Kurunzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2009
- 9,753
- 10,747
LEO asubuhi ndio nimegundua kuwa ile Yanga ya Nasreddine Nabi ilikuwa hatari ndani ya Uwanja,Yanga ya Gamondi pia ni hatari lakini hii Yanga chini ya ENG HERSI SAID ni hatari zaidi ndani na nje ya Uwanja.
AKILI za Eng Hersi na pesa za GSM inaonesha inaweza kwenda kujitengenezea ufalme wa mda mrefu ndani ya Tanzania kama wengine hawatashtuka mapema na ikafanya makubwa nje ya Tanzania ambayo yataiduwaza Afrika.
NILIKUWA namsikiliza George JOB akizungumzia sababu alizoambiwa na Bwana Hersi juu ya kuachwa kwa wachezaji wawili,Djuma Shaban na Yanick Bangala akisema ni sababu ya mipango yake (Hersi Said) kuhusu Msimu wa 2024/25.Yaani hawajaachwa kwa sababu ya Msimu huu,no bali Msimu ujao.
WAKATI watu wengi wakishangaa kwanini Wachezaji hao ambao walikuwa wakiamini wangeisaidia Yanga Msimu huu,yeye alikuwa amewaza mbele zaidi ya msimu huu.Aliwaza na kufanya maamuzi hayo tangu mwezi Januari.
ENG HERSI aliamini huenda nyota hao wangeweza kuendelea na Yanga msimu huu ila wasingeonesha kiwango bora kama kile walichoonesha msimu wa 2021/22.Nini cha kufanya? Ni kuandaa Kikosi kingine wakati bado mastaa wengi waliopo wapo kwenye ubora.
KIPINDI ambacho viongozi wa timu zingine wakiwaza juu ya msimu huu,yeye tayari anachora ramani ya namna ya kuwa na timu bora kwa misimu miwili mbele zaidi. Alijua wazi kwa kikosi walichonacho,uwezo wa kufanya vyema msimu huu wangekuwa nao ila ni vipi baada ya msimu huu kuisha?
NADHANI viongozi wa timu zingine wanapaswa kuchangamsha akili zao maradufu ili waweze kushindana na Yanga nje na ndani ya uwanja na hata kuizidi akili ya Eng Hersi iliyochanganyikana na Pesa za GSM.
INAONYESHA kwamba hata msimu ujao huenda wakaendelea kuwa bora zaidi kwa namna wanavyozipangilia strategies zao. Wasipoamka mapema basi tusubiri kuwaona Wananchi wakiendelea kutamba tu.
Cc: C&P
#SisiNiMashahidiTu
#hallaywsmm🇹🇿