Akili ya binadamu

Akili ya binadamu

Baadaye kuna daktari mmoja mtaalamu wa Neuroscience alimfanyia mtu upasuaji wa ubongo ili kuondoa uvimbe, alifanya upasuaji akamaliza akamruhusu mgonjwa aende nyumbani, baada ya siku kadhaa mgonjwa akarudishwa hospitali akilalamika kuwa anapoteza kumbu kumbu hawezi kukumbuka matukio ya miaka ya nyuma na amewasahau mpaka watoto wake,

Ndipo hapo huyo daktari akanga'mua kuwa kumbu kumbu huhifadhiwa kwenye sehemu ya ubongo wa kati sehemu aliyoiondoa wakati wa upasuaji ndiyo hiyo inayohusika na kumbukumbu, baada ya ugunduzi huo wakaona kuwa akili na kumbu kumbu zote zipo kwenye ubongo ambapo ni sehemu ya mwili wa binadamu kwa hiyo wakawa wame m proof wrong bwana RENE DISCARTE na duality theory yake aliyokuwa akidai akili inapatikana nje ya mwili wa binadamu
Maarifa huwa hayaishi. Na wewe tukuongezee.

Kwenye ubongo unatengeneza brain cells. Kwahiyo ukiwaza brain cells zinaamshwa na mwili unaanza kufanya kazi.

Yaweza kuwa huyo dokta ali disturb hizo cells. Mfano mtu akipigwa stroke inakuwa brain cells zimekatwa hata ukiwaza kunyanyua mkono hakuna mawasiliano ya cell za ubongo na mwili.
 
Natumai mko poa pamoja na hizi tozo[emoji1].

Mind-body dualism hii ni dhana kwamba akili(mind) na mwili(body) wa binadamu ni vitu viwili tofauti kila kimoja kinajitegemea kivyake.Dhana hii ilikua maarufu katika karne ya 17 kutokana na mwanamahesabu wa ufaransa aitwaye René Descartes,alikua na msemo wa kilatin “Cogito, ergo sum,” kwa kiingereza ni "I think, therefore I am” kwa lugha nyepesi ntasema "You are not your mind, you are the one listening to it" yanii wewe sio akili yako wewe ni yule unaesikiliza akili inakwambia nini.

Akili(mind) inahusisha ufahamu (consciousness) hii inafanya akili igawanyike kwenye makundi makuu matatu hii dhanaria ilikuwepo kitambo lakini ilielezewa vizuri na mwanasaikolojia kutoka Austria,bwana Sigmund Freud.

Makundi ya akili ya binadamu
1.unconscious mind
2.subconscious mind na
3.conscious mind

1.UNCONSCIOUS MIND.

Akili hii imeundwa na hisia,tabia,mawazo,mihemko kwa ujumla kumbukumbu za zamani au za sasa ambazo mara nyingi huwa ni za kuogofya au za kututia aibu,hivyo tunazipotezea na tunaziweka nje ya ufahamu wetu tusiweze kuzikumbuka.

Ingawa hatujui uwepo wa kumbukumbuku hizi ila zina ushawishi mkubwa juu ya tabia zetu za kila siku,zinaweza kusababisha shida kadhaa, pamoja na
hasira,woga,tabia ya kuchaguachagua vitu(mfano chakula),mwingiliano mgumu wa kijamii na shida kwenye mahusiano.Freud aliamini kuwa wakati mwingine kumbukumbu hizi zilizofichwa hujidhihirisha kupitia ndoto na kuteleza kwa ulimi(ulimi hauna mfupa).


2. SUBCONSCIOUS MIND.

Akili hii imeundwa na kumbukumbu zote zinazohitajika kukumbukika kwa urahisi, kama tarehe ya siku yako ya kuzaliwa,inashikilia kumbukumbu tunazotumia kila siku, kama tabia na hisia.Pia hushughulika na kila kitu ambacho mwili wako unahitaji kufanya kazi vizuri, kutoka mfumo wa chakula hadi mfumo wa upumuaji hata unapokua umelala na pia ndio chanzo cha ndoto tunazoziota hata kama tukiwa tumelala na hatujitambui.

Subconscious mind mara nyingi huwa inahusishwa na imani kwani ina nguvu sana katika maisha ya binadamu, miujiza yote kama uponyaji huwa inatokea kwenye akili hii mtu anapoamini,kwasababu wazo lolote tunalopanda katika akili hii aidha baya au zuri kwa kurudiarudia siku moja litakuwa ukweli(maneno uumba) hivyo tunahitaji kuwa makini sana na mambo tunayofikiria na kuyaongea.Tukiwaza vitu hasi(negative) itatupelekea kutokuwa na furaha,afya bora na kutofaulu katika maisha yetu pia tukiwaza vitu chanya (positive) tutapata furaha,afya bora na utafanikiwa kwenye maisha yetu.

Kwa kuchukua udhibiti wa akili hii, tunaweza kuwa na uhakika wa kudhibiti tena maisha yetu na kufanikisha chochote tunachotaka. Hii ni kwa sababu wakati subconscious mind, conscious mind na mwili(body) zinapofanya kazi pamoja ili kufikia lengo moja, tunaweza kuamini kwamba lengo hilo litafanikiwa kivyovyote. Meditation ni njia rahisi zaidi inayoweza kutuunganisha na akili hii.


3. CONSCIOUS MIND.

Akili hii inahusisha vitu tunavyotambua na ambavyo tunavifikiria hivi sasa kwa mfano, unavyousoma huu uzi, sauti ya muziki unaosikiliza na kufanya mazungumzo.

Akiili hii ndio mlango wa taarifa kwa njia ya picha au sauti kutoka kwenye mazingira ya nje yanayomzunguka binadamu na kuzihifadhi kwenye akili nyingine za binadamu,pia ni kupitia akili hii ndio tunaweza kufikia subconscious mind na kuficha na kufukia kumbukumbu nyingine kwenye unconscious mind.




Fisherman.
Good presentation kwa karne ya 17 huu utafiti ulikuwa juu sana japo kwa uchunguzi na ugunduzi zaidi na vifaa vya kisasa zaidi mambo mengi yamewekwa wazi ikiwa ni mwendelezo wa hayo ya karne ya 17

Mungu ni fundi na anatupenda sana kushinda tunavyojipenda.

Ila kuna wapuuzi wametengeneza mfumo wa elimu kuharibu akili na ubongo wa watoto wetu. Shame on them
 
Back
Top Bottom