Akilia sana, karibu kutunguliwa...!


huyo ndo TEAMO sasa....
 
Kwani ana rangi gani, hebu nijuzeni
Yupo yule wa kijani, anaringa mtini
kwa madaha anaghani, tena kama hayawani
Pretta nitoe gizani, kama umeme wa dowani
 

umenena kaizeri , nadhani hukukosea
hata namimi nakiri, bata hana mazoea
ni mchafu sio siri, tena sio maridhia
kunataka ujasiri , kumpakata sawia

tokea tangu na tangu, bata hulazwa bandani
iweje magulumangu, amuweke mapajani?
naona kizunguzungu, jibu sipati jamani
naapa haki ya mungu, sitojaribu maishani

bata akiwa sokoni , kwa nje anavutia
kama hukuwa makini, waweza kumrukia
mpeleke kwako uwani, hapo utajionea
atakushusha thamani, nyumba ataichafua

chakula alacho bata, pia ni cha kuzingatia
humeza anachopata, usaha hata mafua
iweje kumpakata , hamuogopi churua?
wengi walompakata, hivi sasa waugua.


kalamu naiangusha, nafasi ninaitoa
kama unaweza bisha, shairi nilolitoa
wamalenga mnatisha, kijasho mnanitoa
bata mwampakatisha, kinyume na mazowea


na klorokwini a.k.a malenga bubu.
 


huyo ndo klorokwini sasa....,malenga bubu lakini hapo naona umesema! hahaha so entertaining!
 
mwanakijiji hivi ni wewe hua unaandika makala katika gazeti fulani hapa nchini?
 

Klorokwini ndugu yangu, nakupa zangu hongera,
Kumpata ndege wangu, hukuwa nazo papara,
Usimle wanguwangu, usijepata kuhara,
Ndege huyu ndege wangu, ni ndege aso hiyana

Ndege huyu aimbaye, siyo siyo kama anolia,
Kwa upole amwindaye, mtini atatulia,
Kwa papara afanyaye, ndege wangu takimbia,
Ndege huyu ndege wangu, ni ndege aso hiyana.
 

Homi wangu homu boi, Ndege gani wasemea?
Ndege mtini hakai, bata huyo wasemea,
Bata hakika hafai, mtini hawezi kaa,
Ndege mkaa mtini, ndio hoja simamia.

Bata zake ni bandani, nchi kavu mwakemwake,
Jifarakua majini, uchafu ni ndugu yake,
Akienda msalani, uharo ni fani yake,
Kumkumbatia bata, Ni fani ya wachafuzi.
 
Akijelengesha tungua

Ndege ajilengeshe, nasema usimtungue,
Raha ya ndege abishe, umsake akimbie,
Kimtego utegeshe, ndaniye aingie,
Heri ndege asumbue, nami nijibidishe.

Akijilengesha, chukua

Ndege ajilengeshe, kibudu usichukue,
Kwa nini ajileweshe, ni wa mdondo ujue,
Ndege raha kasheshe, kwata akuchezee,
Heri ndege asumbue, nami nijibidishe,

Akijilengesha pasua

Ndege ajilengeshe, si vema umpasue,
Ndege raha msemeshe, nyimboze zikuingie,
Hata chambo umlishe, ulimbo umnasie,
Heri ndege asumbue, nami nijibidishe,

Akijilengesha, kamua

Ndege ajilengeshe, kataa usikamue,
Ni usaha umuoshe, angani umuachie,
Nakuonya usibishe, ni kwani ndege asinzie?
Heri ndege asumbue, nami nijibidishe,

Akijilengesha nyanyua!

Ndege ajilengeshe, uvundo usinyanyue,
Mbali msafirishe, na huko akaozee,
Mke usimjulishe, itabidi azomee,
Heri ndege asumbue, nami nijibidishe,

Akijilengesha tumbua!

Ndege ajilengeshe, rafiki usitumbue,
Kaditama na yaishe, ndege raha asumbue,
Mpinzani na abishe, vya mdondo atumbue,
Heri ndege asumbue, nami nijibidishe,
 
Mhhhhhhhhhh imekaaa njema sana
 
Daah.. nyie jamaa wabaya sana! Hongereni sana kwa kuonesha wenu weledi kwenye tasnia ya ushairi.Ntarudi nimjibu Kaizer na maswali yake kwa Al-Batat.
 
Aspirini aksante, kutuliza yangu hofu
Bado kidogo nidate, nikupe wangu mnofu
Kiuno litaka nikate, vina vilonitia upofu
Mh kweli u malenga mzuri Asprini

Mwanakijiji kumbuka, ndege makazi yake mtini
mwindaji yake hulka, kumtibua usingizi
Ukicheza ataruka, kutafuta jema zizi
Kwanini kumtioungua, ngemuacha singelia
 
Shukurani za dhati ziwaendee MMM, Teamo, AmaniGK, Klorokwini na Asprin, haki ya nani nimedownload thread nzima kwa kumbukumbu zangu binafsi!

Once again wapwaz na mabinamz mmeprove kuwa JF ni KISIMA KIREFU kilichojaa Hekima!

Asanteni sana na endeleeni kutufunza!
 
huyu ndege atakuwa kunguru wa zenji.
akijilengesha chakachuwa pwaaaa!!!!!!:A S kiss:
 
hahahahahaa unampandia unamchukua eee???
du humu leo kuna mambo nimependa sana
 
huku kwetu beach labda mapapa na manyangumi
 

moja mbili nimerudi , hapa tena uwanjani
ewe jibaba la wodi , ya wazazi, aspirini
nimeanza kumfaidi, ndege alie mtini
kurejea sina budi , kuwapeni shukurani.

ndege niliempata, hakuwa tawi la chini
tamaa sikuikata , moyoni nilijiamini
mitego nikatafuta,nikaiweka begani
polepole sikusita , nikaingia kazini.

sikutumia manati, nilihofia madhara
nilikitega kijiti , akaja bila papara
alishuka kwenye mti, akaishiwa na sera
sasa nimemdhibiti , hakuna wa kunikera

rangi yake ni smati, weusi wa kahawia
ana doa kati kati , jekundu linavutia
na tena kila wakati, huwa ananiimbia
nimeshaandika hati,hakuna wa kuniibia.

nilimshika mkia , sauti akalegeza
pumzi zikanishia, ghafula nikateleza
macho ya kusinzia, hakika kanimaliza
ndege huyu maridhia, amejaa miujiza

simalizi sifa zake , musije mukaniloga
nyembamba sauti yake, akiimba hana woga
ni kijani kope zake , anang'ara bila kukoga
ni njema tabia zake, hapendi kula mizoga.

kwasasa natua hapa, nimefika kituoni
inanibidi kusepa , nirejee nyumbani
ni wakati wa kumpa, chakula ndege tunduni
kazi kwenu vidampa, mlofeli mawindoni.
 

Mjukuu orijino, Sante kunifagilia,
Nitanenepa unono, kwa sifa ulonigea,
babu kwa hayo maneno, bichwa limejivimbia,
Ahsante kwa ufagio, Babu raha nasikia.
 

Ndugu yangu klorokwini, ndege ulojipatia,
Usimtupe shimoni, ndege asije kulia,
Ahsante kwa shukurani, sisi ni ndugu sawia,
Ila usije sahau, zuri kula na nduguyo.

Ndege huyo maridadi, kama ulivomsifu,
Asipigwe na baridi, wala kung'atwa siafu,
Kumtuna huna budi, Asije kupata ufu,
Msiba wake mkubwa, kufiwa na ndege wako.

Kaa naye kwa makini, haja kumtimizia,
Asijeshinda bandani, njaa kumuumizia,
Chakula alie ndani, siyo chini kumwekea,
Ndege akinona nona, ndo utamu utapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…