Asante nimekupata vizuri kabisa. Vipi unaweza kuelezea kuhusu conscious mind na subconscious mind japo hata kidogo in relation to brain?
Kwanza kabisa inabidi ujue kazi za ubongo , zimegawanyika ktk makundi makuu mawili
- Kuratibu matendo ya hiari~ambayo wewe unaamua mwenyewe kwa kujipangia mfano kutembea, kukaa, kuingia JF, Kwenda pub kunywa bia n.k
- Kuratibu matendo yasiyokuwa ya hiari~mfano mapigo ya moyo, blood pressure, kasi ya kuvuta hewa kwenye mapafu n.k
Kazi namba moja inaingiliana na counsious mind, kazi namba mbili inaingiliana na uncomscious mind, hapa kitu kinacho hitaji maelezo zaidi ni subcounscious mind
subcounscious mind
kuna mwanasayansi mmoja anaitwa PAVLOV, alikuwa na mbwa wake mmoja kila akitaka kumpa nyama yule mbwa akiona nyama tu anatokwa na mate, pavlov alikuwa anampa mbwa nyama ktk muda maalum aliokuwa ameuset, akawa kila akitaka kumpa mbwa nyama kengele inapiga kwanza ndio anampa nyama, alilifanya hilo zoezi kwa kipindi kirefu, sasa siku moja nyama hazikuwepo alichokifanya ni kupiga kengele tu bila kumpa mbwa nyama, kilichotokea mbwa baada ya kusikia sauti ya kengele alitokwa na udenda bila nyama kuwepo
Hapa tunajifunza kwamba kwenye ubongo wa mbwa kuna circuit mbili alizitengeneza, circuit ya kwanza ni ya nyama, circuit ya pili mlio wa kengele,
Kuna kitu kinaitwa CONDITUONING yaani circuit mbili zinakuwa stimulated ktk event moja mfano nyama na kengele, ubongo unahamisha taarifa za circuit mbili tofauti kwenda kwenye circuit moja, ndicho hicho kilichotokea kwa mbwa kasikia kengele tu bila nyama katokwa na mate
Mfano namba mbili kuna binti alipata ajali na wenzake kwenye gali, kabla ya ajali walikuwa wanacheka kutokana na story zao za kufurahisha, baada ya ajali, alikuja kuzinduka akiwa kitandani wodini wenzake wote walikufa, huyu binti akawa kila akisikia watu wanacheka anapatwa na mfadhaiko anaanza kulia
Hiyo ndio subcounscious mind yaani iko kati kati ya counscious na uncounscious
Hii inatumika kwenye matangazo mfano Ronaldo kuongea na wanahabari huku wameweka cocacola mezani. That is scientific manipulation marketing conditioning reflex tactic.