Akili ni nywele

Akili ni nywele

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Tukio siyo halisi.

Mtanzania mkazi wa Kijiji cha Kowak (a.k.a Home of Intellectuals) Wilayani Rorya Mzee Sebastian Obaso Ogutu (70) amedakwa na Polisi Migori–Suna County Kenya kwa kosa la kujisaidia haja ndogo na kubwa sehemu isiyoruhusiwa kwenye mtaro wa barabara kuu ya Migori–Isebania. Baada ya kukamatwa akajitetea kwa hila (uongo) kwamba anaumwa tumbo sana, na hana ela ya kulipia huduma ya choo cha umma hivyo akamwomba Askari amsamehe au amwache amalizie haja zake ndiyo ampeleke kituoni kukabili mashtaka yake, Askari akakataa kumsamehe ila akamruhusu amalizie kujisaidia (moyoni Askari akisema ndiyo nipate kidhibiti/exhibit), ikawa ni kosa, kumbe jamaa amemwekea Askari mtego kwa kujisaidia nusu haja kubwa na ndogo na kudai amemaliza, kabla hajavaa akaanza kuugulia tena tumbo tumbo tumbo akijikunyata kwa kushika sehemu ya chini ya tumbo na kurudi chini na kujisogeza mahali pengine hatua chache hivi toka alipojisaidia awali, na kujisaidia upya tena haja kubwa na ndogo na kuzoa kidogo vumbi la udongo na kunyunyuzia kwenye haja kubwa moja, ndipo akamwambia Askari sasa nimemaliza niko vizuri tunaweza kwenda.

Njiani Askari akaanza kumsulubu kidogo kidogo kwa sababu mhalifu hapelekwi kituoni kama Bibi harusi. Alipofikishwa kituoni akafunguliwa jalada na kukimbizwa Mahakama ya mji kabla haijaahirisha shughuli zake alasiri. Baada ya kujitathmini kwamba yuko nchi ngeni hana mtu wa kumdhamini akaazimia moyoni kwamba anaenda kuifanya kesi yake iwe nyepesi ili asije kupoteza muda wa kuletwa Mahakamani kila mwezi mara moja ambayo ingemchukuwa muda mrefu Mahabusu ya ugenini.

Mhalifu huyu alizua mtifuano mzito Mahakamani pale alipodai kwamba anakiri kutenda kosa, isipokuwa hakuwa kichaa wa kujisaidia hadharani mchana ila aliamua kufanya hivyo baada ya kumuona Askari aliyemkamata akivua sare za jeshi na kujisaidia hapo ndipo na yeye ambaye alipata usumbufu wa tumbo akaona kumbe hapa ni mahali sahihi pa kujisaidia madhali Askari mwenyewe mlinda sheria anajisaidia hapo.

Akamwambia Mhe. Hakimu kuwa yeye mtuhumiwa apimwe akili kuthibitisha utimamu wa akili yake. Ndipo Mhe. Hakimu akaamuru Mahakama ihamie kwenye eneo la tukio kujiridhisha na ukweli wa madai ya mtuhumiwa kwamba kuna haja mbili pale ya kwake na ya Askari, Mhe. Hakimu alipomhoji mtuhumiwa kwamba kuna ushahidi gani kuthibitisha kwamba haja hizi mbili ni za watu tofauti, mtuhumiwa akajibu kwamba pana tofauti ya wazi kwamba haja kubwa moja ni rangi ya khaki na mkojo na haja kubwa nyingine ni ya ugali wa nafaka mchanganyiko ndiyo maana rangi yake siyo khaki (kumbe moyoni akijuwa kwamba ni lile vumbi alilotia ili kuleta utofauti), akamwambia Mhe. Hakimu kwamba mtu mwenye akili timamu kama yeye hawezi kujisaidia haja mbili tofauti. Mhe. Hakimu akakubali hoja hiyo ya utetezi, Mahakama ikarudi kwenye eneo la Mahakama na Mhe. Hakimu kuagiza mtuhumiwa apelekwe kwa Daktari wa akili ambaye alimpima na kumkuta mzima.

Baada ya ripoti ya Daktari Mhe. Hakimu akaamuru mtuhumiwa arudishwe rumande kesho aletwe kwa ajili ya uamuzi/hukumu madhali amekiri kosa mwenyewe. Kesho yake alipoletwa Mhe. Hakimu akaamuru apelekwe kwa Daktari kumpima afya ya mwili na alipogundulika ni mzima pia ndipo Mhe. Hakimu akaamuru achapwe viboko 12 na kuondolewa nchini mara moja baada ya adhabu ya viboko, sambamba na uamuzi huo, Mhe. Hakimu akaamuru yule Askari (ambaye baada ya kujitetea bila kuishawishi Mahakama) afungwe miezi 6 jela na mamlaka ya nidhamu ya jeshi analolitumikia imchukulie hatua za kinidhamu za kijeshi. Askari huyu akapandishwa Karandinga la Magereza kwenda kuanza maisha jela huku akilia machozi kwa uchungu mwingi. Huyu mtuhumiwa Mtanzania akafanikiwa kujiponya kwenda jela ugenini. Kuanzia siku hiyo habari hii iliposambaa kupitia vyombo vya habari vya Kenya, raia na Askari katika mji wa Migori wanawaogopa sana Watanzania kwa uwezo wao wa akili wa kucheza na sheria ili kujinasua na kumuacha Mkenya kwenye hatia. Ikawa akipatikana Mtanzania ana hatia Migori basi moja kwa moja anakimbizwa mpakani ili kuvushwa kurudi kwao Tanzania badala ya kupelekwa Mahakamani.

Kipindi kongwe na maarufu cha "Vioja Mahakamani" cha runinga nchini Kenya kilipotaka kutumia tukio hili kuigiza kwenye runinga Mzee Sebastian Obaso Ogutu alidai wamlipe kwanza Tzs.20ml, kiasi ambacho kikundi hicho cha sanaa kilishindwa.
 
Huyo askari alifungwaje wakati mashataka yana msoma mwingine.
Je kam wote walitenda kosa moja kwa nn mmoja afungwe mwingine apigwe viboko.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
 
Huyo askari alifungwaje wakati mashataka yana msoma mwingine.
Je kam wote walitenda kosa moja kwa nn mmoja afungwe mwingine apigwe viboko.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Fuatilia kesi ya Mbowe na wenzake dhidi ya akina Kingai and Coy/Silikale ndiyo utajua kwa nini mshtaki au shahidi anaweza kufungwa.😝😝😝😝😝
 
Huyo askari alifungwaje wakati mashataka yana msoma mwingine.
Je kam wote walitenda kosa moja kwa nn mmoja afungwe mwingine apigwe viboko.

Sent from my SM-A025F using JamiiForums mobile app
Tukio siyo halisi, huu ni uga wa Chit-Chat. Hata Hakimu anayeendesha shauri hilo awezashitakiwa nalo kama mazingira yakipelekea.
 
Back
Top Bottom