Akili ni nini?:Swali lililokwamisha mjadala wa Mshana na Kiranga.

Akili ni nini?:Swali lililokwamisha mjadala wa Mshana na Kiranga.

Ila kiranga ameshamjibu kwama Akili ni akili ila kiranga amegomea jibu
wewe jamaa ndio jibu gani hili ambalo halina definition..

fogoh2 ninani "??"? fogoh2 ni fogoh2...
 
Kuna thread ya Mshana Jr inayosema kuwa Kiranga sio atheist ni non-believer inaelekea page ya 50 ikiwa imekwama kwenye neno "akili...".
Kwa upande wangu naona mjadala ule hauna maana yoyote kwasababu kila mtu anakwepa kumjibu mwenzie swali moja tu.

Mshana:Kiranga una akili au hauna akili?
Kiranga:Akili ni nini?

Eeh bhana eh!mjadala umetumia karibu posts 700+ kwenye kipengele hiko bila mafanikio.Mshana hataki kutoa maana ya akili na kiranga hataki kusema kama anazo bila kuambiwa akili zipi.
Kwa ujumla naona wale jamaa wanajidhalilisha tu...
Kwahiyo ulitaka Kiranga ajitoe akili kwa kujbu kuwa hana akili? au Mshana ajibu kuwa akili ni nini ili ampe Kiranga jibu?
 
Mimi wacha nijibu hilo swali lao:

Akili ni ufahamu....ufahamu hauna umbo, ni kama umeme, umeme upo na unatenda lakini hauna form, hauuoni, ni kama hewa, ipo inafanya kazi zake lakini haibebeki haishikiki.

Kiumbe chochote chenye uhai: Binadamu/Mnyama/Ndege/Mti ana vitu viwili...Akili na Roho: Akili ni ufahamu na Roho ni Uhai.

Mtu akirukwa na akili Roho ina take control, ndio maana Kichaa akisikia njaa atatafuta chakula, mti ukikosa mwanga utaona unaota kwa kufuata dirisha lilipo, Mbwa akila chakula kisichomeng'enyeka i.e. mafuta basi hujitapisha etc.

Katika hivyo viumbe, kimoja kimejitukuza sana na kujipendela kwamba kinawazidi wengine nacho ni binadamu...utasikia binadama tunasema sisi ndio tuna roho...wanyama hawana roho, au sisi tuna ufahamu, wanyama hawana ufahamu wana roho...pia tunajichanganya zaidi kuongeza neno Nafsi, eti tunasema mnyama hana roho ila ana Nafsi.

Kuna tofauti ya Akili/Ufahamu, Roho/Uhai na Nafsi/Utashi.

OVA
 
wewe jamaa ndio jibu gani hili ambalo halina definition..

fogoh2 ninani "??"? fogoh2 ni fogoh2...
Recursive definition is like image reflection on the mirror reflected from another mirror.

It will go on repetitively to infinite.
 
Hivi akili kwa kiingereza ni nini? Tuchambue mswahili anasema nini na mwingereza anasemaje ndipo tujumlishe tupate wastani. Huenda akili inategemea ubongo kama ni tabula raza basi akili ni zero
 
Ni umahiri wa kuchambua mambo na kuleta mabadiliko katika jamii. Mf. Kijiji kina ukame na maji ni shida, ukapasua akili ukagundua wamekaa juu ya maji mengi chini ya ardhi , ukatumia utaalamu ukatoboa maji na shida ya maji ikaisha . Hiyo ndiyo skili.
 
Back
Top Bottom