Kumbuka ili uweze kufanikiwa katika mambo yote kwenye maisha yako, yaani; Kiuchumi, Kijamii, Kisiasa, Kiutamaduni, Kiteknolojia, Kiafya, Kidini na Kielimu kwa namna yoyote ile lazima uwe na KUMBUKUMBU na AKILI timamu. Mtu asiye na akili timamu wala kumbukumbu ni mfu anayeishi, hawezi kuona vinavyoonekana wala kusikia vinavyosikika, kiufupi anapishana na fursa nyingi sana za kufanikiwa katika maisha. Ni heri mbwa aliye hai kuliko simba aliyekufa.
Kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wenye magonjwa ya akili duniani. Magonjwa ya akili ni matatizo ya ubongo ambayo humfanya mtu kuwa na tabia, hisia, fikra na matendo tofauti na yale ya kawaida yanayotarajiwa katika jamii ambapo hupelekea kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha. Magonjwa ya akili yanaweza kutokana na sababu za Kibaiolojia na Kisaikolojia. Nchini Tanzania kwa siku za karibuni kumekuwa na matukio ya mauaji ya aina mbalimbali ambayo hutokea miongoni mwa watu wenye mahusiano (wapenzi), watu wa familia moja (baba, mama, watoto na ndugu wengine) na watu wengine kwa njia ya ajali, kupigana risasi, kukatana kwa vitu vya ncha kali, kuchomana moto n.k, ndiyo imepelekea kutolewa kwa taarifa za watu kuwa na matatizo ya akili ambazo zimethibitishwa na Wizara ya Afya kupitia kwa waziri wake Mhe.Ummy Mwalimu
KUMBUKUMBU NI NINI?
Ni uwezo wa kufikiri, kutafsiri na kukariri jambo uliloona, ulilosikia, ulilonusa, uliloonja au ulilohisi, yaani uwezo wa kutumia milango yako ya fahamu vizuri ili kuweza kutambua, kufafanua au kuelezea jambo.
Kwa mantiki hiyo, uwezo wa kuwa na kumbukumbu hauwezi kufanana kati ya mtu na mtu kutokana na sababu mbalimbali, baadhi ikiwa ni pamoja na kiwango cha akili, kiwango cha elimu, kiwango cha lishe, mtindo wa maisha au maumbile ya mtu. Kwa mfano; mwanaume na mwanamke, mwanaume anaweza kustahimili jambo moja kwa wakati mmoja kwa umakini zaidi akizidisha basi ataharibu moja au yote kabisa, mwanamke ni tofauti yeye anaweza kustahimili mambo zaidi ya moja na akafanya kwa ufanisi mambo yote bila kuharibu hata mmoja.
MWANAMKE ANA KUMBUKUMBU YA KUFANYA KAZI ZAIDI YA MOJA
AKILI NI NINI?
Ni hali ya kuwa na ufahamu wa kutambua mema na mabaya, yaani uwezo wa kufanya maamuzi binafsi bila shuruti. Akili inaratibiwa na ubongo, hivyo viumbe hai wote wenye ubongo wana akili, lakini akili ya binadamu ni tofauti na akili ya mnyama kwa sababu binadamu ana utashi mkubwa zaidi wa kufikiri na kufanya maamuzi.
Pia inaaminika binadamu ndiyo kiumbe mwenye uhusiano na Mungu zaidi na alipewa uweza na mamlaka ya kumiliki na kutawala dunia na vyote vilivyomo ndani yake (utiisho) kutokana na akili ya ajabu aliyonayo zaidi ya viumbe wengine.
MWANAUME ANA AKILI YA KUMILIKI NA KUTAWALA
1.Akili na Kumbukumbu kwenye Afya
Afya ni kuwa timamu au vizuri katika maeneo matatu; kiakili, kimwili na kiroho mbali na magonjwa. Afya njema hujenga kinga bora ya mwili, kinga bora ya mwili huimarisha ubongo na milango ya fahamu ambayo ndiyo chanzo cha akili na kumbukumbu.
Hapa unahitaji Akili ya kula chakula bora na kufanya mazoezi pia unahitaji Kumbukumbu ya kuzingatia dondoo za afya na kufanya vipimo vya uchunguzi wa afya (check up)
Hivi karibuni kumezuka ugonjwa wa COVID-19 ambao umebadilisha mfumo wa maisha ya watu kote duniani. Ni ugongwa unaoathiri mfumo wa upumuaji na unawaathiri watu wote bila kujali umri au jinsia
UGONJWA WA COVID-19
2.Akili na Kumbukumbu kwenye Elimu
Elimu ni ujuzi na maarifa anayopata mtu kwa njia ya kujifunza.
Hapa unahitaji Akili ya kuchagua elimu faafu na kupata maarifa mapya kwa nadharia na vitendo pia unahitaji Kumbukumbu ya kuweka mipango, kuweka vipaumbele na kuzingatia muda hususani unapofanya maamuzi ya kusoma/kujifunza.
Kwa dunia ya sasa elimu yoyote ile iwe ya nadharia au ya vitendo katika mfumo rasmi au usio rasmi inahitaji ujuzi wa msingi ambao ni kusoma, kuandika na kuhesabu. Elimu ni mchakato endelevu kwa watu wote wanaohitaji.
WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA
3.Akili na Kumbukumbu kwenye Kilimo
Kilimo ni shughuli ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara mashambani au bustanini.
Hapa unahitaji Akili ya kujua aina ya kilimo, ardhi yenye rutuba, na majira/hali ya hewa pia unahitaji Kumbukumbu ya kuchagua mbegu bora, mbolea na dawa za kuua wadudu waharibifu.
Kilimo ni uti wa mgongo wa uchumi wa mataifa mengi duniani ikiwemo Tanzania, kwa sababu huzalisha chakula kwa binadamu na mifugo pia malighafi za viwandani. Kwa sasa ushindani umekuwa mkubwa ili uweze kupataza faida au kipato kupitia kilimo lazima uzalishe kwa ubora. “Kilimo ni ajira kilimo ni biashara”,
KILIMO BIASHARA
5.Akili na Kumbukumbu kwenye Uchumi
Uchumi ni mchakato wa kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya uzalishaji wenye faida.
Hapa unahitaji Akili ya kuweka akiba, kupanga bajeti na kuwa na vitega uchumi (kuwekeza) pia unahitaji Kumbukumbu ya kupanga mapato na matumizi sahihi ya fedha.
Zipo rasilimali watu, rasilimali fedha, rasilimali miundombinu, rasilimali maji, wanyama na mimea, rasilimali asilia n.k Uchumi wa nchi unaweza kupanda au kushuka kwa kuangalia viashiria kama vile; pato la mtu mmoja, pato la taifa na kiwango cha ajira.
RASILIMALI FEDHA
4.Akili na Kumbukumbu kwenye Siasa
Siasa ni mfumo wa uongozi wa kidiplomasia unaofuata misingi ya katiba na demokrasia.
Hapa unahitaji Akili ya ujuzi wa mawasiliano (communication skills) hususani ujuzi wa kuongea pia unahitaji Kumbukumbu ya kuelewa katiba na kutekeleza ahadi.
Siasa jukumu lake kubwa ni kuchochea maendeleo katika nchi kwa mipango ya muda mfupi na muda mrefu. Ndani ya siasa kuna serikali na serikali ndiyo chombo kinachobeba sera na dira ya taifa. Huu ni mwaka wa sensa kiserikali na ni haki ya kila mwananchi kuhesabiwa ili kupata idadi ya raia wote nchini na kusaidia mipango, huduma za kijamii na maendeleo ya nchi kwa ujumla.
6.Akili na Kumbukumbu kwenye Sayansi na Teknolojia
Sayansi ni mbinu za namna ya kutumia maarifa mapya kufanya vitendo vya ubunifu.
Teknolojia ni ujuzi wa kisayansi wa kutumia ufundi na utaalamu kuzalisha vitu vya kisasa.
Hapa unahitaji Akili ya kufanya utafiti, uvumbuzi, ubunifu na majaribio pia Kumbukumbu ya kuzalisha wataalamu na kujifunza kwa walioendelea.
HADUBINI
Kumbuka Akili ni Maarifa (kujua siri zilizojificha kuhusu kitu fulani) na Kumbukumbu ni Hekima (kujua nifanye au niseme nini kwa wakati gani); kwa hiyo ili uweze kufanikiwa na kustawi katika mambo yote unahitaji AKILI na KUMBUKUMBU.

Upvote
0