Badrin Elisha Nchimbi
New Member
- Jul 2, 2023
- 2
- 1
Akili ya mwanadamu
Kuna nadharia mbalimbali zinazotoa tafsiri ya akili. Leo nitazungumzia tafsiri ya akili kwa muktadha wa kitheolojia. Akili ni nini? Akili ni uwezo wa ki Mungu ambao umewekwa ndani ya mwanadamu, inatafsiriwa kama kitendea kazi cha mwanadamu. Mungu alipomuumba mtu alimuumba kwa mfano na sura yake, kwa maana ya kwamba, alimpa uwezo wa kupambanua mambo (utashi). Mtu ni mjumuisho wa mwili, nafasi, na roho. Akili imewekwa ndani ya nafasi. Kama ilivyo kwa mwili na roho zina mahitaji yake, pia akili ina mahitaji yake. Mfano, mahitaji ya mwili ni chakula, maji, hewa safi, mazoezi, kupumzika, na tendo la ndoa kwa wanandoa. Pia, roho inahitaji ibada, kuabudu, nk.
Turudi kwenye akili; akili inashibishwa na maarifa/elimu. Akili inahitaji taarifa za kutosha ili uweze kufanya maamuzi sahihi katika maisha yako, kama akili haitakuwa na taarifa za kutosha utaamua na kuishi katika viwango vya chini. Usipokuwa na maarifa katika jambo fulani, utakuwa mjinga katika hilo eneo. Mazingira yanaweza yakakubadilisha na kuwa mtu mwingine tofauti na ilivyokusudiwa kuwa, kwa sababu mazingira yanazungumza, mazingira yanabadilisha, mazingira yana nguvu. Ukitoka sehemu moja kwenda nyingine kikazi, lazima utafute taarifa za eneo hilo unaloenda ili uyajue mazingira yake ili uweze kuyaishi vizuri, vinginevyo mazingira yatakubadilisha.
Afya ya akili mara nyingi inatokana na mazingira, malezi, na makazi kuanzia umri wa miaka 0-11. "Akili ni uwezo wa kiMungu uliomo ndani ya mwanadamu", hapa ni lazima upate maarifa, elimu, na taarifa sahihi ili akili yako iweze kuchanganua mambo kwa usahihi. Hapa unarudi kwenye kusudi la wewe kuwepo duniani. Mfano, katika Taifa la Israeli wana mtaala wao unaoitwa "Pentateuch". Huu mtaala unafundishwa kwenye shule za msingi na wameelekeza taarifa sahihi kupitia vitabu vitano kwa Musa ambavyo ni Mwanzo, Kutoka, Hesabu, Mambo ya Walawi, na Kumbukumbu la Torati.
Kwa tafsiri yao, hivi vitabu vitano ni taarifa sahihi ya kuwafundisha watu wao, kwa sababu imeelezea historia ya taifa lao, mababu zao, imani yao, na sheria zao. Hii ndio msingi wao wa akili. Je, sisi Tanzania msingi wa taarifa zetu sahihi ni nini? Kwa maoni yangu, kama taifa turudishe nguvu ya uwekezaji kwa watoto kwa kuwapatia maarifa sahihi, taarifa sahihi, na malezi sahihi. Mfano, kwa sasa mitaala yetu inafundisha mtu alitokana na nyani, binafsi naona hii si taarifa wala maarifa sahihi ya kuwekeza kwa watoto. Haya maarifa yanamfanya mtoto aanze kujiona yeye ni duni.
Madhara ya kutopata taarifa sahihi kwa ajili ya kuilisha akili ni kupata jamii isiyostarabika, viongozi watapatikana wenye maamuzi mabovu, uwezo mfogo wa kuchanganua mambo, na udumavu wa akili yenyewe. Kwenye makusanyiko ya dini watu wapatiwe taarifa sahihi kwa maana ya mafundisho, maana huko nako kuna tatizo kubwa "watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa". Vyombo vya maamuzi wapewe elimu iliyo sahihi, na kila taasisi na jumuiya ya watu taarifa sahihi kwenye akili zinahitajika ili tuwe na jamii iliyo bora itakayoleta ustawi kwa taifa.
By Mch. B. E. Nchimbi

Upvote
1