Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,626
hiyo siyo sawa ni hatari na ujinga juu.
kuna wengine wanawapa watoto pombe ili walale,kazi kweli kweli.
kwa kweli kama wana uwezo wa chumba kimoja tu lazíma tendo la ndoa wasilifaidi ili kumlinda mtoto,najaribu kufikiria suluhisho nakosa jibu.
Kumpatia mtoto dawa za aina yoyote hata pombe ni jambo baya sana. Hata hivyo tukubali kuwa kuna watu wana mitihani katika maisha yao. Na hapo tunaongelea watoto wa miaka 3, je wanaoishi na watoto wakubwa zaidi ya miaka 10?
Ni vizuri kuacha mambo ya kuhamishia mazingira yetu kwa wengine. Jambo la msingi tukubali tu kwamba kuna watu kwao kila kitu ni shida; hata starehe waliyopewa na Mwenyezi Mungu wanaipata kwa kuibia!