Akilia sana, karibu kutunguliwa...!

Akilia sana, karibu kutunguliwa...!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Watani habari gani, nawasalimu jamani,
Kumi na moja i ndani, nakuja na hizi ghani,
Limenijia kichwani, wazo hili si utani,
Ndege akilia sana, karibu kutunguliwa!
Akijelengesha tungua!

Nimemuona mtini, ndege kweli chakarani,
Ana mbwembwe kama nini, na rangirangi mbawani,
Sijui ni wa Kingoni, Anaimba kama nini,
Ndege akilia sana, karibu kutunguliwa!
Akijilengesha, chukua

Kafumba macho tawini, na kawimbo mdomoni,
Ndege wenzake mtini, wamenyamaza kwa soni,
Anabadilisha tyuni, kama kasomea fani,
Ndege akilia sana, karibu kutunguliwa!
Akijilengesha pasua

Mwindaji akaja chini, na manati mkononi,
Kaangalia mtini, achague ndege gani,
Mwenye kelele mtini, akamlenga jamani,
Ndege akilia sana, karibu kutunguliwa!
Akijilengesha, kamua

Mara Puh! Ndege chini, wenzake wako angani!
Kisu kikambusu shingoni, kisiwe kibudu jamani,
Kanyonyolewa majini, akatundikwa motoni,
Ndege akilia sana, karibu kutunguliwa!
Akijilengesha nyanyua!

Ndipo nikaja amini, chunguza kwanza mtini,
Yule anojiamini, huimba sana tawini,
Ni kitoweo mtani, cha maakuli jioni,
Ndege akilia sana, karibu kutunguliwa!
Akijilengesha tumbua!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM) – Sauti ya Kijiji
 
huyo ndege anae lia kingoni ndege gani mkuu
 
......
Akijelengesha tungua!

......
Akijilengesha, chukua

......
Akijilengesha pasua

......
Akijilengesha, kamua

......
Akijilengesha nyanyua!

......
Akijilengesha tumbua!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM) – Sauti ya Kijiji


???
 
Mwanakijiji tungua, kwani kajilengesha
nami nishamchukua, aloanza jiegesha
tungua tena tungua, hawezi tena kwepesha
si vibaya kugundua, kilio ni kulengesha
akidondo kungu'ta, na kidonda upulize
 
Mwanakijiji na wewe sasa bwana ! hii lugha gongana
Asante sana
 
eeeh makubwa kumbe dege mwenyewe wa kunyumba?au Mwana unanisema mm?si uniambie tu?au unaogopa kuni................................?
 
Sijawahi kusikia, ndege kuwa akilia,
Ndege zake kuimbia, hakuna kulialia,
Mtini akitulia, sauti nzuri atoa,
Mandege yanayolia, hayo mandege haramu.

Kikaa zake mtini, ndege kwa raha huimba,
Sauti toka kooni, na machoye kayafumba,
Miguu shika tawini, hakika Mungu kaumba,
Vindege vinavyoimba, hakika ndivyo vya kula.
 
asee asprini hapo juu......!

Ndege muone mtini, machoye yapendezea,
Muangalie kwa chini, aimba kwa kurembua,
Akiingia tunduni, kazi kwako kuchukua,
Mandege yanayolia, Labda popo au bundi.
 
Ndege akiimba sana, yu mbioni kutimka!!
Ila akilia sana, mwepesi kukamatika!
 
Mwanakijiji kaopoa kunguru imekuwa tabu mtaani, jee angepata ziwarde!
 
ndege muone mtini, machoye yapendezea,
muangalie kwa chini, aimba kwa kurembua,
akiingia tunduni, kazi kwako kuchukua,
mandege yanayolia, labda popo au bundi.
sasa asprini si ndo huyu sasa....?!
Sasa babu babuka si ndo huyu sasa...?!
Sasa vile anayashuka mashairi si ndo hivi sasa....!?
Sasa vile anaweza ulari wa vina si ndo hivi sasa...?!
Sasa vile anatambaa na mizani si ndo mnaona saasa...?!
 
sasa asprini si ndo huyu sasa....?!
Sasa babu babuka si ndo huyu sasa...?!
Sasa vile anayashuka mashairi si ndo hivi sasa....!?
Sasa vile anaweza ulari wa vina si ndo hivi sasa...?!
Sasa vile anatambaa na mizani si ndo mnaona saasa...?!

hahahaha...busara za Teamo!
 
Ndege muone mtini, machoye yapendezea,
Muangalie kwa chini, aimba kwa kurembua,
Akiingia tunduni, kazi kwako kuchukua,
Mandege yanayolia, Labda popo au bundi.
Twenzetu hommie tukanate na beat..
 
Mwanakijiji asante kwa vina,,,umeniwezesha pia kutambua waliokuwa hawavumi lkn wamo Asprin na Teamo!
 
Back
Top Bottom