So funny... Yaani wakina dada wote wamekimbilia kusema sio wakina dada WOTE wanaofanya hivyo, na huo ndio ukweli, lakini zikitokea mada za kuwaponda wanaume wanakuwa wa kwanza kushusha lundo la lawana kwa wanaume wote. Mara ooh wanaume wanatudanganya, malaya walevi, n.k.
Ni bahati mbaya sana mambo mengi hapa jamvini tunajadili kama vikundi (Gangs), hakuna independent thinking. Wanawake watasema wanaume wachawi na wanaume nao watasema wanawake wadanganyifu, kwenye siasa ndo usiseme, hata dini zinalazimishwa ziingie. Tukubali kwamba hakuna tabia za kikundi, kuna tabia za individuals kulingana na malezi waliyokulia.
Kama mtu una masahibu yamekukuta, just share the story, usikimbilie kulaumu wanawake wote au wanaume wote. Kwa jinsi watu wa jinsia moja wanavyowasema vibaya watu wa jinsia nyingine, unajiuliza kama hapa kuna mtu MAMA yake ni MWANAUME na BABA yake ni MWANAMKE!