Kweli kabisa usemayo MJ1, Kuna kiini ambacho kinatakiwa kufanyiwa kazi.............manake hiyo kutoa ni matokeo ya mambo mengi sana.
Na hatutakiwi ku-support hata kidogo.....
Lakini kuna changamoto iliyopo katika hili Speaker, Tuache kwanza sababu za kiroho.......ujasiri na neema ambayo mtu anaweza kuwa nayo wkati anapita katika hayo majaribu na akiweza kushinda anashinda.
Hebu jaribu kumsoma MJ hapo juu vizuri, halafu fikiria uhalisia wa swala zima la utoaji mimba, angalia makundi yote watoto, vijana, wanandoa wasio kuwa na ndoa, wanaobakwa, wanakataliwa.........tena hiyo hiyo historia ya mama yako unadhani ni kwa sababu mama aliweza kukuhifadhi tu? Hapana, mi naona hapa kuna mkono wa Mungu na Neema kubwa sana, USIOMBE kukataliwa na mimba kaka angu.........bila Neema huu wakati ni mgumu sana.