Akilia sana, karibu kutunguliwa...!

Ndege aliye mtini, hawezi kamwe kulia,
Labda aliye shimoni, hewa imempelea.
Hivi ni sababu gani, machozi hawezi toa?
Ndege aliye mtini, kamwe hawezi kulia.

we babu we kiboko kila fani umo? nimekuvulia kofia, bora wewe sasa teamo ndio sikudhani kabisaaaaa kumbe watu wana vipaji humu lol
 

Naomba MMM, Teamo, Asprin na AmanGK muwe mnakuja namna hii kila inapowezekana maana wanasema ukicheka waongeza siku. Ilikuwa full kucheka

You guys are GREAT!!!
 
Wazushi waniwangia, ndege kunifukuzia,
Hakika nawaambia, wangu namng'ang'ania,
Kamwe hawatopatia, watabaki angalia,
Ndege amekwishalia, mwajua kitofatia!
Kutunguliwa.

MMM
 
Wazushi waniwangia, ndege kunifukuzia,
Hakika nawaambia, wangu namng'ang'ania,
Kamwe hawatopatia, watabaki angalia,
Ndege amekwishalia, mwajua kitofatia!
Kutunguliwa.

MMM
Asante Mzee kwa vitu adimu hivi!
 
huku kwetu uswahilini, hata ndege hakuna
tumezungukwa na nyani, na ngedere wengi sana
tena tupo hatarini , kifo lini? tunaulizana
ndege alie mtini , ni ndoto kwetu kuona.

udenda umenitoka, kusoma hili shairi
ndege wa kusadikika, moyoni ameshamiri
mengi nimelazimika, akilini kufikiri
lini mimi nitamshika, nipate nijivinjari.

mnasema analia, natamani lake chozi
wengine wamebishia, kulia katu hawezi
vyovyote itavyokuaa, kuvumilia siwezi
kuhama nimeamua, naenda hamia mbezi
ndege nipate tungua, kwa manjonjo na mapozi.




ni mimi malenga wenu klorokwini a.k.a mshamba mstaarabu
 
Kumtungua hutomfaidi, kibudu si fanani
Polepole mnyatie, Koo usimkabe
Poke kwa staha
Polepole mnyakue, ndani kwako muweke
Potepote Kwa makini mchunguze, afaa kuliwa?
Ni popo masikini si ndege si mnyama
Si wa kufuga, si wa kitoweo, ni dege lisiloliwa!!!!!
 

Naona hili shairi wapewe TBC liimbwe kabla ya taarifa ya habari safi sana Mzee Mwanakijiji.
 
Wazushi waniwangia, ndege kunifukuzia,
Hakika nawaambia, wangu namng'ang'ania,
Kamwe hawatopatia, watabaki angalia,
Ndege amekwishalia, mwajua kitofatia!
Kutunguliwa.

MMM

Hapa hakuna mzushi, ukweli twakuambia,
Tatizo lako mbishi, jambo ukilishikia,
Domo unafuka moshi, hoja kiishikilia,
Achana wako ubishi, ndege halii aimba.
 

Ewe kidonge mwenzangu, kumbe nawe uko ndani,
Napata kizunguzungu, umenigusa moyoni,
Ndege wa kwenu kimbungu, leo wamkataani?
Ndege huyu ndege wetu, kila shemu huishi

Labda kama baharini, kusipokuwa na miti,
Huko hakuwezekani, asijepata mititi,
Hamia kwetu nyumbani, nitakupatia hati,
Nitakupatia hati, ndege umuweke ndani.
 

pia mimi sikudhani, uwanja huu ni wako
na sasa nimeamini, hii pia fani yako
aspirini, klorokwini, hii dozi ni kiboko
mwanakijiji haamini, tunavyotoa milipuko.

huyo ndege unaesema, tayari nimemuona,
mwili umenitetema , leo nimeita jana
kumpata ni lazima , iwe usiku au mchana
nitamla mzima mzima, tena kwa kumtafuna.

naipanga mikakati, na mitego ya kileo
naitengeza manati, gobole pia koleo
nitamtungulia kati, apapatike na kilio
nikamle kwa chapati, nimfanye kitoweo
 

Siko kifani zaidi,ni hoja kuhusu ndege,
Ninayo yangu miadi,kama alivyo moringe,
Wengi wao makuwadi,kutaka wote waige,
Kama hoja ni ya ndege, mie nachagua bata,

Bata ndo namchagua, ndiyo wangu modeli,
Bila ya kuchakachua,kwa utulivu ni kweli,
Pakata ukidadua, pachika kwa baisikeli,
Kama hoja ni ndege, mie nachagua bata,

Mandege yako mengi, bundi njiwa kunguru,
Sijui wewe kitegi, ulimpata maguru,
Tumia hata ulegi,usije pata udhuru,
Kama hoja ni ndege,mie nachagua bata,

Utatungua wangapi,katika miti mingapi,
Usije pata makapi,kwa kuzani ni kopi,
Hoja yako ndio ipi,nipe nikupe tipi,
Kama hoja ni ndege, mie nachagua bata,

Pakata kwa raha zako, baada ya kumuoka,
Manati kitu ni chako,ya nini kukukuruka,
Huitaji mulengo wako,usije pata sumbuka,
Kama hoja ni ndege,mie nachagua bata,

Ni wewe mwanakijiji,ulezoea porini,
Kwetu yapo majiji, hewala i kibindoni,
Nenda mpaka ujiji,bata mpaka sebureni,
Kama hoja ni ndege,mie nachagua bata,

Ngoja niweke koma,bata wangu nimpakate,
Asije pata ukoma,kisha nimpe mate,
Nisije mwaga tama,kuku waule wote,
Kama hoja ni ndege,mie nachagua bata,
 
duh! Imetulia mbayaaa

sawa imetulia! Lakini maudhui ya washairi hawa umeyapata? Isije ikawa tunashabikia ladha ya maneno halafu ujumbe hauingii akilini!! So watch out wana jf.
 
Nilikuwa ninawaza, kalamu nisiishike,
Nikae kwenye baraza, moja mbili nisishike,
Maguluma kanikwaza, ngoja mic niishike
Bata anapakatwaje, nawauliza malenga?

Ndio hapa mnambie, kwa nini wampakata?
Tena nidadavulie, ni raha gani wapata?
Ili nami nikimbie, nimsake huyo bata,
Nawauliza malenga, bata anapakatwaje?

Hommie wangu 'Sipirini, hata nawe Klorokwini,
Mwanakijiji Amani, Magulumangu mwiteni,
Aje hapa barazani, aujibu mtihani,
Bata anapakatwaje, nawauliza malenga?

'Mesikia nimeona, bata yake kuharisha,
Wala sio kunong'ona, hilo usije kubisha
Kumpakata mi naona, hilo jambo la kutisha,
Bata anapakatwaje, nawauliza malenga?

Domo lake lachokoa, vinyesi na konokono,
Alacho ndio atoa, kwani nimpe mkono?
Usije kunizodoa, haya yangu ni maono,
Bata anapakatwaje, nawauliza malenga?

Na Kaizer K. Kaizer (Sauti ya watu)
 

Pope at his best,,kumbe ndo maana ulikuwa huji mlimani!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…