Uchaguzi 2020 Akili za kukariri na kuhariri katika siasa za Tanzania

Uchaguzi 2020 Akili za kukariri na kuhariri katika siasa za Tanzania

DITOPILE WAPILI

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2015
Posts
384
Reaction score
261
Matokeo ya Uchaguzi wa Tanzania yameanza kutoka tangu tarehe 29/10/2020 na Chama cha CCM kwa asimilia kubwa kinadalili ya kushinda ushindi wa kishindo.

Vyama vya upinzani wakiwa wanabeza na kukariri kwamba CCM imepata ushindi kwa kuiba kura, kuendelea kukariri hivi ni makosa makubwa sana pia kunaweza kusilete majibu chanya ya ustawi wa vyama vya siasa hasa upinzani.

Vyama vya Siasa wanapaswa kuhariri kwanini? wanashidwa uchaguzi hii itawasaidia sana kupata wigo mpana kujenga vyama vyao na kujua shida ipo wapi?

Uchaguzi wa mwaka 2015 CCM ilipitia changamoto na upinzani mkali sana mpaka kupoteza majimbo mengi waliokuwa wanatawala, lakini baada ya uchaguzi 2015 CCM ilikubali kujifanyia tasmini, kujikosoa, kufanyia kazi mapungufu yao wakilenga kukijenga chama chao na kubomoa upinzani wao,

Faida ya kujenga upya CCM, Tuliona baadhi ya viongozi wa upinzani wakitoka kwenye vyama vyao na kuingia chama CCM, Pia kipindi cha janga la korona viongozi upinzani kwa kiasi kikubwa walipishana falsafa na mitazamo kuhusu ugonjwa huu, upinzani waligawanyika tena wengine walibaki na wengine waliondoka.

Viongozi wa upinzani waliobaki kwenye vyama vya upinzani hawakuwa wamoja kama walivyokuwa kwenye uchaguzi wa 2015, pia hawkukaa pamoja kumaliza tofauti zao, ili ni dosari kubwa sana kwa vyama vya upinzani.

Nina imani wapizani wakifanyia kazi mapungufu yao na kujua wapi walipokosea kwenye uchaguzi huu wa mwaka 2020, itawasaidia sana kujenga upinzani imara katika uchaguzi wa 2025. Lakini wakikubali kuimba wimbo wa kuibiwa kura, ni kujitokomeza kabisa.

Tabia ya kukimbilia kulaumu watu juu ya matatizo yao wenyewe, kupenda kutafuta njia rahisi na ya mkato tunapotaka kutatua changamoto zetu, ni kukwepa kuwajibika pale tunapokosea. MUDA BADO UPO UPINZANI KUJIPANGA na kufanya vizuri.

Mwisho wa uchaguzi huu ni mwanzo wa uchaguzi 2025.
 
Back
Top Bottom