Akili ya Dr. Shika sio ya nchi hii, hivi unajua majina yake halisi?

Akili ya Dr. Shika sio ya nchi hii, hivi unajua majina yake halisi?

Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha,
Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja (Elibariki Dishon) anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotel ya Sputnik
Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi uku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Africa, na amekuwa akitaftwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi,

mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko uko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo,

Shirika la Lancerfort limekuwa likimilika asset kubwa nchini urusi na kwingineko duniani wakati chanzo cha hela yao hakijulikani, hivyo moja kwa moja kuhisiwa ni miongoni mwa mashirika ma spy ambao wafadhiri wake ni wamarekani ambao wana uhasama wa mda mrefu na urusi,

wametelekeza mali nyingi kukiwemo na priovate jets na maghari ya thamani,

Kupitia wapelelezi wa ndani ya urusi ambao walilichunguza shirika ambalo inasemekana rais wake ni Dr Luis Shika kwa kipindi kile, waligundua mawasiliano ya karibu na baadhi ya mashirika yafuatayo AMNESTY INTERNATIONAL, CIA, FBI , HGRE, OKLE, ambayo mara nyingi huwa ni waanzilishi wa upelelezi katija nchi nyingi,

Baada ya kugundua hayo walitekwa na kuwekwa mateka na wawili kuuwawa , mmoja wapo akiwa mkenya Edward Koinange na mwingine wa siera leone Yunusu AKhbu, Na wawili kukimbilia Tanzania lakin rais wao akapelekwa hospitali baada ya kuwatoroka akiwa ameumizwa vibaya, hakutibiwa urusi alitoroshwa kinyemela mpaka mjini Dnipro Ukraine, na kutoroshewa Tanzania,
Baada ya kufika Tanzania hakuenda moja kwa moja kwao akajificha mjini Dar es salaam, (Haya ni maelezo kwa mujibu wa mtu wake wa karibu)
Baadae kutorokea Uhispania Mjini Malaga , amekaa malaga miez 8 Na kurudi Tanzania,

Mwaka 2012 wakaidhinisha malipo kutoka marekani ambayo bado yapo kwenye mlolongo wa
kukamilisha mchakato.
Malizia hii kitu imeniweka serious kuisoma
 
Dr Louis Shika ni mtu makini anayejielewa sana ila kwa wale waliokuwa wanakimbilia kujibu maswali ya kuchagua shuleni watamuona kama kichaa.. ni mtu mwenye utimamu wa kipekee angalia anavyojibu Maswali kwa umakini kabisa... huyu jamaa nimegundua anaakili nyingi sana kuliko 95 %ya watanzania ndio maana wengi hawamuelewi na hawa waandishi wetu wenye D mbili hawamuulizi maswali ya maana..
 
Love you Dr. Shika! Super IQ man, ordinary IQ inasumbuka kikujua hawawez kukuelewa. This man is another level, sema akili zikizid jamaa inakususa kwa sabab unawaza vile ambavyo asilimia kubwa haiviwazi wala kuviona
You are right,akili yake iko juu sana hata ukimsikiliza anavyoongea,yuko kwenye level ya juu sana ya uelewa...
 
Lancefort Ltd ni kampuni iliyosajiliwa nchini Russia miaka kadhaa iliyopita, na kwasasa haifanyi kazi kwa kipindi kirefu baada ya watendaji wake kupotea gafla kwa mazingira ya kutatanisha,
Kutoka mjini Rostov on don napokaa mpaka Moscow ni mwendo mrefu kidogo ambao ni km 1200 na zaidi, kwa mwendo wa trein ni 5hrs,
nimefika mjini moscow na kuanza kuuliza hasa legality ya kampuni hiyo ndani ya moscow na Urusi kwa ujumla, nimefanikiwa kupata maelekezo ya kukutana na Mtanzania mmoja (Elibariki Dishon) anaisha mtaa wa Tverskaya Street, ambaye kanikaribisha na kuanza kufanya uchunguzi wangu, nikaamua kwanza nipate hifadhi ndani ya hotel ya Sputnik
Baada ya kwenda kwa watanzania wanaoishi uku nimegundua huyu mzee alipata matatizo kwa kuhisiwa ni spy wa marekani, ambaye kapandikizwa kutokea Africa, na amekuwa akitaftwa na kufuatiliwa nyendo zake zote kuanzia kwenye kampuni yake na nyumbani alipokuwa anaishi,

mke wake bi Luisa Kvonkov ndo alibanwa na kueleza kwao ni Tanzania Magu, Lakini inasemekana kwamba kuna kampuni kubwa la kimarekani aidha shirika la upelelezi ambalo liko nyuma ya kampuni ya Lancefort, ndio chanzo cha kutiwa msuko suko uko alikokuwa anamiliki kampuni hiyo,

Shirika la Lancerfort limekuwa likimilika asset kubwa nchini urusi na kwingineko duniani wakati chanzo cha hela yao hakijulikani, hivyo moja kwa moja kuhisiwa ni miongoni mwa mashirika ma spy ambao wafadhiri wake ni wamarekani ambao wana uhasama wa mda mrefu na urusi,

wametelekeza mali nyingi kukiwemo na priovate jets na maghari ya thamani,

Kupitia wapelelezi wa ndani ya urusi ambao walilichunguza shirika ambalo inasemekana rais wake ni Dr Luis Shika kwa kipindi kile, waligundua mawasiliano ya karibu na baadhi ya mashirika yafuatayo AMNESTY INTERNATIONAL, CIA, FBI , HGRE, OKLE, ambayo mara nyingi huwa ni waanzilishi wa upelelezi katija nchi nyingi,

Baada ya kugundua hayo walitekwa na kuwekwa mateka na wawili kuuwawa , mmoja wapo akiwa mkenya Edward Koinange na mwingine wa siera leone Yunusu AKhbu, Na wawili kukimbilia Tanzania lakin rais wao akapelekwa hospitali baada ya kuwatoroka akiwa ameumizwa vibaya, hakutibiwa urusi alitoroshwa kinyemela mpaka mjini Dnipro Ukraine, na kutoroshewa Tanzania,
Baada ya kufika Tanzania hakuenda moja kwa moja kwao akajificha mjini Dar es salaam, (Haya ni maelezo kwa mujibu wa mtu wake wa karibu)
Baadae kutorokea Uhispania Mjini Malaga , amekaa malaga miez 8 Na kurudi Tanzania,

Mwaka 2012 wakaidhinisha malipo kutoka marekani ambayo bado yapo kwenye mlolongo wa
kukamilisha mchakato.
Isije ikawa wewe ndo "dokteri shikwa menyewe".najisemesha kimoyo na kama sio wewe basi n mwngne amekuja tyu humu ili na sisi tuokoke kupitia yeye.
 
Inasemekana Warusi walikuwa wakimgwaya sana Dr. Shika kwa ugenius wake na akili yake iliyokuwa na uwezo mkubwa (si bure kuna kitu walimfanyia). Dr. Shika kwa manufaa anayoyajua yeye, inaonekana pia alibadili majina yake kam ifuatavyo:

Lunyalula - Louis (Ukitamka kwa Kizungu au Kirusi cha ndani kabisa, Lunyalula ni almost Louis)

Kidola - Kid

Shika - Kaicha kama ilivyo.

Mimi nadhani kutokana na akili yake kubwa na kwa sababu Warusi ni watu wabaya sana wakikuona una akili, aliamua kujinasibisha na koo za kirusi kwa kubadilisha majina angani ili awe salama. Hata hivyo inaonekana kuna fitna walimfanyia.

Dr. Shika na Msomi Morris Sankuu ingekuwa ni hazina kubwa sana kwa Taifa hili.

NB: Dr. Shika hashikiki, kuna jamaa kaeleza kuwa akienda dukani kwake, anacheki halafu anamwagiza bidhaa ambayo haipo dukani.

Cheki hapa:

Ila sikupenda jinsi huyu polisi alivyomsema vibaya:

*R.I.P DR. SHIKA😭*

Dr.Shika alikuwa ni miongoni mwa wasomi wazuri lakini bahati mbaya elimu yake haijaweza kusaidia taifa hili achilia mbali kumsaidia yeye binafsi.

Wengi walimchukulia kimzaha tangu alipoonekana kwenye tukio la mnada wa nyumba za Lugumi (mia tisa itapendeza). Makampuni ya kibiashara yalitumia umaarufu wake kama fursa ya matangazo lakini yakamuacha hohehahe asiye hata na mahali rasmi pa kuishi. Aliwahi kuripotiwa na kituo kimoja cha TV kufukuzwa kwenye nyumba aliyokua akiishi huko Tabata baada ya kushindwa kulipia kodi.

Vyombo vingi vya habari vilikuwa vikimdhihaki na vingine kumuita Kalubandika. Lakini bila shaka vilifanya hivyo pasipo kumjua kiundani *Dr.Shika.*

Ni mzaliwa wa kijiji cha Kalemela wilaya ya Busega, mkoani Simiyu. Majina yake halisi ni Louis Shika Kidola. Yeye na ndugu yake Jeremiah Shika Kidola *(marehemu pia)* walikuwa wanafunzi wenye akili sana na waliofaulu vizuri masomo yao ya sekondari kwa alama za juu na kupata ufadhili wa kusoma udaktari nchini Urusi mwaka 1984 hadi 1991 waliporejea na kuanza kutibu hospitali ya taifa Muhimbili.

Mwaka 1994 Louis Shika alirejea Urusi kujiendeleza kimasomo. Alisomea shahada ya uzamili katika magonjwa ya kuambukiza (MSc in Infectious Diseases) na udaktari bingwa wa magonjwa ya akili Master of Medicine (Psychiatry). Akiwa huko alishirikiana na wenzake kuanzisha kampuni ya usambazaji wa kemikali viwandani iitwayo Lancefort Ltd.

Kwa sasa ni moja ya makampuni makubwa ya usambazaji wa kemikali nchini Urusi, na jina la Dr.Shika lipo kwenye website yao kama Muasisi na Rais wa kwanza wa kampuni.

Inadaiwa shirika la ujasusi la Urusi (KGB) liligundua kwamba akina Shika walipata fedha za kuanzisha kampuni kutoka Marekani kama mkakati wa Marekani kudukua taarifa za Urusi. Kwahiyo baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo walikamatwa. Dr.Shika alitekwa na watu waliodhaniwa kuwa majambazi kupewa mateso makali sana ikiwemo kukatwa vidole.

Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Urusi, Patrick Chokala mwaka 2017 alinukuliwa na vyombo vya habari kwamba ilibidi kutumia mbinu za "kijasusi" kumnasua Dr.Shika na kumrudisha nchini kwa dharura. Tangu aliporejea alijiingiza kwenye ulevi wa kupindukia kutokana na msongo wa mawazo.

Kwahiyo ukifuatilia historia ya *Marehemu Dr.Shika* utagundua hakuwa "kalubandika" kama ilivyodhaniwa. Ni mtu aliyekua na maono makubwa. Kama si mipango yake kuvurugika huenda angekuwa daktari bingwa na mfanyabiashara mkubwa wa kemikali duniani.

Ni kwamba tu alijikwaa, akadondoka na hakuweza kusimama tena. Serikali ilipaswa kumsaidia kusimama lakini nayo ilimtelekeza. Kwahiyo ameishi maisha ya upweke, masononeko na msongo wa mawazo kwa muda mrefu.

Kampuni aliyoanzisha ya Lancefort Ltd ambayo kwa sasa inamilikiwa na serikali ya Urusi (ilitaifishwa) ina thamani ya $27Bil sawa na TZS 60Trilioni (Bajeti ya nchi kwa miaka miwili).
_
Kwa hiyo Dr.Shika alikuwa anajiita "Bilionea" si kwamba alikuwa anaota. He used to have money. Na hiki ndicho kilichokuwa kinamtesa maana alishindwa kukubaliana na hali yake ya sasa. Hakutaka kuamini kama aliwahi kuwa na pesa.

Kujikwaa na kuanguka ni kawaida katika maisha lakini jambo la msingi ni uwezo wa kusimama tena baada ya kuanguka. Whinston Churchil aliwahi kusema "Success is not final and failure is not fatal. It is the courage to continue that counts"
_
Mtu kama huyo hakuwa mtu wa "kumchukulia poa" hata kidogo. Serikali haikutakiwa kumtelekeza. Alipaswa kupewa nafasi nyingine. Either angerudishwa Muhimbili kutibu au angetafutiwa fursa mahali pengine ambapo taifa lingeweza kufaidi ujuzi wake na pia ingekua njia ya kumsaidia kuondokana na msongo wa mawazo na kusahau "mabilioni" yake kule Urusi.

*Pumzika kwa amani Mr. mia tisa itapendeza*

C&P from WhatsApp group.

RIP Dr. Louis Shika.

P
 
Back
Top Bottom