Akina baba tuweni makini sana!

Nguvu moja

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2017
Posts
3,371
Reaction score
2,713
Kama kichwa cha habari kinavyosema
Hapo juu twende moja kwa moja kwenye mada.
Utakuta asubuhi sisi akina baba ukitaka kumpa pesa za matumizi mkeo.
Unampa ndani chumbani, mama akitoka pale wewe hapo baba aupo ushaenda kazini huku mama kaivisha chai anawaita "watoto" wanangu njooni mnywe chai nimewaandalia, baba ukitaka kutoa hela za nguo watoto wanunuliwe pia utatoa chumbani kumpa mkeo, mke atatoka pale chumbani wakati wewe umeenda kazini, mama nae ataenda dukani kuwanunulia watoto nguo za sikukuu anawaita "watoto" wanangu njooni mpime kama zinawatosha vizuri nimewanunulia nguo za sikukuu, wakati wa kulipa pesa ya usafiri was basi la shule hivyo hivyo.
Utampa ndani chumbani pesa akalipie ada ya usafiri wa shule.
Atachukua watoto na kuwaambia wanangu twendeni nikakulipieni ada ya basi la shule, sasa pale mtoto anaweka kumbukumbu na watoto kwa kutunza kumbukumbu ni hodari sana.
Kesho na kesho kutwa wanaona huduma zote alikuwa anatoa mama na wala sio wewe baba... Tunatakiwa tuwe makini tunapotoa pesa za matumizi majumbani kwetu.
Akina baba wenzangu hili tusinyanyapaliwe na watoto wetu wa kuwazaa!
 
dah kweli
 
Baba sasha sina hela mwenzio nataka nipake rangi kule saluni kwangu, kwanza j2 twende tukaangalie kile kiwanja chetu cha goba
 
Sijaona tatizo hapo mm
Hahahhaa ila watu mnajua kujifariji kwa mambo madogo sana, kama baba ni responsible watoto wananoti mapema tu, sasa unataka kuweka wakili wakati unatoa? Au unataka watoto wawe mashahiddi
 
Mmh. Nguvu moja sijui umewaza wapi na wewe lol.

Mie naona ni namna wale wazazi watakavyokuwa ukaribu wao na uelewano wao ndani ya familia. Ikiwa kuna maelewano ya kutosha na watoto wao wanawalea pasi makando makando haitokaa itokee kwamba eti wawe na mawazo hayo kwamba sijui huduma zote anatoa mama pekee.

Ukiona mtoto ana mawazo hayo jua kalishwa sumu na Mzazi mmoja.
 
Wanabodi

Nimemuelewa mjumbe, kuwa kuna huduma mbaba anafaa aprovide ryt away sio kupitia mama, mfano; Manunuzi ya nguo, ina cost how much kwenda shop kumchagulia dogo outfit?

[HASHTAG]#Tubadilike[/HASHTAG]
 
Hata ukitolea chumbani...

Watoto automatic wanaijua ni nguvu ya baba...

Kwa sababu mara nyingi kuna msemo wanawake wanaupenda sana kuutamka... "Msubirini baba yenu"


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…