The ricco king
New Member
- Aug 1, 2021
- 2
- 0
Dunia ya leo imesheheni mataifa mengi na jamii nyingi kutoka kila pande ambazo kila moja ya jamii hizo iko na desturi na utamaduni wake wa pekee. Tamaduni na desturi hizo zinaweza kuwa chanzo cha kuongezeka au kudorora kwa maendeleo katika jamii husika, mfano mzuri ni uzingatiaji wa afya ya akili ya binadamu ,jambo ambalo jamii nyingi za maghribi zimetilia mkazo ufatiliaji na utunzaji mzuri wa afya ya akili za watu wake tofauti kabisa na jamii za hapa nyumbani Afrika tukisahau kwamba akili ya binadamu ndo muhimili mkubwa wa maendeleo yote tunayoyaona duniani, bila kuitunza hakuna ambacho tungeweza kukifanya.
Afya ya akili ni nini?
Kwa mujibu wa jarida la 'Tap Elderly Women's wisdom for youth (TEWWY) Afya ya akili ni ustawi wa mtu katika ngazi kuu tatu: nafsi na utashi, akili na fikra, mwili na hisia/mihemko. Afya ya akili inahusisha sana mtu anavyofikiria, anavyojisikia na anavyotenda, mtu akifikiri vizuri ni rahisi kujisikia vizuri na kutenda mambo mazuri, akiwa na fikra hasi hata matendo yatakuwa hasi vilevile.
Kwa hiyo afya ya akili ni ile inayomwezesha mtu kujitambua uwezo wake, kipaji na hata udhaifu wake, anachopenda na asichopenda, anaweza kudhibiti na kuhimili changamoto za kawaida za kimaisha, anaweza kufanya shughuli zake za kimaisha na kuchangia katika familia na jamii kwa ujumla.
Kivipi waafrika tunaipuuza?
Hapa afrika ni nadra sana kukuta jamii inashughulika na ustawi wa akili ya mtu yoyote hata awe wa familia moja unaweza kukuta mama anamtukana hadharani mtoto wake wa kumzaa matusi ya nguoni bila kujali athari ya kitendo hicho kwenye akili ya mtoto huyo, pia serikali zetu hazijatilia mkazo sana maswala ya afya ya akili ndio maana imekua jambo la kushangaza muafrika kwenda kwenda kwa mwanasaikolojia kumweleza matatizo yanayomsumbua, ukiacha kwamba hao wanasaikolojia wenyewe ni wachache mno na hakuna elimu juu ya umuhimu wao hao wachache waliopo pia jamii imechukulia hili jambo kama ni udhaifu na mtu anabidi atatue matatizo yake mwenyewe kitu ambacho si sahihi.
Hili swala ni la muhimu na kuna muda hadi viongozi wetu huenda wakawa wana matatizo haya ya akili yaliyokosa msaada ndio maana kiongozi anaweza kufanya maamuzi yasiyoeleweka na taifa zima lakini yeye anaona sawa, hii pia ni chembechembe au dalili ya matatizo ya akili.
Chanzo cha matatizo ya akili
Kwa mujibu wa kituo cha afya cha chuo kikuu cha Dar es Salaam, matatizo au magonjwa ya akili yanaweza kusababishwa na sababu za kibaiolojia au kisaikolojia. Sababu za kibaiolojia zaweza kuwa kurithi, magonjwa ya muda mrefu kama degedege ,malaria kali, ukimwi au matumizi ya dawa za kulevya.
Sababu za kisaikolojia ambazo ndio lengo langu la kuandika makala hii katika stories of change ni pamoja na;
-Majanga, ubakaji, uvamizi, ajali, utekaji nyara, kukosa elimu, kukosa ajira n.k
-Kufiwa, kutengwa, talaka, ugoni na kufungwa.
-Kufukuzwa kazi, kukosa mshahara, kustaafu kazi n.k
-Kutokufanya vizuri masomoni au kufukuzwa shule/chuo
-Matatizo yanayowaathiri watoto kisaikolojia kama vile;
i/Kunyanyaswa kingono
ii/Kupigwa na kutengwa
iii/Kutothaminiwa
iv/Kutokupata matunzo stahiki.
Kwenye sababu hizi za kisaikolojia ndizo zinatutafuna waafrika wengi sana na ni ngumu kugundua kwa haraka ukilinganisha na zile sababu za kibaiolojia.
Jinsi sababu hizi zinavyotafuna waafrika.
Afrika ni sehemu ambayo vitendo kama unyanyasaji wa kingono, kupigwa na kutengwa kwa watoto na kunyimwa matunzo stahiki vinafanywa kwa wingi na wahusika wanaotenda vitendo hivyo hawachukuliwi hatua zozote na wanaochukuliwa hatua ni kama asilimia mbili tu ya wanaotenda mambo hayo na hii huacha majeraha makubwa mioyoni mwa waathirika wa vitendo hivyo na kuwapa sonona inayopelekea kupata matatizo ya akili na hasa vitendo hivi hufanyiwa watoto ambao hukua bila msaada wowote na jamii inawalazimisha kukaa kimya na kutosema lolote hivyo huugulia ndani kwa ndani mpaka ukubwani.
Na tatizo hili sio kwa jamii za kimasikini pekee maana mpaka kwenye familia zenye kauwezo kidogo pia wanaathirika na janga hili, mfano kuna familia mtoto asipofanya vizuri masomoni basi huonekana mjinga na hafai na familia inamtenga na kumsimanga kila kukicha na muda mwingine husemwa hadharani mbele ya wadogo zake (ikiwa yeye ni mkubwa) mambo yote yanayomhusu hupuuzwa kwa sababu tu hakufanya vizuri masomoni na wanaofanya hayo hudhani wanamfundisha lakini kiuhalisia inamuathiri sana kisaikolojia kuliko wanavyofikiria.
Sekta ya elimu pia inachangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa matatizo ya akili Afrika, kukataa shule na kufeli muda mwingine husababishwa na shule zenyewe kwa sababu shule zetu zimekua zimejaa vipigo vizito kwa watoto ambavyo tumesikia kesi kadhaa za vifo vya wanafunzi vinavyotokana na vpigo kutoka kwa waalimu na ubaya ni pale ambapo tunaangalia athari inayoonekana kwa juu ile ya mwanafunzi kufa tukiwasahau wale walioingiwa na hofu kubwa na kuacha shule baada ya mwenzao kufa kutokana na kipigo kutoka kwa mwalimu, kuna wale waliopigwa lakini hawakufa hivyo taarifa zao hazisikiki ila baada ya vitendo hivyo imefanya wachukie shule na maisha yao kiujumla, hii inaongeza maskini wengi katika jamii tena wasio na elimu na mbaya zaidi wenye matatizo ya akili pia ndoto nyingi hufa, huenda aliyeacha shule ndo angekuja kuwa kiongozi bora asiyeumiza wananchi kwa kodi zisizo na kichwa wala miguu matokeo yake hata wanaobaki shule wanakua ni wenye nidhamu ya uoga iliyopitiliza kwa walimu na hii inaathiri mpaka akili zao na kujenga taifa lenye watu wasiojiamini ndo hawa watu wazima wa leo au baadae wanaofanya mambo ambayo jamii inbaki imeduwaa.
Aina za matatizo/magonjwa ya akili
Zipo aina mbalimbali za matatizo ya akili yakihusisha hisia, wasiwasi, magonjwa yatokanayo na majanga, msongo wa mawazo na matumizi au utegemezi wa vilevi n.k
Yafuatayo ni baadhi ya matatizo ya akili;
a)Ugonjwa wa sonona (depression)
Huu ni ugonjwa wa akili ambapo mtu hujiskia huzuni ya mara kwa mara inayoambatana na mawazo au fikra hasi na tabia ya kutoweza kujumuika na wengine. Hali hii hudumu kwa wiki kadhaa, miezi hata miaka.
b)Magonjwa ya wasiwasi/tashwishi (Anxiety disorder)
Hii hutokana na hali ya wasiwasi uliozidi kupindukia au hali ya hofu inapojitokeza pasipo sababu ya msingi na kumkosesha raha mhusika.
c)Ugonjwa wa Baipola (Bipolar disorder)
Haya ni mabadiliko yasiyo ya kawaida ya hisia yanye kuathiri nguvu za mwili, tabia ya mtu na uwezo wa kutekeleza shughuli zake za kila siku. Dalili mojawapo ni furaha iliyopitiliza.
d)Ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (dementia)
Husababisha kupoteza kumbukumbu hata za mambo na
matukio muhimu ya karibuni mfano mtu mwenye ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu unaweza kumwambia jina lako sasa hivi na baada ya dakika tano akauliza tena jina lako.
e)Ugonjwa wa ukosefu wa umakini na kushindwa kutulia (Attenition deficity hyperactivity Disorder- ADHD)
Ni tatizo la kiakili linaloanzia utotoni lenye kuhusisha ukuaji wa mfumo wa fahamu ambalo husababisha kukosa umakini na kufanya vitu kwa msukumo usio wa kawaida.
f)Ugonjwa wa skizofrenia (schizophrenia)
Ni ugonjwa wa kibaiolojia unaoathiri mchakato wa mawazo ya mtu na mara nyingi uwezo wa kiutendaji. Mara nyingi hii hufanya mtu kuona, kuhisi au kusikia vitu ambavyo kiuhalisia havipo.
g)Ugonjwa wa kimawazo na tabia za kukithiri (Obsessive compulsive disorder - OCD)
Ni ugonjwa unaosababishwa mtu kupata mawazo yanayojirudiarudia na wakati mwingine kupata hali inayomsukuma kurudiarudia kutenda jambo bila hiari yake na hii humkosesha raha.
h)Usonji (Autism)
Ni ugonjwa unaoanza kuonesha dalili zake kwa mtoto anapofikisha umri wa miaka kuanzia mitatu na mtoto huwa mzito kuelewa mambo kama watoto wengine na hapendi kuchangamana na wenzake, pia hushindwa kujieleza.
i)Msongo baada ya janga (post traumatic stress disorder -PTSD)
Ni ugonjwa au tatizo linalompata mtu baada ya kupatwa na janga mfano kubakwa, vita, unyanyasaji wa kijinsia, ukatili kwa watoto na ajali za kutisha.
NINI KIFANYIKE?
Nafikiri kuna haja ya serikali kuliangalia hili suala kwa umakini zaidi, jamii ielimishwe namna bora ya malezi ya malezi ya watoto kwa kuzingatia afya ya akili na pia umuhimu wa kuwaamini wanasaikolojia katika matatizo yanayoikumba jamii lakini pia kutoa elimu kwa wanafunzi kuibukia katika tasnia hii ya wanasaikolojia yenye nguvu kazi kidogo sana kwa maana ya watu, pia kuna umuhimu wa kupima hadi akili kwa viongozi wa nchi, wafanya kazi, vijana kabla ya kuoa na kuolewa, na hata wanafunzi kabla ya kuingia shuleni/vyuoni.
Hii itasaidia sana kupunguza matukio ya kikatili, maamuzi yasiyoeleweka na kujenga jamii yenye watu timamu wenye afya ya akili ili waweze kuleta maendeleo katika nchi na hata kesi za kujiua na mauaji zitapungua pia kwakua mara nyingi akili huwa ndo chanzo cha haya yote. Pia wanaume wa kiafrika kuna haja ya kuacha kasumba ya kubaki na vitu moyoni au kufa na tai shingoni kama waswahili wasemavyo hii inaathiri mpaka akili zao na matokeo yake yanaathiri mpaka jamii nzima kiujumla.
Binafsi ni mhanga wa sonona na msongo wa mawazo unaotokana na sababu nyingi ikiwemo kutopewa sapoti au kutengwa na familia kihisia, kusemwa na kuonekana sifai kwa sababu tu sikufanya vizuri masomoni na nina ndoto tofauti na matatajio yao kama wazazi na familia na sababu nyingine nyingi na hii ilipelekea mpaka kufikiria kupoteza maisha yangu zaid ya mara moja ili nipumzike na kwa muda huo niliona hilo ndilo jibu la matatizo yangu na kuna siku niliingia mtandaoni na kutafuta namna nzuri ya kujiua bila maumivu, nahisi huenda mwenyezi Mungu alitumia njia hii kuninusurua na kitendo kile maana nilikutana na tovuti moja yenye kichwa cha habari ambacho nilikua nakitafuta lakini maudhui yake yalilenga kubadilisha mawazo ya watu kama mimi wenye malengo ya kukatisha maisha yao hivyo baada ya kusoma nakala ile kweye ile tovuti nilibadilisha mtazamo wangu na huenda bila ile leo hii nisingekuwepo kuandika makala hii hapa jamii forum natumaini ujumbe utafika panapohusika na kusaidia watu wengi zaidi hasa hapa nchini kwetu Tanzania.

Upvote
1