marekani VOA hivi karibuni ilichapisha makala yenye kichwa "Akili Bandia: Ushindani mpya kati ya Marekani na China barani Afrika", ikifichua kuwa akili bandia inazidi kuwa chombo kipya kwa Marekani kuchochea "mashindano ya mataifa makubwa" barani Afrika. Na wiki hii habari kuhusu timu ya Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani kukiri kuiga modeli ya akili bandia ya wanasayansi wa China na kuomba radhi hadharani imezua mjadala mkubwa tena kwenye majukwaa ya kijamii.
Afrika Kusini ni moja ya nchi za Afrika zinazokimbiza haraka katika akili bandia, na ina ushirikiano mpana na China na Marekani katika akili bandia. Mwezi uliopita Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo ilianzisha kitengo cha utafiti wa akili bandia kwa ulinzi. Alipoulizwa kuhusu ushiriki wa nchi mbili hizo, Naibu Mkurugenzi wa kitengo hicho Wayne Dalton alisema, "Afrika inahitaji suluhu za changamoto za Afrika, China na Marekani watakuwa na nafasi nyingi za kusaidia kutimiza mikakati na malengo ya akili bandia." Ni wazi, nchi za Afrika ikiwemo Afrika Kusini hazikubaliani na kitendo cha Marekani kujaribu kutumia akili bandia kuchochea "mashindano ya mataifa makubwa" barani Afrika, na zinatarajia China na Marekani kuwa washirika wazuri katika kukuza maendeleo ya sekta hii. Kuhusu hilo, msemaji wa ubalozi wa China huko Washington, Liu Pengyu, alisema hivi karibuni: "China inataka kushirikiana na pande zote zikiwemo nchi za Afrika na Marekani katika akili bandia, kuhakikisha akili bandia inapiga hatua kuelekea maendeleo na ustaarabu wa binadamu."
Marekani kama taifa lenye nguvu duniani, pia ni mojawapo ya nchi zinazoongoza katika maendeleo ya akili bandia duniani, ina jukumu na wajibu wa kusaidia nchi za Afrika kuwa washiriki muhimu wa maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani, na kunufaika na faida za maendeleo ya akili bandia, jambo hili ni muhimu kwa nchi zinazoendelea duniani.